Vyuo vya Veta kujengwa kila Wilaya nchini, Wananchi wahaswa kuchangamkia fursa

Vyuo vya Veta kujengwa kila Wilaya nchini, Wananchi wahaswa kuchangamkia fursa

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Imeelezwa kuwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipiga kuwa na Chuo kila Wilaya nchini ili kusogeza karibu fursa ya wananchi kupata ujuzi ambao utaweza kuwawezesha kujiinua kiuchumi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, wakati akihutubia katika kufunga kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Agost 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.

aeb4d83c-7546-4289-a82a-c8085ce6fedf.jpeg
Prof. Mkenda amesema kwamba katika jitihada za kuongeza ujuzi Serikali ina mpango wa kupeleka vyuo vya Veta kila mkoa ili kutanua wigo wa kuwezesha wananchi ikiwemo Watu wazima kupata ujuzi ambao unaweza kuwasaidia kujiinua kiuchumi.

Afisa uhusiano VETA, David Edward amesema kwamba mamlaka hiyo inaendelea na utekelezaji wa mipango ya kufikisha vyuo kila Wilaya, ambapo amesema kuwa hadi sasa vyuo takribani 80 katika maeneo mbalimbali nchini vinatoa huduma, lakini ameongeza kuwa vyuo vingine 65 vitajengwa kwenye Wilaya mbalimbali nchini.

David amesema kuwa lengo la kusogeza karibu vyuo hivyo kwa Wananchi ni mpango wa kutanua wigo wa huduma, ili wananchi waweze kupata ujuzi katika fani mbalimbali ambazo zinaweza kuwawezesha kujipatia kipato.

"Tunasogeza huduma hizi karibu na wananchi lengo ni kuongeza wigo ili wananchi waweze kupata ujuzi kwenye fani mbalimbali, lakini gharama zetu ni nafuu sana kwenye vyuo vyetu. Na niwakumbushe kuwa dirisha letu lipo wazi kwa sasa hivyo niwaombe Watu wachangamkie fursa" amesema David

Hata hivyo Mtaalamu huyo amesema kuwa Mamlaka hiyo inashirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika nyanja mbalimbali ikiwemo, kuandaa Walimu wa ufundi stadi, kuandaa mitaala ya mafunzo kwa Walimu wa ufundi na ufundi stadi pamoja na kuandaa maandiko ya miradi ya kutafuta wafadhili.
2601386e-e9f2-482d-9cc9-3687c5d37753.jpeg

Katika maadhimisho hayo Veta walikuwa na banda la maonesho wakionesha fundi stadi mbalimbali ambazo zinafanyika zinazoweza kuleta tija kwa jamii na Mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom