Vyoo vyetu vya enzi hizo, lakini ajabu hakujakuwa na magonjwa ya UTI tofauti na sasa
View attachment 3145857
Mzigo unaenda moja kwa moja chini na baadaye humwagwa majivu humo humo UTI haichomoi. Kutumia maji ni optional lakini wengi tulitumia gazeti, majani n.k. alimradi umejiweka safi.
Lakini hivi vya kileo (sasa) vinatumia maji kwa wingi, sabuni HALAFU ni
wet muda wote. Hapo UTI inastawi 24/7. Mbaya zaidi tena wakati wa "Huduma" unachuchumaa au unaketi. Ukichuchumaa mzigo husababisha "splash" Ukiketi ndo balaa unagusa majimaji yaliyorukia pembeni mwa sahani (sink).
Vyoo hiyo vya kisasa HAVIFAI kabisa kutumika kwenye public e.g.
Stend za mabasi, Makanisa, Misikiti, Hospitali/Zahanati,
Mashuleni, Kumbi za starehe, Guests n.k. kwa sababu hapo watumiaji ni wengi na kila mtumiaji ana mapungufu yake kiustaarabu, Usafi, uelewa au ni mgonjwa wa UTI. Kiwango cha Usafi sio cha kuridhisha kabisa ni ulipuaji. Ukweli ni Vyoo hivi vinachangia pakubwa sana usambaaji na kuambukizana UTI, Candidiasis (fungus hatari ukeni) na Balanitis kwa wanaume.