Wewe nawe bana, mbona hizo tabia na sifa bainishi zipo kwa watu wote bila kujali wanatokea wapi? Hizo ni sifa bainishi (traits) za kibinadamu. Mimi nimebahatika kusoma na kuishi na watu wa kutoka kila pembe ya dunia kuanzia Nepal, Peru, Albania, Armenia, Uingereza, Mauritania na kwingineko na nilichoona na kujifunza ni kuwa sisi kama binadamu kitabia kwa ujumla hatuna tofauti sana. Na hapa nazungumzia tabia kama kusema uongo, ulafi, kupenda hela na vitu vya gharama kubwa, kupenda matanuzi, na mengineyo kama hayo.
Sasa hii ya kuja na kusema kwamba mademu wa Kitanzania wako hivi au wako vile wakati hizo tabia ziko hata kwa watu wa mataifa mengine si haki (not fair). Cha kuzingatia wewe tafuta wako anayekufaa na unaweza ukampata sehemu yoyote ile hapa duniani. Si lazima iwe Tanzania au Ufaransa. Mambo ya stereotypes achana nayo. Ku stereotype watu ni ujinga.