kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mpira una wadau wengi wa aina tofautitofauti wenye umri, jinsia, uchumi, kada za siasa, utumishi na hadhi mbalimbali. Kwenye upira wamo hata marais wa nchi. Unapokuwa kiongozi wa timu ya mpira ujue kuwa unaongoza treni yenye mabehewa yaliyobeba wato mbalimbali. Msemaji wa timu huwezi kuongea au kuandika chochote unachotaka kuhusu timu unayoiongoza au kuisemea kwakuwa utaudhi au kusumbua watu wengi sana.
Wasemaji wetu wanajiropokea na kujiandikia tu chochote kama vile anaongelea mradi wake wa kuku waliokufa kwa kideli. Hawana weledi hata chembe kwa niaba ya timu nzima. Unaweza kumsikia msemaji akisema au akiandika leo saa 6 usiku tunashusha majembe, usipitwe, Halafu inafika saa 6 usiku hamna kitu. Huu ni utoto wa hali ya juu uliopitiliza. Kwani msemaji wa timu ni lazima useme hata kama timu haina kitu cha kusema?
Unamsikia msemaji akijiapiza kuwa leo tutamfunga mtu, mwisho wa mechi amefungwa na anaanza kuwakimbia watu wasimhoji, huu sio weledi.
Vyuo vya habari anzisheni kozi fupi za kutoa mafunzi juu ya usemaji wa taasisi, usemaji wa vilabu au usemaji wa familia. sasa hivi ni vuluvulu tu. Kila kiongozi na kila mchezaji akihojiwa utamsikia akianza mahojiano kwa kusema "tunamshukuru Mungu...." kama fashion vile. Mbona inafahamika tu kuwa Mungu yuko kazini muda wote wa uhai wetu, kwanini kila mtu ni..... ninamshukuru Mungu kila siku na kila wakati?
Kuna uhitaji wa mafunzo ya usemaji wa timu, badala ya hili boringo nangai la sasa la vijana wetu. Wanatuboa kwelikweli kiasi cha kupuuza kuangalia Apps na Instagram accounts zao.