Vyoo vyetu vya enzi hizo, lakini ajabu hakujakuwa na magonjwa ya UTI tofauti na sasa

Vyoo vyetu vya enzi hizo, lakini ajabu hakujakuwa na magonjwa ya UTI tofauti na sasa

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Vyoo vyetu vya enzi hizo, lakini ajabu hakujakuwa na magonjwa ya UTI tofauti na sasa
1730959251638.jpg
 
Choo cha kudumbukiza kupata UTI ni ngumu sana, hadi uambukizwe kwa njia ya ngono.

Vyoo vya kisasa ukiflash, kuna maji huwa yanatuama pale kwenye tundu. Ukikaa au kuchuchumaa kujisaidia, ukishusha mzigo kama sio mlaini huyapiga yale maji na kukurukia sehemu za siri. Na kama kuna maambukizi basi utayapata.

Nandio maana ni vema kujaza povu zito kabla hujakitumia ili ikishusha mzigo uzame povuni.
 
Vyoo vyetu vya enzi hizo, lakini ajabu hakujakuwa na magonjwa ya UTI tofauti na sasaView attachment 3145857
Mzigo unaenda moja kwa moja chini na baadaye humwagwa majivu humo humo UTI haichomoi. Kutumia maji ni optional lakini wengi tulitumia gazeti, majani n.k. alimradi umejiweka safi.
Lakini hivi vya kileo (sasa) vinatumia maji kwa wingi, sabuni HALAFU ni wet muda wote. Hapo UTI inastawi 24/7. Mbaya zaidi tena wakati wa "Huduma" unachuchumaa au unaketi. Ukichuchumaa mzigo husababisha "splash" Ukiketi ndo balaa unagusa majimaji yaliyorukia pembeni mwa sahani (sink).
Vyoo hiyo vya kisasa HAVIFAI kabisa kutumika kwenye public e.g. Stend za mabasi, Makanisa, Misikiti, Hospitali/Zahanati, Mashuleni, Kumbi za starehe, Guests n.k. kwa sababu hapo watumiaji ni wengi na kila mtumiaji ana mapungufu yake kiustaarabu, Usafi, uelewa au ni mgonjwa wa UTI. Kiwango cha Usafi sio cha kuridhisha kabisa ni ulipuaji. Ukweli ni Vyoo hivi vinachangia pakubwa sana usambaaji na kuambukizana UTI, Candidiasis (fungus hatari ukeni) na Balanitis kwa wanaume.
 
U.T.I sio ugonjwa wa maabara kweli, maana umeshika kasi wadada, wamama, wasichana wanateseka kweli na madawa yake makali hatari, angalau wanaume huu ugonjwa hautusumbui
 
Tena humo ilikuwa ndo makazi ya kudumu ya majoka makubwa kama koboko, kifutu nk.
Sio kweli. Kama Usafi wa kina ukiwa unafanyika nje na ndani ipasavyo ni nadra sana umkute nyoka tena mkubwa ndani ya eneo hilo. Wazee walilijua hilo na walikuwa wanapanda aina ya miti mimea sio rafiki kwa nyoka e.g. omwitanjoka kwa kihaya au maua kaburi (Vinca rosea) kuzunguka hapo.
 
Back
Top Bottom