Vyuo vya Ualimu kuhamia NACTE

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Wanajamvi kuna tetesi kuwa vyuo vya ualimu vitakuwa vinaendeshwa na NACTE.Kama kuna yeyote mwenye kujua taarifa kamili naomba azimwage ili tujue nini kinajiri. Pia ningeshauri kuwa vyuo vya ualimu vinavyotoa diploma ya ualimu vijikite kutoa mafunzo ya kiufundi (kama VETA).Hii ni kwa sababu vyuo vikuu vinavyotoa shahada ya ualimu ni vingi nchini.
 
Tayari imepitishwa rasmi,wakuu wa vyuo wk iliyopita alhamis walisain kukubali kuhamia nacte chini ya Katibu mkuu jijini Dar es salaam.
 
mchome hataki kusikia kabisa hiv vyuo na ukaguz wa shule hta wakurungezi wote walioko wizara ya elimu wanahamia tamisemi,pia mtihani wa form two utakua chini ya tamisemi,wizara inataka kubaki na vyuo vikuu tu,
 
Ni vyuo 6 tu katika vyuo vyote vya ualimu vya serikali.
 
Kuna tangazo pia katika jengo la wizara ya elimu kuwa watumishi watakaobaki kwenye jengo hilo ni 70 tu kati ya 400. Kwa hali hiyo hali siyo shwari wizara ya elimu - makao makuu.
 
ujue pale wizarani kuna watu hawana kazi kabisa kwa mfano kuna mkurugunzi idara ya shule za msingi,mkurugenzi idara ya shule za sekondari,mkurugenzi idara ya elimu ya watu wazima
 
mchome hataki kusikia kabisa hiv vyuo na ukaguz wa shule hta wakurungezi wote walioko wizara ya elimu wanahamia tamisemi,pia mtihani wa form two utakua chini ya tamisemi,wizara inataka kubaki na vyuo vikuu tu,

Duuuh hiyo Kali kweli, kama hataki kila kitu cha elimu anabaki na Vyuo Vikuu tu basi ni vema ikaitwa Wizara ya vyuo Vikuu maana wigo wa elimu ni moans zaidi ya vyuo Vikuu pekee
 
Kuna tangazo pia katika jengo la wizara ya elimu kuwa watumishi watakaobaki kwenye jengo hilo ni 70 tu kati ya 400. Kwa hali hiyo hali siyo shwari wizara ya elimu - makao makuu.

Hiyo itakuwa ni zaidi ya Tsunami, wanatakiwa wawe wameondoka lini Mkuu?
 
hapa tutajua kipi ni chuo bora cha ualimu,walimu wengi walikuwa hawafundishi wakitegemea kutungiwa mitihani na kusahishiwa.walimu vilaza waliopo vyuo vya ualimu wakae chonjo.wataumbuka vibaya ikiwa serikali ijitahidi kuwafanyia ukaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…