Pang Fung Mi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2022
- 6,653
- 13,919
- Thread starter
-
- #21
Hawana pesa maisha yao ni mshahara tu kwa walio wengi 90%+ sasa hao si misukule tu, kuna pesa benki zimelala wao wanajenga Nyumba za kuishi badala ya kufungua hardwares stores na miradi mingine, unaeezaje kukopa milioni80-100,-150 unaenda kuizika hizo si akili za misukule. Hivi unajua 150M ni sawa na kununua Shamba la ekari ngapi na ukapanda miti kwenye hekari zote?Punguza dhara kwa kazi za watu. Unaita ualimu wa chuo kikuu ni sawa na msukule?. Please.
Hali tete, japo ubunifu wenye dhamira ya kuongeza mapato ya vyuo ni muhimu ukahimizwa sana,Kumbe Ndiyo maaana vingine vipo after business badala ya kuzingatia ubora wa elimu?
Yaani wanawafata watu maofisini wanaokota vilaza wenye elimu ya kuungaunga yaani duuh.
Ilimradi wapate hela kwa njia ya ada.
Waziri mwenyewe muongo muongo. Toka aliponusurika kuangushiwa jumba bovu la heslb, ameisusa hiyo wizara.Waziri mwenye dhamana hajui haya au ndio kisa wao wanajipa kipaumbele
Hali tete, japo ubunifu wenye dhamira ya kuongeza mapato ya vyuo ni muhimu ukahimizwa sana,
Maprofesa wanakosa karatasi?, ni vema wakakatwa mishahara yao ili kununua karatasi kwa kuwa moja ya chanzo kikuu cha mapato na projects zilizoandikwa na walimu, aidha, ndicho chanzo cha wao kupanda vyeo na kupata marupurupu-------- sasa kwanini vyuo vikose fedha za kujiendesha????Niende moja Kwa moja maada, habari kutoka kwa wahusika, hali ya kifedha vyuo vikuu Tanzania so njema, inasemekana, ndaki, skuli, idara toka mwaka jana mwezi Juni hawapati pesa za uwendeshaji, mathalani hata karatasi tu za kuchapishia mitihani ya mazoezi ni shida tu, je hazina na Waziri wa elimu na wakurugenzi wanafahamu hilo, Rais wa nchi anajua hilo, waziri mkuu anajua hilo?
Mamlaka husika amkeni hali ya kifedha vyuo vikuu vya Umma si shwari, vyuo vingi hicho mnachoita OC/ sijui mapato ya ndani hawana kuhimili mzigo wa uendeshaji.
huko nako hali mbaya nasikia wanakaa mpk miezi sita awajalipwa posho zaoMorogoro SUA na Mzumbe sio
Sua ya zamani na sasa hivi ni tofauti,kwa sasa kile sio chuo kikuu ni sehemu ya kufoji hela za umma.Zamani vyuo kama SUA vilikuwa vinapata pesa nyingi za miradi ya wafadhili, labda kwa sasa mabeberu wamepunguza ku support projects hadi waanze kufikiria OC.
SUA iache uvivu. Pale mjini wana ekari elfu 3, badala ya kuzitumia kulima mahindi, mtama na mazao ya aina hiyo wao wanaendekeza kujenga bar na guest house.Hao ndio habari hii inaweza kuwa ni mfano, chukua tahadhari, hao SUA ndio wako ICU serikali itume timu yake hapo.