Teknolojia zimetoa mchango mkubwa kwenye mapambano ya China dhidi ya janga la virusi, hasa kwenye kipindi ambacho inakuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.
Vyoo vya kisasa vinavyohamishika vimekuwa sifa maalumu ya mfumo wa mzunguko uliofungwa kwenye michezo hiyo, na waandaaji wa michezo hiyo wamesema vimekuwa nyenzo muhimu katika kuzuia maambukizi ya virusi.
Mfumo kamili unaweza kutumiwa kwa ishara ya mkono tu, bila kugusa chochote. Baada ya mtumiaji kuondoka, kifaa cha kunyunyiza dawa za kuua virusi kilichoko ndani kinaanza kufanya kazi kwa kujiendesha, ili kupunguza hatari ya kuambukizana.