Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Ukiinuliwa na Mungu hakuna awezaye kukushusha na kukuvuta nyuma. Hakuna mwanadamu awezaye kuondoa kibali apewacho Mwanadamu kutoka kwa Mungu. Aliyebarikiwa kabarikiwa tu na huwezi kushindana naye hata kidogo. Rais Samia Ni Mbarikiwa na Mwenye Neema ya Mungu Ndani yake .
Ameletwa Duniani kuwa jawabu kwa kero na matatizo ya Watu. Amefanyika Baraka kwa Maisha ya Watu, amekuwa nuru na Mwanga uangazao Maisha ya watanzania. Ni Nyota ya Matumaini katika Macho ya Watanzania,Ni Tumaini la watanzania.
Ni Daktari wa kero na changamoto za Watu. Kila afunguapo kinywa chake huleta uponyaji katika mioyo ya watanzania,kila neno litokalo ndani ya kinywa chake ni faraja kwa Watu. Ni Mama ambaye huchoki kumsikiliza azungumzapo . Ni kiongozi ambaye huzungumza ajenda na maisha ya Watu na namna ya kuyainua na kuyaboresha.
Sasa Dunia imetambua mchango wake ,Dunia imeona kazi zake , uchapakazi wake , umahiri wake wa kiuongozi,utatuzi wa kero za wananchi.
Dunia imejionea kwa macho yake namna wasichana na Mabinti waliokuwa wamekatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali wakianza kurejea shuleni kuendelea na Masomo. Dunia imeona namna Rais Samia akipambana kutokomeza vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma za afya kwa kujenga miundombinu ya afya ,ununuzi wa madawa ,vifaa tiba ,kuajiri watumishi bora wa afya na mengine mengi.
Dunia imeona juhudi na jitihada za Rais Samia kuokoa vifo vya akina mama wanaopoteza Maisha kwa matumizi ya nishati ya kuni na mkaa. Dunia imeona namna Rais Samia amefanya juhudi kubwa kumtua ndoo mtoto wa kike na mwanamke wa kitanzania,Dunia imeona namna Rais Samia ametoa maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana waliokuwa wamekaa mitaani kwa muda mrefu.
Dunia imeona juhudi na jitihada za Rais Samia kupambana na umasikini ,kuboresha mazingira ya biashara,kuvutia watalii na wawekezaji ili kukuza mapato na hatimaye kuongeza pesa za kuwekeza katika maeneo mengine muhimu kama ya Elimu ,afya , miundombinu n.k.
Ndio sababu taasisi na vyuo mbalimbali vinajipanga Duniani Kote kumpatia Tuzi Rais wetu Mpendwa pamoja na Udaktari wa Heshima kwa kutambua kazi kubwa na ya heshima na tukuka iliyofanywa na kutekelezwa na Rais wetu Mpendwa.
Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia Rais wetu na kumshukuru Mungu kwa kutupatia Rais Samia. Tutembee vifua mbele na kwa kujiamini na tuwe na uhakika hakuna mtihani utatushinda kama Taifa tukiwa na Rais Samia. Atatuvusha kila sehemu na kutufikisha salama katika Nchi ya ahadi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.