the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Wakuu salama,
Baada ya CHADEMA kupata mwenyekiti mpya watu wamekuwa na imani kuwa huenda chadema wataitoa madarakani CCM, lakini uhalisia ni kwamba kama wananchi hawatoungana kwa pamoja CCM haiwezi kubanduka pale ikulu.
Lissu mwenyewe amekiri licha ya kampeni ya 'No reforms no election' waliyoianzisha wao kama chama lakini bado wanahitaji nguvu kubwa ya wananchi ili hayo mabadiliko yatokee, amesisitiza kuwa iwapo wananchi hawatounga mkono harakati hizo basi hakuna namna tena na ataendelea kuwaacha waendelee kupitia wanachokipitia.
Siku wananchi wakiamua kwa pamoja hata vyombo vya dola vitasimama upande wao na hakika nguvu ya umma itakuwa imeshinda na kitakuwa kizazi cha dhahabu sana kilicholeta mabadiliko yaliyosubiriwa kwa muda mrefu. Hata malawi wananchi walipoamua kulinda kura zao na kupambana na chama kilichokuwa madarakani hata vyombo vya dola vilisimama na wananchi.
My take; Tusiichukulie kazi ya kuitoa CCM ni jambo la Chadema peke yao
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025