desmond3076
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 279
- 184
Hali ya vyoo vya stendi ya mabasi ya Bweri katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ni ya kutisha. Vyoo hivyo ni vichafu, vimejaa, na masinki yameharibika, huku kukiwa hakuna maji kabisa. Pamoja na changamoto hizi, mamlaka husika zimeendelea kukusanya mapato bila kuchukua hatua yoyote ya kuboresha hali hiyo.
Hali hii ni hatari na inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. Ni muhimu viongozi na wahusika wachukue hatua mara moja, kwani ni miezi kadhaa sasa bila mabadiliko yoyote.
Hali hii ni hatari na inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. Ni muhimu viongozi na wahusika wachukue hatua mara moja, kwani ni miezi kadhaa sasa bila mabadiliko yoyote.