Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?

Ngoja nikuambie kitu, Private Universities hata waalimu wao hawana vigezo vya kufundisha University! Nimemaliza chuo cha serikali, kuna jamaa zangu wa3 wote wana GPA za 3.1. mmoja anafundisha SAUT, mwingine MWENGE, mwingine RUCO.. unategemea nini kuajiri wasiojua...Obvious hata mwanafunzi akiandika pumba atampatia marks tu.

Naomba management za vyuo private waangalie kuanzia kwenye kuajiri, wazingatie 3.5 and above!
 
achana nae,lime disco uko linakuja leta tope humu

Wewe vyuo vyenu mnagawa G.P.A kubwa ambayo hata mtu hawezi kuitetea ! kuna jamaa kamaliza TUMAINI ,LL,B na G.P.A ya 4.1 namuuliza viswali rahisi hajui! mensrea,actus reus,mistake of fact hajui kitu
 
Huyu jamaa mleta mada ni wa kuhurumia sana. Nlishamwambia aje huku duniani aone watu tunavyokula bata kutoka hivyo vyuo anavyovidharau. Pita hapa https://www.ethz.ch/en.html pimbi weeee!
 
Hua sina tabia ya kutukana watu lakini wewe inabidi
Hv matokeo gani yanawekwa notice board kunakua na calculation za GPA?? Najua matokea hutoka kwa mtindo wa marks and grade
GPA nenda kwenye saris,aris yako
Acha pumba kijana

Wewee nimekwenda mwenge university nimekuta matokeo kwenye noticeboard miG.P.A mikubwa hadi unaogopa unakuta mtu mwenye G.P.A ndogo ana 3.5
 

Wewee SAUT ,LL,B mnagawa maG.P.A hamna kitu nina ndugu yangu kamaliza LL,B pale ananiambia shule laini
 
naonea huruma sana taasisi zinazojaza watu wa vyuo vya private maana ni matatizo!
Vyuo vya private wanagawa mi G.P.A mikubwa uwezo mdogo
Kwa akili yako ilivyo mbovu usingegusa hapo kwenye link niliyotoa, wanaume tunakamua vitu huku duniani na kutoa madude ya uhakika. Endelea na jukumu lako la kuponda vyuo. Kwa taarifa yako tafuta rank ya hicho chuo nilichokupa halafu linganisha na chako cha MUCCOBS.
 

kumekuwepo na wimbi kubwa la watu na hata mada zikibeza na kutilia shaka uwezo na ubora wa vyuo vya binafisi kiasi cha wengine kuviita majina ya ajabu ajabu.

kwa mkutadha huo nimeona bora niwaeleweshe wote wanaojigamba kwa majina ya vyuo vyao na si ubora wao kuwa elimu waliyoipata bado haijawasaidia na hawajakombolewa na kuwajengewa uwezo wa kufikiria,kung'amua na kutambua ukweli halisi ulivyo na nitawashauri warudi darasani wakasome upya ili wapate uwezo wa kuona mambo kwa usahihi wake.

BACK TO TOPIC.
napenda kuweka wazi ukweli huu na watu waniambie kama ni sahihi kwa wanavyofikiria.

1.mfumo wa elimu ya tanzania kuanzia form one mpaka form six unazipendelea shule za serikali kwa kuzipa nafasi ya kuchagua wanafunzi waliofaulu tu na makapi wanaachiwa ndugu zangu wa private.


-shule za serikali form one zinachukua wanafunzi walio na ufaulu wa juu na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaokosa kuchaguliwa kwa sababu ya marks zao kuwa za chini wanaenda kujaribu bahati yao private.

-matokeo ya form two necta yakitoka shule za private pamoja na kwamba ziliachiwa wanafunzi wengi wenye marks za kawaida zinaibuka kidedea dhidi ya shule za serikali ambazo zilichagua wanafunzi wazuri tu

-matokeo ya kidato cha nne yakitoka shule za private zinafanya vizuri tena kuliko za serikali pamoja na kwamba shule za serikali zilichagua wanafunzi wazuri tu.


MAELEZO HAYA YANATOA FUNDISHO KUWA ELIMU YA SERIKALI SI BORA KULIKO YA PRIVATE NA SERIKALI KAZI YAO NI KUHARIBU FUTURE ZA WATOTO ALAFU WANAWAACHA ILI TENA WAOKOLEWE NA PRIVATE SCHOOLS KIDATO CHA TANO NA SITA BAADA YA KUACHWA.

mimi mwenyewe ni mwathirika maana darasa zima tulikula za uso kwenda form one hakuna hata mmoja aliyepenya,ndipo wanafunzi watano tukaokolewa na private ya huko home na kati ya hao ni mmoja tu ndio alishia form four ila wengine walichanja mbuga mpaka vyuoni.


SABABU ZA UBOVU WA ELIMU SERIKALINI ZINAJULIKANA NA SITAZITAJA ILA ITOSHE TU KUSEMA KUWA SABABU NYINGI ZINAZOATHIRI ELIMU SEKONANDARI HATA KWENYE VYUO VIKUU VYA SERIKALI SABABU HIZO ZIPO NA ZINAFANYA KAZI YA KUPUNGUZA UFAULU WA WANAFUNZI HUKO ALAFU WENYE KUKOSA MAARIFA YA KUFIKIRI WANASEMA WAKIPATA GPA NDOGO NDO ELIMU ILIKUWA NZURI KUMBE WAMEATHIRIKA NA MAZINGIRA MABOVU ZIKIWEMO TARATIBU.

-wanafunzi wanaofeli form four kwa kupata angalau three ya mwisho na four za mwanzo serikali inawaacha ambao wengi wao ni wa shule za serikali na ndio hao serikali ilituambia ndio waliostahili kusoma ilipowachagua form one,hawa wanafunzi inabidi waende private kutafuta bahati yao huko, wengi wao kati ya hawa huwa wanafaulu tena na kuthibitisha kumbe wanaweza kufaulu ila walifeli kulingana na kusoma serikalini na si ajabu tena hawa serikali ikawataka.


KIFUPI NI KWAMBA PRIVATE SECTORS WAMEONYESHA UWEZO MZURI WA KUWAFUNDISHA WATOTO NA KUFAULU NA HAPA HAKUNA ANAEBISHA KWA SABABU WANAFUNZI WOTE WANASOMA KWA SYLLABUS MOJA NA MITIHANI NI ILE ILE ILA TATIZO LINAKUJA VYUONI AMBAPO WATU HAWANA SAME SYLLABUS NA MITIHANI YAO NI TOFAUTI NA NDIPO UNAANZA KUSIKIA MAJINA YA AJABU AJABU KWA HIVI VYUO KISA WANAFUNZI WAKE WANA GPA KUBWA.

mfano wanafunzi wanalundikwa lecture hall ukute wapo 400,humo wapo hawasikii kabisa najua maana wanafunzi wengi wanakimbilia mbele ili angalau wasikie na wakichelewa wanakaa nyuma na kusikia ndo inakuwa utata,wengine hawaelewi lakini hawawezi kusema hawaelewi na inabidi wakaushe tu nk nk alafu wakipata GPA ndogo wanalalamika wanapoona wale wa vyuo vya vitongoji wamepata GPA kubwa wakati wenzao walifundishwa darasani wanafunzi 40 tu,wasipoelewa wanauliza na wote wanasikia,lecturer akizingua ama haeleweki analipotiwa na kubadilishwa ama kutimulimuliwa.


mbona hamsemi mashule ya private yanavyofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa ambapo kuna mtihani mmoja?


ama huko hamuoni kama wanapata one na two wengi na hata one kali kali kiasi hata cha tanzania one wengi kutokea huko?

nini tofauti ya mifumo ya shule za private na vyuo vya private katika ufanisi?nini tofauti ya shule za serikali na vyuo vya serikali katika ufanisi?

mbona pia hamuulizi kwa nini shule za serikali pamoja na kujichagulia wanafunzi wazuri lakini bado zinafelisha badala ya kufaulisha?

ingekuwaje kama siku moja shule za private zichague wanafunzi waliofaulu alafu makapi yaende serikalini?watu wangetoka kweli?haki ya nani itakuwa kiama,naamini hata division four zinaweza kukosa kabisa kwenye necta na wanafunzi wote kubaki na zero.


ingekuwaje kama mfumo wa elimu ungetaka kuwa wanafunzi wa shule za binafisi waendelee kuwa wa binafisi mpaka vyuoni?kwa kuwa wanafunzi wa shule za serikali ndio wanaongoza kufeli je mpaka kufikia form six kuingia chuoni serikali ingebaki na asilimia ngapi ya wanafunzi ilioanza nao na je ingeonekanaje kama ubora ungeangaliwa kwa ufaulu tu kama wanavyofanya watu wetu wenye uwezo mdogo wa kufikiri?hizo one nyingi leo sizingekuwa private universities?



2.udahili wa vyuoni na hoja za wanaosema vyuo vya watu binafisi havina ubora.

-kwanza vyuo hivi vinadahili wanafunzi wenye marks za chini sana mpaka hata three za 17 lakini mwisho wanapata GPA kubwa za 4 na kuendelea(si maneno yangu bali ni hoja ya watu hao)

MAJIBU KWA HOJA HII.

kabla hujafikiri chochote kuhusu majibu kwa hili unapaswa kujua pia kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi hata waliofeli la saba lakini wanaibuka na one?

unapaswa pia kujua kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi wenye three za mwisho na div four kusoma advance alafu wanaibuka na division one na two na hata three kwa combination zote hata za sayansi?


HAPA SITAKI KUPIGIA DEBE SHULE NINAYOIJUA ILA NAJUA KAMA WATU NI WAJASIRI WATAKUJA HAPA KUTOA USHAHIDI KUWA WAO WALIPATA FOUR O LEVEL SHULE ZA SERIKALI ILA WAKAENDA PRIVATE NA KUIBUKA NA ONE AMA TWO YA FORM SIX NECTA NA WALIENDA UDSM AMA UDOM AMA MZUMBE AMA SUA.

UKISHAPATA MAJIBU HAYO NI VYEMA UKAJARIBU KUYAUNGANISHA TENA KWA MATOKEO YA GPA KUBWA ZA VYUO VYA BINAFISI.

JE UMEWAHI KUJIULIZA INGEKUWAJE KAMA VYUONI KUNGEKUWA NA PAPER MOJA KWA VYUO VYOTE?JE PRIVATE WANGEONEKANA MABOYA AMA WANAWEZA?hayo majibu kila mtu anayo yake.

-UBORA WA WANAFUNZI WA CHUONI UNAPATIKANA KWA VIGEZO VIPI HASA?

nimefatilia kwa kiasi kikubwa kwa wenye hoja hizi nikabaini wanaangalia matokeo ya wanafunzi ya kidato cha sita tu huku mengine wakiyaacha kabisa kuyaangalia.

NASEMA KUNA MAKOSA MAKUBWA SANA HAPA NA WATU HAWATAACHA KULALAMIKIA VYUO VYA BINAFISI KWA SABABU YA UFINYU WAO WA KUFIKIRI NA NDIO MAANA NIMESHAURI HAWA WARUDISHWE TENA SHULE UPYA WAKAJENGEWE UWEZO WA KUFIKIRIA.

MAPUNGUFU KATIKA HOJA YA MATOKEO KAMA KIPIMO CHA UBORA WA MWANAFUNZI.
-kwanza matokeo yanayotazamwa na wengi ni ya form six pekee,hawajui kuna wanafunzi wana one na two za form six na wapo udsm ama udom ama mzumbe ama sua ila form four walikuwa na four ama three za kuchechemea na waliokolewa na private, ama hawajui kuna wanafunzi wana three za 17 form six ila wana wana one za single digit O level ila kisa wapo vyu vya kitongoji ni tatizo.

SASA JE TUTUMIE MATOKEO YAPI KUSEMA HUYU MWANAFUNZI NI BORA?TUKITUMIA YA SIX NI MWAKE ATAONEKANA ALIFAULU VIZURI LAKINI TUKITUMIA YA O LEVEL NANI ATASEMA HUYU NI MWANAFUNZI BORA?
swali kwa nini mnatumia hasa matokeo ya kidato cha sita tu na mnasahau kuchukua historia ya matokeo yote mpaka ya form four?

mbona udsm ina watu walikuwa na four O Level ama nacho ni chuo cha kitongoji? NAJUA WATU WATASHANGAA HAPA LAKINI NDIO UKWELI WENYEWE.

KIDOGO NINGEPENDA KUELEZA KWA NINI UDSM INACHUKUA WANAFUNZI WENGI WENYE MATOKEO MAZURI YA FORM SIX.

kwanza udsm ni chaguo na ndoto za wanafunzi wengi kusoma hapo(ila haikuwa mimi) na sababu ni za kihistoria,mpaka leo ndicho chuo kinachojulikana na wengi hasa watu wa zamani ambao ni wazazi wetu kwa hiyo wengi tumejengwa tokea mwanzo kuwa hicho ndio chuo kikuu,ukisema kwingine wazee wanakushangaa sawa na watakavyomshangaa mtu atakaekuja hapa aseme yeye ni engineer wa kemikali mana wao wanajua injia ni yule wa civili engineering tu.

kwa hiyo udsm inapata request nyingi sana na wote tunajua utaratibu wa kuchagua ni kuanza na aliye bora zaidi kushuka chini,japo nao udsm wanaangalia sana matokeo ya six na ndio mana hawajali sana kama o level uligonga four ama three ya mwisho.

na sababu nyingine ni kwamba udsm ina uwezo mdogo wa kuchukua wanafunzi wanaostahili kusoma degree,na ninawahakikishia kuwa hata wanafunzi wenye div three za 17 wapo eligible kusoma udsm kama tu wana C tatu O level na principle mbili Advance ila kutokana na uwezo mdogo wa udsm ku accomodate wanafunzi ndio inawaacha.



-sababu zilizopelekea hawa wanafunzi waliofeli kufeli hazizingatiwi katika kuangalia ubora wa wanafunzi,mtu katoka shule ya serikali haina hata walimu amekomaa mwenyewe akapata three yake ya 17 alafu unasema hana uwezo wa kupata GPA ya 4.5 kumbe anao uwezo kama akifundishwa na kupewa kila kinachostahili. na wanapofika vyuo vya private elimu inaonekana kumbe ni nyepesi maana wanafundishwa vizuri,sasa kwa ni nini wasifaulu na kupata GPA ya 4?

ngoja nitoe mfano mmoja,kuna shule moja kali ya private arusha nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni sister(katoliki) na yeye ndo alikuwa mkuu wa shule ile,ilikuwa kipindi cha kuchagua wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza.
kwa kuwa ananiamini sana akaniambia nisahishe mitihani ya kiingereza nikakataa,baadae akaniambia nisahishe ya hesabu nikakataa ila akanilazimisha,ikabidi nikubali,nikasahisha na marks za wanafunzi wote zikawa tayari.

sasa vigezo vya shule ile kuchagua wanafunzi ndio vilinishangaza ila nikajifunza kitu baada ya kuelekezwa.

-kwanza wanaangalia mwanafunzi katoka wapi?na shule ipi?na kukoje huko?hapa wanaweza kumchukua mwanafunzi hata mwenye marks ndogo kabisa ila ameonyesha uwezo fulani baada ya kuangalia alikotoka na kubaini kuwa huyu katoka eneo ambalo elimu iko chini sana na hivyo atakuwa mzuri ila mazingira ndio yanamfanya asijue. ama wanaweza kumuacha mwanafunzi mwenye ufaulu wa wastani aliyetoka shule bora kabisa japo amefikisha marks kwa kuangalia kuwa amepata marks za kawaida sana pamoja na kuwa katika mazingira bora zaidi na shule bora zaidi.

sister akanipa mfano wa mwanafunzi aliyekuwa form three wakati ule 2012 ambaye ndio alikuwa akiongoza darasani,akaniambia yule mwanafunzi alipata marks ndogo sana ila walilazimika kumchukua kwa kuwa waliona katokea ndani kabisa maporini huko arusha kwa wamasai ambako elimu ni kitendawili na walihisi atakuwa mzuri sema tu huko elimu ni mbovu kupindukia,alipoanza form one wakadili nae kumfundisha english kwa ukaribu zaidi na baada ya mwezi wa sita tu akaanza kuongoza mitihani ya shuleni licha ya mwanzo kuanza na namba za mwishomwisho,aliongoza necta ya form two na hata form three bado alikuwa moto.


NADHANI PIA MMEJIFUNZA KITU HAPA JUU YA UBORA WA MWANAFUNZI KUWA UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA NA HATA UFAULU WA MWANAFUNZI UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA IKIWEMO YEYE MWENYEWE NA MAZINGIRA YA SHULE AMA CHUO

MWISHO NINGESHAURI WATU MJIPAMBANUE KWA MAFANIKIO YENU BAADA YA KUMALIZA VYUO KAMA UBORA WA ELUMU YENU NA SI KULAZIMISHA KUPATA SIFA KISA UMESOMA CHUO FULANI AMA KUMUBEZA MWINGINE KISA KASOMA CHUO FULANI.

tunataka akina Stive Jobs hapa,tunataka kina Newton hapa,tunataka kina Eisten hapa,tunataka kina GALILEO GALILEI hapa na wengine wengi,hatutaki majina ya vyuo ama shule. show your quality of education to innovations and is when we shall appriciate your quality,UNLESS YOU ARE A NORMAL PERSON WITH A NORMAL QUALITY.


 

Unamatatizo ya akili wewe MUCCoBS(SUA) unafananisha na vyuo vyenu takataka
 
huu uzi una ukweli ndani yake.



proud to be government scholar!
 
Wewe vyuo vyenu mnagawa G.P.A kubwa ambayo hata mtu hawezi kuitetea ! kuna jamaa kamaliza TUMAINI ,LL,B na G.P.A ya 4.1 namuuliza viswali rahisi hajui! mensrea,actus reus,mistake of fact hajui kitu

Njoo uchukue hiyo G.P.A kama wanagawa.Naona akili yako imejaa kinyesi.
 
There is elements of truth in this thread, angalia GPA zinazo gawiwa vyuo vya private ni za juu na kudisco ni kwa nadra au hakuna.
unahitaji tu kueleweshwa kwa sababu hujui.

mifumo yote ya taasisi za binafisi kokote duniani ina ufanisi wa hali ya juu sana na wanasimamia kwa kikamilifu na hata uende marekani utakuta private wana ufanisi kushinda taasisi za umma.

wakati unaropoka hivi jaribu kuanzia mwanzo wa elimu mpaka juu ya elimu.

1.shule ya msingi.

ukichukua watoto wanaosoma shule za binafisi na wale wa shule za umma. utabaini haya.

kwanza marks wanazopata watoto wa shule za binafisi ni kubwa sana kwa sababu kila kitu wamefundishwa kwa ukamilifu na wakaelewa,wale wa shule za umma wanapata marks ndogo sana kwa sababu hawajafundishwa kwa ukamilifu na hakuna usimamizi na wengi wao wanakuwa ni wanafunzi wa kubahatisha maana hawaelewi.

lakini unaweza kushangaa huyo wa shule za umma akawa ana akili kushinda wa binafsi lakini kwa sababu hakufundishwa sawasawa ama hakufundishwa kabisa basi hata ukiwapa swali moja huyo wa umma anaanza kujiumauma asijue la kufanya na huyo wa binafisi anafanya kwa haraka sana na kwa usahihi. bisha kama wewe ni mbishi wa asili lakini kama unachangia kwa hoja utakubali ukweli huu

pili,hata ukiamua kuwajaribu watoto hawa juu ya uelewa wao wa jumla katika mambo mbalimbali utakuta hawa wa private wamejengwa katika misingi ya kujua mambo mengi sana ya kidunia na hawa wa umma unakuta hawaelewi nini kinaendelea na kwa kiasi kikubwa wao ni kukariri kwa kwenda mbele.

tatu,unapokuja mtihani wa darasa la saba unakuta hawa wa shule za binafisi wanapata marks za juu mno sawa na marks wanazopata kwenye mitihani ya shuleni na hawa wa umma ndio wengi wanaishia kupata marks za chini na kufaulu kwa mbinde sawa na marks walizokuwa wanazipata kwenye mitihani ya shuleni

KAMA SHULE YA MSINGI WANAFUNZI WANGEKUWA WANAPEWA MITINI YA SHULE ZAO TU kama mitihani ya kuhitimu,BASI BILA SHAKA UNGESEMA YALEYALE KUWA KWA NINI WANAFAULU WOTE AMA KWA NINI WANAPATA MARKS ZA JUU,LAKINI KWA SABABU MTIHANI NI MMOJA HAPA UTAKUWA KIMYA WALA HAUTAKUMBUKA KAMA NA HUKO WANAPATA MARKS ZA JUU KUSHINDA WA SERIKARI

2.sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne.
huku nako hali ni ileile,wanafunzi wa private wanafundishwa vizuri kwa ustadi mkubwa chini ya usimamizi makini,wale wa shule za serikali ndio wanajitafutia wenyewe,kama kuna kitu hakupata ndio basi,hawana mwongozaji,wengi wao hata hawajiaminina darasani wamelundikana kama mahindi,


tofauti yao.

kwanza,wanafunzi wa sekondari shule binafisi wanacover karibu kila kitu kwa wakati sawia,lakini wale wa umma wengine mpaka wanaingia necta form four hawajawahi kusoma kitu,wanaishia kujaza majina tu. kwa hali hii wanafunzi wengi wa private ukikagua marks zao wanapata marks za juu sana hata mashuleni kwao lakini wale wa shule za serikali wanapata marks za chini hata huko mashuleni,kumbuka shule za serikali O LEVEL ndio zinapewa nafasi ya kwenda kuchagua wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba na hivyo wanafunzi wengi wa private walikosa nafasi hizo na hivyo shule za private wanafunzi wengi ni makapi baada ya shule za serikari kuwaacha,MIMI MWENYEWE NI MHANGA,SIKICHAGULIWA KWENDA FORM ONE IKABIDI WANINUSURU NA SHULE YA PRIVATE na ni watano tu tulinusuriwa na wengine hawakwenda kokote kwa kuwa hakuna aliyepenya darasa zima,na nikawa mzuri na baadae moto wa kuotea mbali.


pili,wanafunzi wa shule za binafisi wanaongoza kwa ufaulu katika mitihani ya kitaifa huku wale wa shule za serikali wengi wakioongoza kufeli hata kama wanaakili kwa sababu hawahudumiwa ipasavyo,na kwa KUWA WANAFANYA MTIHANI MMOJA WOTE HAKUNA ANAEPIGA KELELE KUWA MBONA WA SHULE ZA PRIVATE WANAPATA MARKS ZA JUU,LAKINI KELELE ZINAZOPIGWA NI KWAMBA SHULE ZA SERIKALI NDIZO MBOVU ILA WANAFUNZI SI WABOVU,kaangalie marks za mitihani ya mashuleni kati ya watoto wa private na wale wa serikali utakutana na tofauti ileile ya watoto wa private kupata marks za kubwa bila kujali kama walikuwa na uwezo usiostahili hata kuchaguliwa serikali na wale wa shule za serikali wanapata marks ndogo licha ya kuwa ndio waliokuwa na ufaulu mkubwa darasa la saba.


mfano mdogo tu,shule niliyosoma mimi O level haikuwahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja form two kwenda form three kwenye necta ya form two toka nilipoanza shule pale miaka ya 2000s na kuna siku mwanafunzi mmoja wa shule za serikali akaniambia haiwezekani wafaulu wote kila mwaka labda kama mnaiba mitihani,ukweli naujua kuwa shule haijawahi kuiba mtihani ila nikamuacha kwa sababu yeye alisumbuliwa na imani,na mfano mwingine,mimi nina mdogo wangu wa kike palepale niliposoma na uwezo wake ni wakawaida sana,jana ndo kanitumia matokeo kuwa ana wastani wa 77 na kapata A tano,wa kwanza ana 95 na wa mwisho ana 50, na wako 142. hapo hakuna aliyefeli wote wamefaulu.
lakini ukiniambia niweke matokeo ya shule yoyote ya serikali ni aibu,lazima wapo waliofeli ama wamepenya kwa tabu.


tatu,matokeo ya necta form four hakuna anaebisha kuwa kila mwaka shule za private ndio zinafanya vizuri wakati wanafunzi wote wanatumia syllabus ileile na mitihani ni ileile na vitabu ni vilevile na walimu wao wametoka kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo na hivyo vyuo mnavyoviita vya kata


3.advanced level.

kama kuna elimu mbovu niliyopata kuishuhudia ni advance shule za serikali,kama kawaida yao,serikali wanajichagulia wanafunzi wote waliofaulu alafu makapi wanaachiwa tena ndugu zangu wa private,private wanafunzi wao ni wale wa div 3 za mwisho na four,wapo wanaoreseat kabisa,lakini wao ukifika na CCC(C TATU) ZA MASOMO YOYOTE HATA KAMA KWENYE KOMBI INASOMA DFC ama DDF ama CCF nk watakuchukua wanakuumba mpaka unakuja kuapata one,two ama three ya kwenda chuoni.


KWA SABABU NAMI O LEVEL NILIFAULU serikari haikuwa tena na jeuri ya kuniacha,wakanipeleka kwenye shule zao,nilipofika tu shuleni nilichanganyikiwa na mandhari peke yake kabla hata sijaingia darasani,nilipiga simu palepale nyumabani wanihamishe shule lakini ilishindikana,nilisoma kwa tabu sana na mpaka namaliza shule siwezi kusema nilienda advance kufundishwa bali ile shule ni sawa na tu na kituo cha kufanyia mtihani,sitaki hata kusikia serikali na shule zao,pale shuleni nilibahatika kukutana na wanafunzi waliopenya toka shule za serikari ambao kwa idadi walikuwa wachache sana mana wengi tulitoka private schools,wengi wao walionekana kuna vitu vingi sana hawakujua na walifaulu kwa kukariri zaidi hata kama walikuwa na akili nyingi.


nakumbuka matokeo menyewe ya shule ya mtihani wa necta form six yaliwaangusha wengi na wengine wakapata hata zero lakini yote hayo ni kwa sababu,hatukufundishwa,hatukupewa vitabu,yaani ni mwendo wa watoto wa bata wa kujitafutia kila kitu.


matokeo ya form six yakishatoka unakuta watu mpaka wanafunzi wa shule za private walioreseat wamefanya vizuri kwenye shule za binafisi na wale waliopenya na kuchaguliwa serikalini wanaanguka


4.vyuoni

katika vyuo mambo ni yale yale,kwanza ikumbukwe kuwa vyuo vya serikali vimekuwepo muda mrefu sana na vyuo vingi vya private si vya siku nyingi,lakini ni ajabu kuwa kwa muda mfupi sana private wamepiga hatua kubwa sana,si tu katika kuweka miundombinu bali hata katika ubora wa elimu maana hawataki mchezo,sema kinachosumbua watu ni kule kukariri kuwa mtu akisema chuo basi ni mlimani pekee,ama mtu akisema anaenda kusoma engineering basi ni civil engineering,lakini ukimwambia mtu eti nasoma telecom engineering kwa kiasi kikubwa watu wengi mtaani wataona unachukua kitu cha ovyo labda mpaka uanze kumwelewesha taratibu,IMANI NI KITU KIBAYA SANA WAKATI MWINGINE.


NIMETOA MFANO HUMU,shule niliyosoma O LEVEL kuna mwanafunzi kamaliza form six mwaka jana pale,matokeo yake ya o level alipata four ila akafanikiwa kuwa na C tatu katika 4 yake,ikabidi asome pale maana hakuwa na pa kwenda,shule ya private ikamfundisha akawa anapata marks nzuri tu na mpaka necta inafika alikuwa anafikisha wastani wa shule,matokeo yake ya six akafaulu vizuri na sasa yuko tena serikalini wamemchukua kwa kuwa katengenezwa,yuko hapo udsm mwaka wa kwanza,na ndio alikuwa mwanafunzi bora wa mkoa mzima mpaka serikali wakampa zawadi wakati kuna shule kubwa na za muda mrefu za serikali na mashuhuri lakini wanafunzi wake hawakufua dafu kwa huyu,pia shule yenyewe pamoja na kuchukua makapi yote kitaifa ilikuwa ya 17(TUNAPOSEMA SERIKALI HAIFAI WATU HAWAELEWI KUWA KARIBU KILA TAASISI IMEATHIRIKA NA UBOVU WA SERIKALI AMA UBOVU WA MFUMO NA HATA ELIMU HAIWEZI KUWA IMESALIMIKA NA ATHARI ZA SERIKALI KATIKA MATOKEO)


NISEME KWA KIFUPI SANA KUWA SHULE ZA PRIVATE NA VYUO VYA PRIVATE NI SAWA NA TIMU YA ARSENAL,WAO WANA KAZI YA KUTENGENEZA NA KUNOA VIPAJI VYA WANAFUNZI NA KUWAUZIA SHULE NA VYUO VYA SERIKALI AMBAVYO KWA KIASI KIKUBWA NDIO WANAONGOZA KUHARIBU WANAFUNZI ALAFU WANASINGIZIA UBORA WAO WA ELIMU UKO JUU.


Sasa je wote wana uwezo?

IVI WEWE KAMA UMEPEWA KAZI YA KUFUNDISHA 1+1=2 NA WOTE WAKAELEWA UNATAKA WAKIFANYA MTIHANI WAJIKOSESHE ILI WAONEKANE WANATENDA HAKI?this is crazy.
nimesoma O level katika shule ambayo toka ianzishwe miaka ya 1990s mpaka leo haijawahi kupata div zero,unataka wajikoseshe wapate zero?ili iweje?hivi mbona huulizi kwa nini shule za serikali zinachagua wanafunzi wote wenye uwezo alafu zinashindwa kuwafanya wafaulu wote maana hata kabla hazijawachagua wanakuwa wamethibitika kuwa na uwezo.


NI KICHEKESHO SANA KUWA WATU WENGI HAWAWEZI KUNGAMUA.


PRIVATE SCHOOL=wanachagua wanafunzi wao miongoni mwa makapi yaliyoachwa na government schools
GOVERNMENT SCHOOLS=wanachagua wanafunzi wenye uwezo tu na wanaonekana hawana uwezo wanawaachia private.


KAMA UNGEKUWA MDADISI ulipaswa pia kujiuliza kwa nini shule za serikali zenye wanafunzi wote wenye uwezo hawafaulu wote?
pia kwa nini shule za private zinafanya vizuri pamoja na kuwa wanafunzi wengi ni makapi ambao hawakustahili kupata nafasi serikalini?


Kuna vyuo kama SUA, UDSM,UDOM hata ukipata GPA YA 2.5 huyo mtu anauwezo mkubwa kwa kichwa.

acha uongo wewe kutumia majina na si vigezo na ufanisi wa vyuo,mimi mbona kuna watu nimesoma nao shule ya msingi nilikuwa nawazidi uwezo,nikasoma nao sekondari pia uwezo wao ulikuwa chini yangu na hata advance na kwa sababu huku kote mtihani ni mmoja yaani wa kitaifa hawawezi kubisha,sasa kwa kuwa wao waliamua kusoma huko na mimi nikaenda kwingine na mitihani yetu inatofautiana leo unataka kutoa hitimisho kwa kutumia mitihani tofauti???????


hauwezi kuwapima watu kwa kutumia vigezo tofauti,kungekuwa kuna mtihani mmoja wa vyuo ubishi huu nadhani usingekuwepo maana ni wa kishabiki zaidi.


ngoja nikupe mfano mdogo kwa evaluation yangu kuhusu kusifia watu kwa vyuo walivyotoka.
kuna siku nilihudhuria kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere pale udsm MWAKA JANA,mada ilikuwa ni dira ya taifa,huku tukiangazia azimio la arusha,watoa mada alikuwepo zitto na mdada mmoja simkumbuki,
pia alikuwepo Willy Mtunga wa kenya(jaji wa mahakama ya juu kenya,supreme court),KINGUNGE NA WENGINE WENGI.


ilipofika wakati wa floor panel kuchangia,wanafunzi wa udsm walichangia utumbo karibu wote wakionekana walikuwa na uelewa mdogo sana. binafsi nilishangaa sana kwa wale waliokuwepo watanielewa na wasiponielewa nitawaelewesha.


siku hiyo tukapata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa documentary ya mwanaharati na mpigania uhuru DR. Walter Rodney,UZINDUZI uliofanyika kesho yake na documentary ilitengenezwa na Clairemount Chung kutoka JAMAICA.


nilikuwa mwanafunzi pekee ambaye sikutoka udsm,tulipofika mambo yaliendelea,ilipofika wakati wa kujadili ndipo wanafunzi wa udsm walitia aibu,kwa sababu wazungumzaji walikuwa wanajua mambo mengi sana na english yao haikuwa ya mchezo na mada ilikuwa nzuri sana,

ila nilishangaa kuona wanafunzi wa udsm wakikimbia bila hata kuchangia wala kuuliza swali mara tu baada ya mjadala kuanza na alibaki mwanafunzi mmoja tu,binafisi nilichangia walau kiasi na nikaongea na nguli hao wa histoaria japo mimi si mwana arts. kifupi wale jamaa walikimbia na kwa haraka haraka nilihisi kiingereza ndo kiliwakimbiza na uelewa wa wale jamaa maana haikuwa rahisi kuchangia mbele ya watu wanaojua kupitiliza tena wengine maprofesa toka sehemu mbalimbali duniani.

mjadala uliisha saa sita usiku na wanafunzi tulikuwa wawili tu,mmoja wa udsm aliyebaki japo hakuchangia wala kuhoji chochote na mimi.




maelezo haya nadhani nimeyajibia vya kutosha,ila si vibaya nikaongeza kidogo.
huko private ufundishaji wao ni tofauti sana na vyuo vya serikali na usifikiri wanapewa marks.


mfano. udsm unaingia lecture,wanafunzi mko kama mia 500 ama 400 ama 300 lecturer anafundisha kundi lote hili na wanafunzi wake hawaelewi kwa mmojammoja,hapo anatumia microphone,hakuna hata nafasi ya kusema mwalimu sijaelewa,ikipigwa lecture ngumu wanafunzi mnatoka hamjaelewa na hamkuuliza ili mueleweshwe,hapo unategemea uje kupata GPA kubwa wakati hata darasani hupati nafasi ya kuelewa kila kitu?marks zinaanzia hapa kupungua na ukitoka hapo unategemea discussion zikusaidie na ukute hao wanaokusaidia nao kuna vitu wamemiss.


vyuo vya private unakuta darasa limegawanywa kwa wanafunzi 40 ama 60 kila darasa japo kozi ni moja na labda ina wanafunzi 150.
wanafunzi wanafundishwa kwa ukaribu mpaka lecturer anapata nafasi ya kuwazungukia aone wanafanya nini,je wameelewa,pia anakuwa amewakariri uelewa kwa kila mmoja,na wasipoelewa wanauliza na mwalimu anawaelewesha na hata ofisini unaweza kumfata mwalimu akakuelewesha. rejea idadi inayotakiwa kufundishwa na mwalimu mmoja,maana hili lundo kama mahindi lina athari zake na wengi wanaingia tu kama ushahidi,pia serikalini huwezi kumkataa lecturer ambaye numwelewi yaani ni mtindo wa kwenda nae hivyo hivyo,private kama lecture haeleweki mkisema tu anang'olewa na kibarua kinaota nyasi na mnatafutiwa lecturer anaeeleweka.


HAWA WAKIJA KUFANYA MTIHANI KWA VYOVYOTE VILE LAZIMA WAFANYE VIZURI KULINGANA NA WALIVYOFUNDISHWA.


watu ni wabishi tu. maana sijajua kigezo gani wanatumia kusema WANAFUNZI WA PRIVATE hawana uwezo .
hivyo vyuo vya private vina wanafunzi toka hata shule zinazojulikana kama shule za watu wenye vipaji maalumu kama tabora boys,mzumbe,kibaha,ilboru,tena wengine wamesoma shule za vipaji tu kuanzia form one mpaka form six.

KAMA BADO HAUJAELEWA WEWE UTAKUWA NA AJENDA NYINGINE.
 
Jamaa atakuwa ame-cook data bila shaka kwa maelezo yako inabidi arudi field tena
 
vijana pia lazima waelewe kufaulu katika kiwango cha juu haimaanishi kwamba na chuo ndio utafaulu maana kuna ambao wamefaulu kwa kusoma past paper na kukariri (namaanisha kuna ambao wana deal na mbinu za kujibu mitihani tu kuelewa kiundani haimuhusu na kweli wanafaulu na wanapigiwa makofi), kuna ambao wanafaulu kutokana na kuhudhulia darasani kila siku na kuchukua notisi na kujisomea kile ambacho wamejifunza na kuongeza na mengine kama hapo juu) na kuna ambao kutokana na location ya shule zao unakuta source ya material ni mwalimu na vitabu vichache vya shuleni (of course kuna ambao wanafaulu katika kiwango cha juu lakini pia kuna ambao wanafaulu katika kiwango cha kawaida)

Hivyo unaweza ukakakutana na mtu amepata Division 3 kutokana na shule aliyotoka na mbinu alizokuwa anatumia kupata material ukakuta ana afadhari kuliko hata yule aliyepata division za juu kutokana na ukweli kwamba ufundishaji wa chuo ni tofauti na sekondari kwani mwanafunzi ndio anawajibika kutafuta nondo huku lecturer akitoa area of concentration

LAKINI mwisho ya yote A level hata upate ngapi kama O level ulipita kibahati bahati maisha ya chuo yatakuwa magumu kwako kwani nionavyo mie elimu ya O level kwa kiwango flani ina mchango mtu akifika chuo na hata ukifuatilia wanao disco (acha wale kwa chuki binafsi) utagundua wengi wao O level walikuwa wana problem hata kama walifaulu hasa ukizingatia kuna watu huwa wanashituka mwaka wa mwisho kwa kutumia kila mbinu anafaulu but uelewa wa kiundani wa masomo kuanzia form 1 to 4 unakuwa si kivile.

HATA YULE ALIEPATA DIV 3 ANA UWEZO WA KUFAULU PIA CHUO KATIKA KIWANGO CHA JUU KUTOKANA NA HIYO THREE YAKE ALIIPATAJE
 
Ukimaliza chuo hayo maneno utayaona kosa la jinai kutamka mbele ya workmates wako wanaovuta mpunga wa juu kuliko wewe ambao walipitia hivyo vyuo unavyovidharau.

Asante sana mkuu Mshinga kwa analysis nzuri.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi tambua kwamba private universities are business organizations, vinawachukulia wanachuo kama wateja, hivyo basi kama ilivyo biashara zingine mteja ni mfalme lazima anyenyekewe,akarimiwe ili na kesho arudi kusoma au amlete ndugu yake. Kupewa GPA kubwa ni kama vibanda vya vijijini ukinunua mchele anapima kisha anachota kidogo wa kukuongeza,kisha anasema karibu tena. Ukitaka kujua hawa watu wanachongewa GPA fake fanya nao kazi, au kutana nao TP cognition iko below poverty line, haiendani na matokeo asilani. Alie pata GPA ya 3.5 chuo cha serikali kama SUA ni sawa na mwenye 4.5 private university au hata zaidi ya hapo kwa uelewa wa mambo. Najua nitatukanwa lakini ndio hali halisi ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…