Hakika ni jambo la aibu,dhihaka,ujinga na kukosa ustaarabu na wakati huo huo tukijiona jamii yenye ustaarabu na Elimu.
Maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu,wenye kutafuta huduma au kupatiwa huduma mfano zahanati,vituo vya afya,hospitali(wilaya,mkoa na rufaa), Taasisi za Elimu(shule za msingi, sekondari,vyuo vya ufundi,Kati na vyuo vikuu),Vituo vikuu na vidogo vya mabas,Masoko n.k
Ukibahatika kutembelea maeneo hayo kwa shughuli mbalimbali unaweza kubanwa na haja kubwa au ndogo,hivyo basi lazima uhitaji huduma ya choo iwe ya kulipia au bure.
Kilicho fanya niandike Uzi huu ni hii,sijui niite tabia au desturi ya kipumbavu kabisa ambayo ilipaswa kufanywa na watu wapumbavu,maana mtu mwenye akili timamu hawezi Weka huduma choo iwe ya bure au kulipia alafu akashindwa kuweka Sabuni au toilet paper.
Mfano mtu akijisadia haja kubwa anaweza tumia maji au toilet paper,kiafya inashauri baada ya kukataa gogo,mtu huwa na machaguo mawili atumia maji au toilet paper na baadaye kunawa mikono kwa maji Safi na sabuni.
Sasa inakuaje maeneo ya umma mengi yana vyoo,lakini hakuna Sabuni na Toilet paper ? Na mbaya zaidi Kuna taasisi muhimu zenye jukumu la kutoa matibabu kwa watu,lakini ukienda kwenye vyoo hakuna Sabuni Wala toilet paper na Kuna wakati hata huduma ya maji hakuna kabisa.
Jambo hili hata mwandishi wa habari bwana Denis Mpagaze katika kitabu chake cha "Wasomi Huru Gerezani" anashangaa taasisi kama vyuo vikuu kukosa Sabuni kwenye vyoo.
Jambo hili lina kera na linafanya jamii yetu ionekane kituko kwa jamii zenye ustaarabu.
Rai yangu kwa serikali,umma na mtu binafsi,tubadilike.