Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
TUJIANDAE KUVIPOKEA VYOMBO VIKUBWA VYA KIMATAIFA
Na Elius Ndabila
0768239284
Juzi Rais wa Tanzania, Samia Suluhu HASSAN amewataka viongozi wakuu wa sekta na taasisi za umma kujipanga kuupokea ugeni unaotumia vyombo vikubwa vya habari vya habari watakaokuja kuitangaza Tanzania.
Alisema ugeni unakuja baada ya kuvutiwa na Tanzania kuwa na Rais mwanamke na wanataka kumtangaza kiongozi huyo na Taifa lake.
Jana tukiwa kwenye mjadala mkubwa kwenye group letu pendwa la Global Politics in TANZANIA nilijaribu kuandika misamiati mitatu ambayo nilikuwa ninajaribu kuchokoza mjadala kutokana na maneno ya Mhe Rais. Kuna watu hawakuelewa na kunifuata inbox. Sasa kwa manufaa ya wote nilisema hivi:-
Kwenye soko la Biashara kuna misamiati mikubwa miwili ambayo huwezi kuiepuka unapotaka kufanya Biashara, hasa kipindi hiki cha utandawazi. Huwezi kuiepuka Brand na Market.
Unapofanya brand unakuwa unaitangaza bidhaa YAKO ili ifahamike kwa wahitaji. Unapaswa kuitangaza sana mpaka iwakae watu kichwani. Kitendo Cha kutangaza ni kufanya brandaring. Ukisha kuitangaza KAZI inayofuata ni kufanya marketing. Yaani kutafuta masoko ni wapi kunauhitaji wa bidhaa yangu?
Hata Hivyo ukianza mauzo ukaona bado bidhaa inasua sua kuuzika unaweza kufanya RE-BRAND yaani kuitangaza upya.
Sasa ukirejea kwenye maneno ya Mhe Rais kuwa vyombo vikubwa vitakuja kuitangaza Tanzania ni kufanya REBRAND kwa kuwa Tanzania ipo toka zamani.
Lakini unapokuja kwenye Uwanja wa siasa ya Duniani, utakuja kuona Rais hakuzungumzia Biashara kama nilivyokwisha kuelezea kwenye aya hizo hapo juu, Rais anamaanisha Uwanja wa Diplomasia.
Maneno ya Mhe Rais kuwa vyombo vikubwa vitakuja ili kumtangaza kiongozi na nchi inaonyesha wazi kuwa kuna mahali kama Taifa hatukuwa Sawa SAWA. Hivyo vyombo hivyo vinakuja ku clear doubt kuwa Tanzania ni salama na haipo kama huenda ulimwengu ulivyokuwa umeamini. Hivyo kwa lugha ya kibiashara wanakuja kui Rebrand Tanzania kwenye uso wa Dunia.
Tanzania siku miezi kadhaa huko nyuma iliingia kwenye migogoro ya kurushiana maneno na mataifa Makubwa, lakini pia hata jirani zetu hususani Kenya. Kitendo hicho cha kurushiana maneno ndicho ambacho kinaweza kuwa kiliitoa TANZANIA kwenye ubora wake wa Diplomasia ya nje. Vita dhidi ya Corona nayo ilikuwa ni mgogoro Moja wapo.
Rais SAMIA baada ya kuingia madarakani alisema Tanzania siyo kisiwa na hatuwezi kuijenga nchi pekee yetu.
Hivyo tafsiri ya vyombo vikubwa kuja ni kuja kuitangaza Dunia kuwa TANZANIA ni salama na ipo tayari kutii makubaliano yote ambayo imesaini mikataba.
Somo la kujifunza hapa si tu kumaliza mivutano na nchi zingine, lakini pia ni kuwa vyombo vyetu vya habari vya ndani vimeshindwa kuisaidia nchi.