Vyuo vya private vyenye ada kubwa vyakomeshwa

Vyuo vya private vyenye ada kubwa vyakomeshwa

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
257
Serikali kupitia TCU iliagiza vyuo vikuu vyenye ada kubwa hasa inayokaribia million mbili kupunguza angalau kukaribiana na vyuo vya serikali ili kupunguza mzigo kwa watanzania.

sasa vyuo vilivyogoma vimepewa wanafunzi wachache hadi huruma, yaani chuo kimoja kishiriki cha Tumaini Makumira wamepewa wanafunzi kama 120 kwa kozi zipatazo 6 kutoka kwenye idadi inayo karibia 1000 mwaka uliopita, binafsi nawapongeza TCU kwa hilo, kwanini utoze ada zaid ya mara mbili ya ada inayolipwa na vyuo vya umma?

Kwa hili TCU nawapongeza kwani maisha ni magumu na wanaotaka mkopo ni wengi.

Asante
 
Ni sawa na kujitekenya afu ukacheka mwenyewe. Hapo hawajapata suluhu. Unavyoshabikia ujue hivyo vyenye ada ndogo havitoshi kubaba idadi ya wanafunzi wote.

Maana yake ni nini? Kwamba mara mia 1000 wakose nafasi za chuo sababu ada ni kubwa afu tuwakomeshe vyuo kwa kuwapa 120 si pumba hivi?

Ukitaka kujua elimu ni ghari jaribu ujinga ndo unachokishabikia wewe.
 
Dawa ilikuwa ni kuwanyima kabisa yaani unashangaa vyuo vya kanisa vinatoza ada kama vile ugomvi yet ikifika kwenye ujenzi wa lecture halls makanisani ni michango kwa kwenda mbele daah ni hatari lakini salam hawa jamaa wanapenda pesa kuliko YUDA ISKARIOTE
 
Dawa ilikuwa ni kuwanyima kabisa yaani unashangaa vyuo vya kanisa vinatoza ada kama vile ugomvi yet ikifika kwenye ujenzi wa lecture halls makanisani ni michango kwa kwenda mbele daah ni hatari lakini salam hawa jamaa wanapenda pesa kuliko YUDA ISKARIOTE

Hapo kwenye michango hakunaga mrejesho wa "divident" wakati waliopewa talanta tumeambiwa kwenye biblia "walipata gawio"
panahitajika mahubiri ya ziada kushawishi.
 
Ni sawa na kujitekenya afu ukacheka mwenyewe. Hapo hawajapata suluhu. Unavyoshabikia ujue hivyo vyenye ada ndogo havitoshi kubaba idadi ya wanafunzi wote. Maana yake ni nini? Kwamba mara mia 1000 wakose nafasi za chuo sababu ada ni kubwa afu tuwakomeshe vyuo kwa kuwapa 120 si pumba hivi? Ukitaka kujua elimu ni ghari jaribu ujinga ndo unachokishabikia wewe.

Umekurupuka..wanachuo wengi sasa hiv wamedahiliwa ktk vyuo vya umma ambako kuna unafuu wa ada na vyuo vingine vya private vyenye unafuu kama vile saut, sioni tofauti ya ubora wa elimu kati ya vyuo vya private vyenye malipo makubwa na vya umma vyenye unafuu wa ada, wewe unadhani ni sawa course moja kuwa na ada ya laki saba serikalini na milioni moja na laki saba private?

Muda wote niliokuwa chuoni sijaona ukubwa wa ada ndio penye elimu bora,labda angalau kwa levo ya sekondari lakini sio chuo kikuu,mi nadhani we ni mdau ktk private hizo,inamaana ww sio muelewa ktk hali ya maisha ya mtz!!

Siifurahii serikali iliyopo madarakani lakini ktk hili wametumia akili...
 
Je mmejaribu kuangalia resources zinazotolewa na hivi vyuo vya private hadi wakaweka ada yao juu hivyo??
 
Hakuna resource za maana sana zinazo lingana na ukubwa wa ada zao kwani mi nimesoma moja ya vyuo hivyo vya private vyenye ada kubwa ndio maana tcu ikawaomba kupunguza ili angalau kila mtz awe na angalau na uwezo wa kumudu gharama hata kama hana mkopo,walipo goma ndio hivyo tena
 
Dawa ilikuwa ni kuwanyima kabisa yaani unashangaa vyuo vya kanisa vinatoza ada kama vile ugomvi yet ikifika kwenye ujenzi wa lecture halls makanisani ni michango kwa kwenda mbele daah ni hatari lakini salam hawa jamaa wanapenda pesa kuliko YUDA ISKARIOTE

kweli kabisa mkuu, hasahasa st.joseph wanatumia hata hela za mikopo ya wanafunz ku run biashara zao students had watishie kuandamana ndio wanapewa fedha zal
 
hakuna cha resources wala nini ada ni kibwa jmni tumaini dar es salaam ada yao ni 2.2m tuition fee only imagine.... bado chuo hakina hostel serikali iangalie vizuri bora mwakani wasipewe kabisa hadi wakubali kupunguza ada....

wanatutesa sana hawa majamaa. halafu ety ndo chuo cha kkkt badala ya kusaidia watu kinawakandamiza. hata Mungu hapendi...halafu cha kushangaza course zote ada yao ni moja..

mtu anaesoma education atalipaje ada sawa na anaesoma law na mass comm na course nyingine??? tumaini dar kimezidi.
 
Ok jamani..swali hapa...pendekezo lenu kwa bachelors kwa mwaka ada iwe shillingi ngapi? Maana nimejaribu kupiga hesabu ya 2.2Mil kwa mwaka for bachelor degree kwa chuo kinachopokea wanafunzi elfu moja...hii hela sioni ikitosheleza kabisaa.

ukitilia maanani masomo kama ya udaktari, engineering (Kilimo included), hata HR..labda naomba wana JF wanipe Mwanga zaidi ya pendekezo ya ada iliyo nafuu.
 
Ok jamani..swali hapa...pendekezo lenu kwa bachelors kwa mwaka ada iwe shillingi ngapi? Maana nimejaribu kupiga hesabu ya 2.2Mil kwa mwaka for bachelor degree kwa chuo kinachopokea wanafunzi elfu moja...hii hela sioni ikitosheleza kabisaa..ukitilia maanani masomo kama ya udaktari, engineering (Kilimo included), hata HR..labda naomba wana JF wanipe Mwanga zaidi ya pendekezo ya ada iliyo nafuu.

Angalau ada isizidi milioni moja
 
hakuna cha resources wala nini ada ni kibwa jmni tumaini dar es salaam ada yao ni 2.2m tuition fee only imagine.... bado chuo hakina hostel serikali iangalie vizuri bora mwakani wasipewe kabisa hadi wakubali kupunguza ada....wanatutesa sana hawa majamaa. halafu ety ndo chuo cha kkkt badala ya kusaidia watu kinawakandamiza. hata Mungu hapendi...halafu cha kushangaza course zote ada yao ni moja..mtu anaesoma education atalipaje ada sawa na anaesoma law na mass comm na course nyingine??? tumaini dar kimezidi.

Tumaini watu wabaya sana yaani hata vyuo vyake vishiriki navyo wana ada kubwa inayokaribia milioni mbili mi napendekeza mwakani wasipo shusha ada wasipewe hata mwanafunzi mmoja....wanafanya biashara hawapo kihuduma hawa
 
angali KIU medicine hadi huruma hivi kwa 6.8m mtu anaweza kuimudu kwa 5yrs?
 
Back
Top Bottom