Vyuo vya uwalimu vya serikali vinatia huruma

kibila

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
799
Reaction score
554
Wadau mimi naumizwa sana na wizara ya elimu kushindwa kuvisimamia vyuo vyake vya ualimu kwa maana hii vyuo vingi vipo nje ya miji lakini unakuta chuo hakina mazingira mazuri ya kujisomea.

Kwa mfano chuo cha ualimu dakawa hakuna mnara hata wa simu kupiga simu kule ni tatizo majengo nikiimaanisha madarasa hakuna kuna mabaki ya stoo zilizojengwa kwa mabati magumu enzi izo za wakimbizi wa afrika ya kusini ndio yanatumika km madarasa wanafunzi wakati wa joto wanapata shida kwa joto kali hasa wakati wa mchana.

Hakuna internet kama nilivyoeleza awali location ya hivi vyuo sasa mwanachuo anakosa hata kusoma gazeti ili ajue nini kinaendelea huko duniani internet ingewasaidia kupata si taarifa tu hata material ya kujifunzia maana hakuna hata maktaba mana iliyopo hakuna vitabu vya kutosha ni sawa na hakuna tu.

Halafu tunasema BRN hivi hii nchi ina tatizo gani mwalimu huyu ndio tunataka akawafundishe watoto wetu mambo ya TEHAMA wakati yeye mwenyewe hiyo TEHAMA hajui ni kitu gani huu ni upuuzi na ujinga.

Kwa mawazo yangu kwa hali hii hatutakuja kupata maendeleo kamwe kwenye hii nchi wizara inaleta mchezo kwenye mambo ya maana, sasa wanakuja na swala la kkk ooo watoto huko shule za msingi wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika umebuniwa mradi wa kupeleka watu wakapewe semina mm naona ni kutaka kupiga Hera za walipa kodi wa nchi hii bure.

Hivi kweli tatizo ni walimu kukosa ujuzi wa kufundisha au ni walimu wamekosa motisha mishahara midogo madaraja hawaoandishwi kero kibao alafu unategemea uyo mwalimu apoteze muda mtoto wa mtu wkt hajui kwake watakula nini. Viongozi wetu hawana nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi wanachofanya ni ubabaishaji tu.
 


Pole sana mkuu,NADHANI UNA BAHATI MBAYA SANA KWAMBA UMEENDA CHUO HICHO.NIJUAVYO MIMI VYUO VINGI VYA UALIMU VIKO VIZURI LICHA YA KASORO KADHAA.VINGINE VIMEJENGEKA KULIKO HATA UNIVERSITIES KADHAA.MFANO, UNGEENDA MARANGU TTC AU KRELUU, NADHANI UNGEFURAHI SANA.HATA KIGURUNYEMBE,MONDULI, BUTIMBA, MPWAPWA(JAPO MAJI SHIDA), MTWARA TTC.
 
Hata korogwe TTC kipo poa sana
 
Mm sio mwalimu ila najalibu kuleta picha ya madudu yanayofanyika vyuoni
 
Nakupa kazi fanya utafiti mdogo uone ni vyuo vingapi mpaka muda huu vina access ya internet
 
Kwani unakwenda chuoni kupiga simu?

Pole sana wewe ndio aina ya watanzania tulio nao na ndio maana hatuta kuja endelea kwa dunia ya sasa haya niliyosema ni muhimu kuliko ujuavyo Wewe
 
Nakupa kazi fanya utafiti mdogo uone ni vyuo vingapi mpaka muda huu vina access ya internet

Hapo kuhusu internet accessibility, jaribu kufafanua.KWAMBA VYUO HAVINA INTERNET KWA MATUMIZI YAO AU VIPO MAENEO AMBAYO HAYANA ACCESSIBILITY?
 
nenda nachngwea ttc chozi litakutoka walimu wana maisha magumu kuliko tujuavyo
 
kumbe sio mwanafunzi wala mwalimu hapo kwa hiyo ni utafiti tu,asante wamesikia mkuu
 
Labda ni kozi yao inavyotaka wajifunze kukabiliana na site

Yote aliotaja mtoa maada yapo site za hizo kazi esp huko kijijini

Aka mwona mbali
 
Mhhh Yodoki II. Unasifia chuo cha Marangu kwa nje. Vyoo vilivyo karibu na ukumbi wa mikutano unavifahamu? Mabomba yanamwaga maji ovyo, vyoo vimeziba, ili mradi taabu mtindo mmoja. Ni sheeeeeeda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…