Wa Mikoani kuhusu bia kupungua bei Taifa Star ikishinda

Wa Mikoani kuhusu bia kupungua bei Taifa Star ikishinda

Habarini wadau Mkuu wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alitamka bei kupungua bei kuuzwa nusu ya bei ya awali. Ikumbukwe timu ya Taifa inaliwakilisha Taifa kwa ujumla na si Mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeonyeshwa kupendelewa kwa kupewa promotion ya kushekerekea ushindi. Nauona kama mwanzo wa kuanza kuitenga Dar es Salaam na Tanzania ni vyema timu ya taifa itakaposhinda ushindi uonekane ni Wawatanzania wote na si kwa Dar es Salaam pekee......

Tunaoimba serikali isitutenge sisi wa Mikoani na timu ya taifa kama ni ushindi tanzania nzima tunywe bia kwa nusu bei sababu ushindi ni wa Watanzania wote.

Shukrani.
Sasa ma RC wengi wamekosa ubunifu MAKONDA HUWA ANAJITAHIDI KUWA MBUNIFU JAPOKUWA HUMO HUMO HUWA ANAKURUPUSHA MAJANGA AMBAYO MENGINE HUWA YANAIKOST NCHI NA BABA YAKE MLEZI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka wazo langu halipo kwaajili ya kupinga wala kubeza alichosema mkuu wetu wa mkoa Mheshimiwa PAUL MAKONDA.


Je ni kwanini alichagua kushusha bei ya vinywaji? Kwa ninavyoona hapa atakuwa kuna watu hajawatendea haki! Kumbuka kunywa ni mapendeleo ya mtu, hivyo kuna watu wengi amewaacha!

Kuna vitu vya lazima ambavyo kila mtu lazima atumie kama vile Unga,sukari, mchele, mafuta ya kupikia, nk, Kwanini asingeshusha hivi vitu? Hakika ingekuwa hamasa kwa asilimia 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu ya Taifa official jezi yake (sio ile ya msalaba) ina label kwa mbele inasomeka: SERENGETI
 
Ameegemea kwenye vinywaji kwa sababu baada ya huo ushindi, mashabiki wengi watapenda kupoza makoo yao kutokana na shamrashamra za ushindi.
 
Ni kweli bhana.
Sisi wa mkoani tunywe chibuku wakati Bia zitakuwapo za bwerere iwapo kina samatta watashinda!
Sasa kwanini wa dar tu.?
Ina maana sisi ni wakimbizi??

"acha tulewe sisi "
 
Back
Top Bottom