A
Anonymous
Guest
Vyuo vya kati vya afya havina usimamizi wa kutosha kutoka taasisi husika kama NACTVET na mabaraza ya taaluma ikiwemo TNMC, MCT na Pharmacy Council.
Miongozo ya elimu inaelekeza kuwa wanafunzi wa ngazi ya diploma wanapaswa kufundishwa na wakufunzi wenye elimu ya kuanzia shahada (Bachelor Degree), lakini baadhi ya vyuo vina wakufunzi wenye kiwango sawa cha elimu na wanafunzi wanaowafundisha.
Mfano baadhi ya Wakufunzi wenye Diploma ya Uuguzi na Ukunga kufundisha wanafunzi wanaosomea diploma hiyo hiyo, jambo linaloathiri ubora wa mafunzo na ujuzi wa wahitimu wanaoingia kwenye soko la ajira.
Pia, baadhi ya vyuo vinaajiri wakufunzi wenye sifa ndogo ili kupunguza gharama, hali inayoweza kuathiri ubora wa huduma za afya kutokana na wataalamu kutopata mafunzo yanayokidhi viwango vinavyohitajika.
Tunazitaka taasisi za usimamizi kuongeza ukaguzi na ufuatiliaji wa vyuo ili kuhakikisha miongozo ya taaluma inazingatiwa na ubora wa wataalamu wanaozalishwa unaimarishwa.