Vyuo Vikuu fanyeni mchakato wa kutoa Honoris Causa kwa waandishi wa vitabu vya kitaaluma

Vyuo Vikuu fanyeni mchakato wa kutoa Honoris Causa kwa waandishi wa vitabu vya kitaaluma

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Dar es Salaam – Katika kumbi za mihadhara za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kote nchini, majina kama Angela Anselim Kiseku na Astrid Mushemba yanang’aa kama alama ya ubora wa elimu ya juu nchini Tanzania. Hawa ni wahitimu waliobeba tuzo za kimataifa katika uhandisi wa mafuta na jiolojia, wakiwa na alama za ajabu kama vile Moses George ambaye alikuwa na GPA ya 4.9.
images - 2026-05-01T210122.041.jpeg
Lakini, tukiacha shamrashamra na pongezi hizi za mahafali, kuna swali moja zito ambalo halijawahi kujibiwa: Je, nani alitengeneza njia na misingi ya akili hizi?
images - 2026-05-01T210209.182.jpeg

Kabla Angela hajawa mhandisi mahiri, alipita katika kitabu cha "Conceptual Advanced Mathematics" cha Petro Mayombya wengine walipenda kukiita Mayombya I au Mayombya 2.
images - 2026-05-01T205919.140.jpeg

Kabla Astrid hajajua siri za miamba, alilala na kuamka na vitabu vya Respicus Rwehumbiza na Zisti Kamili. Hawa sio waandishi tu; ni wasanifu wa fikra za Watanzania.
images - 2026-05-01T210302.021.jpeg

Kwa sasa Shahada za Uzamivu za Heshima (Honoris Causa) kiukweli hazina tena heshima, kwani wanapatiwa watu ambao hawana heshima tena. Sio jambo la kushangaza kuona Shahada za Uzamivu za Heshima (Honoris Causa) mara nyingi zikitolewa kwa wanasiasa, ama wafanyabiashara wakubwa.
images - 2026-05-01T210251.603.jpeg

Lakini, ni wakati sasa kwa vyuo vikuu kama UDSM, UDOM, MUST na SAUT kutazama upya vigezo vyao. Kumpa Mayombya au Nelkon (ama familia yake) Shahada ya Heshima ni kutambua kuwa "elimu ya juu haianzi getini mwa chuo, bali inaanza katika kurasa za vitabu vilivyojenga msingi wa vijana hawa"
images - 2026-05-01T210338.493.jpeg

Kutoa tuzo hizi kwa waandishi hawa wala sio hisani, bali ni mkakati bora wa kitu kinachoitwa "Institutional Branding".

1. Utambulisho wa Kimataifa: Chuo kinachomtambua wandishi kama Green, Stout & Taylor katika kitabu chao cha Biological Science ni heshima kwa dunia ya madaktari na pia chuo kinajipambanua kama kitovu cha taaluma kinachoheshimu sayansi ya msingi, jambo linalovutia mashirika ya kimataifa kama UNESCO na wadau wa utafiti.
818Ds+7m-iL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg

2. Uhusiano wa Kiwanda na Shule: Hatua hii itajenga daraja kati ya vyuo vikuu na sekta ya uchapishaji. Mashirika makubwa yataona kuwa vyuo vyetu vinathamini mnyororo mzima wa thamani wa maarifa.
images - 2026-05-01T205756.038.jpeg

3. Kivutio kwa Vipaji: Wanafunzi bora watatamani kujiunga na chuo ambacho kinaheshimu "walimu wao wa kwenye karatasi." Sio ajabu mkiwaheshimisha kina Mehta & Rohit Mehta mtapata wahindi wengi wakija UDSM au UDOM kuomba kusoma taaluma kama kuonesha shukrani.
s200_respicius.rwehumbiza.jpg

Ikiwa chuo kinaweza kumpa heshima kiongozi kwa ajili ya ushawishi wake wa kijamii, kwanini isimpe Mehta & Rohit Mehta ambao wametatua matatizo ya "Physics" kwa mamilioni ya vijana?
14580341.webp

Ni wakati wa kuleta mapinduzi ya kifikra. Vyuo vikuu vyetu vitumie fursa hii kujitofautisha. Kuwatuza waandishi hawa ni kutangaza kwa dunia kuwa Tanzania inaheshimu Mshumaa unaowaka ili wengine waone. Huu ndio wakati wa kugeuza heshima kuwa alama ya kudumu ya kitaaluma.
 
Back
Top Bottom