Wa-Kenya wamshukia reporter aliye-tweet uongo

Wa-Kenya wamshukia reporter aliye-tweet uongo

Uswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,204
Reaction score
627
Bwana Stuart Norval ambaye ni reporter wa france24 english version akitumia twitter handle yake ali-tweet ''BREAKING Gun shots fired in #Nairobi #Kenya as huge crowds fall over each other to vote. Dramatic pictures on @France24_en in 15 min''

Tweet hii ilimuingiza matatizoni kwani maelfu ya wakenya wali-tweet back na kumwambio huo ni 'urongo na uzushi' walimlaumu kwa kile wameitwa irresponsible journalism.

Iliwahi kutokea hivi kwa reporter wa CNN, kwa kutumia hashtag #SomeoneTellCNN maelfu ya wakenya walituma msg kukanusha uzushi uliokua umetumwa na reporter wao Nima Elbagir, CNN correspondent based in Nairobi covering the Middle East and Africa ambae alikuwa akitumia handle ya nimaCNN. Huyu reporter alilazimika kubadilisha handle yake ya twitter kutokana na thousands of tweets kutoka kwa wakenya waliokua wamechukizwa na 'ma-urongo' yake lakini kikubwa zaidi CNN walitoa official apology kwa Kenyans

Najaribu kufikiri kama tungekua tunafanya hivi, suppose tunakubaliana kum-tweet obama asikubali kumpokea vasco da gama ili hali nchini kwake mambo mengi ya msingi yanamuhitahi.......PAMOJA TWAWEZA!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni vyema ukatambua hatuna hata kigezo kimoja cha kujilinganisha na hawa wenzetu wa Kenya; kwani wao wanakimbia wabongo ndo tunavuta shuka kwa kusema jumuia ya Afrika Mashariki itatukomboa Watanzania, nahisi hizi ni ndoto za saa nane mchana.
 
Tupo tofauti sana na wakenya, wakati wao wanafuatilia affairs za serikali yao sisi tunajali matumbo yetu tu!
 
Wakenya linapokuja linalo husu kujenga Kenya wapo pamoja na wanapigana kufa na kupona, sisi ubinafsi, unafiki mwingi na kuchekana chekeana bila mpango.
 
kweli, Tuna la kujifunza hapa
 
Wakenya linapokuja linalo husu kujenga Kenya wapo pamoja na wanapigana kufa na kupona, sisi ubinafsi, unafiki mwingi na kuchekana chekeana bila mpango.
Jaribu kupitia post za wanazi wa CCM utajua kwa nini nchi hii imefika hapa ilipo.
Ujinga juu ya ujinga,na watu hao wanaona sawa tuu
 
CNN has apologised to kenya for false reports and reporter nimaCNN has changed her name to Nima heni
 
Last edited by a moderator:
Tupo tofauti sana na wakenya, wakati wao wanafuatilia affairs za serikali yao sisi tunajali matumbo yetu tu!

tunaganga njaa na siasa zetu za majungu na fitina.me huwa siwalaumu viongozi coz wao wanatambua sisi tunapenda nini(majungu na fitina) so wanatupatia na sie tunaserebuka.
 
nakwambia hili linchi letu sijui tumerogwa na nani?? yaani tupo busy na misukule ya lamadi na uchawi wa gambosh!! tufiakwa linchi hili!
 
wakenya si mchezo

Jamaa ni noma, baadaya bwana stuartf24 kushindwa kuweka hizo alizoitwa dramatic pictures, sasa hivi wameanza hashtag #PicturesForStuart hapo wanamuwekea picha ukitizama unacheka, mara jagoo wanapigana afu wanamkejeli eti labda hicho ndio alichoona, maana mtu kashika uma wa chakula wao wanadai bwana stuart kaona uma akadhani ni Panga. Zote hizi wanam-copy stuart na official twitter handle ya France24

Kenyans mock foreign media coverage on Twitter

wazungu walikuwa wanajiandaa kuandika mauaji Kenya wamezodoka
 
Back
Top Bottom