Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?

:coffee::coffee::coffee::coffee::coffee::coffee::coffee::coffee: najinywea maziwa mie nsije nikafa kwa sumu ya mchana!!! lols!!

wapi Dinazarde!!!...???:focus:.:welcome:

Weee muraa umemariza maziwa rote !!!!nipo muraa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu acha changanya mambo,huwezi linganisha shule za secondary na vyuo,hao wanaofanya vizur shule binafsi secondary wengi wao wanasoma vyuo vya serikari kama udsm,muhas na sua,thats wrong comparison


Hivi kwanini hutaki kuacha hii tabia?
 
[/COLOR]
-shule za serikali form one zinachukua wanafunzi walio na ufaulu wa juu na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaokosa kuchaguliwa kwa sababu ya marks zao kuwa za chini wanaenda kujaribu bahati yao private.

-matokeo ya form two necta yakitoka shule za private pamoja na kwamba ziliachiwa wanafunzi wengi wenye marks za kawaida zinaibuka kidedea dhidi ya shule za serikali ambazo zilichagua wanafunzi wazuri tu

-matokeo ya kidato cha nne yakitoka shule za private zinafanya vizuri tena kuliko za serikali pamoja na kwamba shule za serikali zilichagua wanafunzi wazuri
-UBORA WA WANAFUNZI WA CHUONI UNAPATIKANA KWA VIGEZO VIPI HASA?

kwa hiyo udsm inapata request nyingi sana na wote tunajua utaratibu wa kuchagua ni kuanza na aliye bora zaidi kushuka chini,japo nao udsm wanaangalia sana matokeo ya six na ndio mana hawajali sana kama o level uligonga four ama three ya mwisho.

na sababu nyingine ni kwamba udsm ina uwezo mdogo wa kuchukua wanafunzi wanaostahili kusoma degree,na ninawahakikishia kuwa hata wanafunzi wenye div three za 17 wapo eligible kusoma udsm kama tu wana C tatu O level na principle mbili Advance ila kutokana na uwezo mdogo wa udsm ku accomodate wanafunzi ndio inawaacha.



-sababu zilizopelekea hawa wanafunzi waliofeli kufeli hazizingatiwi katika kuangalia ubora wa wanafunzi,mtu katoka shule ya serikali haina hata walimu amekomaa mwenyewe akapata three yake ya 17 alafu unasema hana uwezo wa kupata GPA ya 4.5 kumbe anao uwezo kama akifundishwa na kupewa kila kinachostahili. na wanapofika vyuo vya private elimu inaonekana kumbe ni nyepesi maana wanafundishwa vizuri,sasa kwa ni nini wasifaulu na kupata GPA ya 4?

ngoja nitoe mfano mmoja,kuna shule moja kali ya private arusha nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni sister(katoliki) na yeye ndo alikuwa mkuu wa shule ile,ilikuwa kipindi cha kuchagua wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza.
kwa kuwa ananiamini sana akaniambia nisahishe mitihani ya kiingereza nikakataa,baadae akaniambia nisahishe ya hesabu nikakataa ila akanilazimisha,ikabidi nikubali,nikasahisha na marks za wanafunzi wote zikawa tayari.

sasa vigezo vya shule ile kuchagua wanafunzi ndio vilinishangaza ila nikajifunza kitu baada ya kuelekezwa.



[/QUOTE]

Ukweli ni kwamba vyuo vya private vipo ambavyo vinawaanda wanFunzi vizuri kabisa lakini jamii ya kitanzania kwa upande wa elimu ya juu wana imani na vyuo vya serikali zaid kuliko vya private. Tofauti na ilivyo kwa elimu ya sekondari.
Wanafunzi wa sekondari za private waliofaulu ni nadra sana kumkita chuo cha private ndio ujiulizesekondar mzazi alipambana mwanae asisome govt bt chuo vice versa. Mfumo wa upataji walimu wa chuowanabebwa the best je skondari ikoje?
 
hoja hii sikutaka kuichambua kwa sababu ya kuchosha wasomaji, ninaelewa mambo mengi sana katika misingi ya hoja nyingi ambazo nyingi hazizungumzi ukweli bali ni imani.

nitaeleza kwa kifupi sana ila nikilazimika naweza kutoa maelezo ya kina kwenye hoja yako.

1.kwanza watanzania wengi ni maskini na hakuna anayependa kuendelea kuwa maskini.

2.pili wazazi wengi wanaosomesha watoto wao shule za binafsi si watu tajiri ila wengi wana maisha ya kati kama walimu,manesi,wakulima,wafugaji nk. ila tofauti ni kwamba hawa wanakuwa wanaelewa umuhimu wa mtoto kusoma shule nzuri. na wazazi wengi sana wanajitahidi sana kutumia nyenzo zote ili angalau mtoto afikie kidato cha sita na baada ya hapo mzazi anajua mtoto wake atapata kusomeshwa na serikali chuo kikuu na hivyo mzazi hatakuwa na mzigo tena.

kwa taarifa tu ni kwamba wapo wazazi wengi sana wanafilisika kisa kumsomesha mtoto O level peke yake na akishindwa kufaulu kwenda serikalini wazazi haohao wanakuwa hawana tena uwezo wa kumpeleka private mtoto yule kwa sababu kama ni mashamba wameuza yote. wengine wanakuwa na nguvu ya kiuchumi inayoishia form six ambapo familia inakuwa haina tena uwezo wowote wa kuchangia hata kiasi kidogo cha ada ya chuo.

hoja yangu hapa ni kwamba wazazi wengi na hata wanafunzi ni maskini na malengo yao ni kutafuta unafuu wa gharama chuoni ambapo serikali inatoa mkopo na si ubora wa vyuo vya serikali ama ubovu wa vyuo vya private ndio hufanya wazazi wengi waseme mtoto wao akasome udsm, na hapa ndipo nilipinga mfumo wa HELSB kupanga asilimia za mikopo kwa kungalia kama mwanafunzi alisoma private=tajiri ama alisoma serikali=masikini, kuna watu wanasomesha private kwa kujikamua na mpaka mtoto anamaliza shule nyumbani ashakomba kila kitu.

ok, nisitoke nje ya hoja yako.

najua kuwa mikopo inatolewa hata vyuo vya private, but how informed the society is? ukweli ni kwamba jamii kwa kiasi kikubwa haielewi kama na wanafunzi wa private wanapata mikopo, hivyo wanaelewa huko mikopo haitolewi alafu kumbuka hapo wanatafuta unafuu wa gharama, unafikiri choice itakuwa nini?

ukweli mwingine ni kwamba ada za vyuo vya private ni kubwa kwa kiasi kikubwa na inapotokea mikopo si asilimia mia linakuwa tatizo jingine na hapo hata wanaoelewa hivyo vyuo wanavikwepa kwa sababu ya gharama. na kumbuka wengine wamemaliza kila kitu huko sekondari.

kihistoria pia inajulikana tangu zamani kuwa chuo unalipiwa gharama na hivyo wazazi wengi wanajua mtoto wao akienda chuo cha serikali anapata nafuu.

MASWALI KWAK
1.wewe wazazi wako wanaelewa dhana ya ubora wa vyuo vya serikali na dhana ya ubovu wa vyuo vya private? mimi wa kwangu hawaelewi na hakuna hata mmoja alishaona hata chuo kimojawapo kati ya vyuo vya serikali lakini huko waliko wanajua kuna chuo kikukuu kinaitwa MLIMANI, je walipotaka nisome mlimani ilikuwa kwa sababu ya ubora ama kwa sababu ndicho chuo pekee walichokuwa na wamezoea kukisikia toka ujana wao?

2. ni watanzania wangapi leo wamebahatika tu kufika na kuona chuo cha mlimani? iwe wamesoma ama walipita tu kama wanatembea? je kwa mkutadha huo ni wazazi wangapi kati ya wengi wanaopenda watoto wao wasome UDSM wana uelewa thabiti na chuo cha mlimani?

ukiniuliza mimi nitakwambia kuwa pamoja na kwamba ni ukweli usiopingika kuwa wengi wa wazazi wanapenda watoto wao wasome UDSM(na si vyuo vya serikali vyote kama hoja yako) UKWELI ni kwamba wengi kati ya hao wazazi hawaelewi chochote kuhusu dhana ya ubora wa udsm kama wengi tunavyofikiria, ila wanajua hicho ndio chuo kikuu na vingine hawaelewi kama ni vyuo sawa na udsm tena wengine hata ukiwatajia UDOM bado hawakuelewi. pia wapo wengi wanataka watoto wao wakasome mlimani lakini hao wazazi hata Dar es salaam hawakuwahi kufika,SO SHORT NI KWAMBA UDSM IS A POPULAR UNIVERSITY IN TANZANIA DUE TO HISTORICAL REASONS. niishie hapa i am not ok hata kupangilia hoja inakuwa ngumu. ila unaweza kutafakari haya maelezo na kama una hoja zingine just raise japo sitajibu sasa my brain is very tired mana kuichambua rasimu ni kazi ngumu na imechosha sana akili yangu.
 
mbona unakuja na maelezo yanayokutambulisha kuwa huna uwezo wa kujenga hoja.

unataka kuniambia hakuna mifano ya watu wa UDSM wenye GPA kubwa wasio na uwezo wa kufanya kazi ama kufundisha? ungekuwa na akili usinge sample out mfano mmoja alafu ukahitimisha, nimeandika na kujibu hoja nyingi sana ambazo hujajaribu kuzichambua kuonyesha mapungufu yake. MIMI binafsi nipo bright sana lakini siwezi kuijtolea mfano ukawakilisha wanafunzi wote waliosoma vyuo vya binafsi, ila ninapofanya hivyo nafanya collective analysis. ukisoma moja ya maandiko yangu niliwahi pia kutoa mfano mfano wa kongamano lililofanyika UDMS 2013 mtoa mada akiwa zito likihusu dira ya taifa ambapo wanafunzi wa UDSM waliochangia walikuwa hawajui kitu na nilibaki nikishangaa maana walichangia hoja za hovyo tofauti na mtazamo kuwa hao walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu walitegemewa kuwa na uelewa mpana na uwezo wa kujenga hoja.

kama haitoshi pia nilitoa mfano wa wanafunzi wa udsm niliokutana nao wakati wa uzinduzi wa documentary ya mwanaharakati na mwanasiasa nguli wa amerika na afrika DR. Walter Rodney siku chache baada ya kongamono la udsm ,kimsingi walionekana hawaelewi hata kiingereza na mbaya zaidi kwa uwezo mkubwa ulikuwa unaonyeshwa na wachangiaji wa kimataifa wakiwemo maprofesa wa nchi mbalimbali ilishangaza kuona zaidi ya wanafunzi 15 waliokuwa wamehudhuria walikimbia majadiliano na akabaki mmoja tu ambaye nae hakuchangia chochote wala kuuliza swali mpaka tunahitimisha majadiliano saa sita za usiku. KWA HOJA HIINAELEWA HATA UDSM YAPO MA-BOGUS PALE lakini siwezi nikahitimisha ubora ama ubovu wa chuo kwa sample hiyo ndogo na kama msomi napaswa kwenda zaidi ya hapo na ndio mana nimechambua mambo mengi sana.

kuhusu ubora wa chuo ndugu yangu pia ni ignorant nyingine inakusumbua na matatizo ya kukariri heading or title of a publication, kama ungekuwa msomaji wa ripoti za ubora wa vyuo wala usingejaribu kujisifia eti unasoma chuo cha nne kwa ubora afrika. sitaki kuelezea ripoti zile ila nakutaka kuanzia sasa wewe mwenyewe uniltee hiyo ripoti hapa inayoonyesha chuo unachosoma ni chuo bora alafu tuzame ndani tusome wote maelezo kama hujakimbia hapa. najua vigezo wanavyotumia ndio maana nakutaka uniltee hapa hiyo taarifa.
 
Wakuu nimefanya utafiti kwenye vyuo vya BINAFSI,,nikagundua kwamba wanagraduate na G.P.A kubwa sana yaani unakuta G.P.A kubwa zimejaa sana ! ! Hebu tujadili wakuu kwa nini hivi vyuo vya PRIVATE wanapewa G.P.A kubwa sana je ni sababu za kibiashara

Jiulize kwanza kwanini shule za sekondari za binafsi watu wanafanya vizuri zaidi kuliko shule za serikalini.
 
Kwani siku hizi ule utaratibu wa Externa Exminers haupo? Kazi yao ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…