KERO Vyoo vya treni ya SGR (Ordinary) vimeanza kuharibika, hakuna hatua zinazochukuliwa

KERO Vyoo vya treni ya SGR (Ordinary) vimeanza kuharibika, hakuna hatua zinazochukuliwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ustaarabu upon ukanda wa kaskazini TU.. . Like deluxe japo linna umri mkubwa hukuti choo kimeharibika au kiti kimechanika ... Huko Kwa washamba train mpya kabisa tayari vyoo vibovu. WALIOHARIBU NI KENGE WA CCM.
 
Watatumiaji ni tatizo, tumeshuhudia ktk miundombinu kama viwanja vya michezo. Tumekuwa watu wa kuharibu, ustaarab ni janga kubwa na lina tutesa huku tukitafuta wakumtupia lawama
 
Mfano, ingia behewa namba 7 kwenye treni ya ordinary uone jinsi vyoo vilivyoharibika na ni zaidi ya mwezi sasa hakuna hatua zozote.

Huu ni mwanzo wa kuiua treni yetu.
Nimejaribu kuingia behewa namba saba nimeshindwa kuliona.
 
Hivi nauli kutoka Dar kwenda Dom ni Bei gani wakuu?
Upatikanaji wa Tiketi zake ikoje?
 
Ndio miradi ya serikali hiyo. Huwa haina ukarabati. Basi za mwendokasi camera zinaning'inia kama bulb na wahusika hawajali. Wanachojua ni kuweka mafuta gari itembee tu. Kwenye treni nako mambo yanaenda kuwa hivyo.
 
Wawekwe "monitors" kuchunga maeneo kama hayo.Akipatikana kenge anafanya uchafuzi au uharibifu ni mahakamani kwa kukiuka misingi ya afya/uhujumu uchumi.
 
Ukweli tuna WAJINGA wengi sana tena waliopita shule kabisa
Ukiangalia baadhi ya miundo mbinu yetu inavyoharibiwa hadi unaona aibu kuwa, mtu aliyesoma hadi darasa la Saba na wengine hadi kidato cha nne nk anawezaje kufanya hayo? Watu wanachafua vyoo bila kujali anayehitaji kutumia choo baada yake, wanavunja koki, wanaharibu miundombinu ya maji, Ni AIBU, AIBU, AIBU SANA!
 
Mfano, ingia behewa namba 7 kwenye treni ya ordinary uone jinsi vyoo vilivyoharibika na ni zaidi ya mwezi sasa hakuna hatua zozote.

Huu ni mwanzo wa kuiua treni yetu.
Mbona hayo madogo vipi tunavyoliuwa taifa letu taratibu huku tukichekelea?Kwa manufaa ya siku,wiki,mwezi au miaka mitano?
 
Hamfai kuwa na vyoo public period
Waambieni muwe mnachimba dawa kama mabasi tu
La sivyo mtaondoka na maradhi
 
Back
Top Bottom