<br />
Haujasema je mlidate??au ilikuwaje?
mmhh tulienda out kwa dinner..
tukaongea kijana mtanashati sana..
yaani kila kitu ambacho ninachotaka anakijua
maneno yote matamu ninayotaka kusikia kayasema..
mmmhh nikajisemea nimepata mume hahahah lol
kumbe jamaa aliingia kwenye facebook kafanya utafit wa kutosha kuhusu mie..
halafu kaanza kuniingia kilaaini..
kwa sababu tulidhani hii itakuwa kitu cha kudumu kwa hiyo hakuja kwangu wala sikwenda kwakweke hiyo siku ya kwanza..
usiku huo mie mawazo kibao na furaha tele..
nika ingia facebook kumu add as a friend ili nisome kidogo kuhu yeye..
nikakutana na mtu ambae namjua ambae alikuwa mmoja wa rafiki zake..
nikaanza kumuuliza maswali kuhusu huyo jamaa..
duuuhhh majibu kidogo nihame dunia..
yaani namtunuku PHD ya UONGO...
siku ya pili kanipigia nikamweleza wazi wazi ..