Wa Tz Tutakufa Maskini Kwa Kimbilia Kuchimbia Pesa (Kujenga) Badala ya Kuizungusha Izae Zaidi

Je hio time vale na inflation ni reasonable enough kujustfy wewe kufanya sunk costs? Kuzungusha kunaweza kuwa na yield kubwa sana kujustfy inflation na TMV!!!!!!!!!!!

kujenga nyumba kwa ajili ya kujihifadhi(shelter) na kununua gari kwa ajili ya kukusaidia kufika kwa wakati katika shughuli zako za kila siku na kuokoa muda mwingi amabao utautumia kwa ajili ya kufanya shughuli za maana zitakazokuongezea kipato haya maamuzi na hela inayoumika sio sunk costs, sunk cost iko kwenye business na investment decisions mfano unaweza kuwa umetumia 500mn kujenga kiwanda, kabla kiwanda hakijaisha hiyo 500mn ni sunk costs kwa sababu haiwezi kuwa recovered, hivyo unaweza kuamua kumalizia kiwanda kifanye kazi 500mn irudi au unaweza kuishia njiani kwa kuona kuwa mradi hautalipa hivyo hiyo 500mn inakuwa sunk cost completetly, sunk cost haina uhusiano na maamuzi ya kujenga nyumba ya kuishi na gari la kutembelea kwani malengo yake si ya kibiashara.
 

Hapo unapokaa umejenga au umepanga? na kama umepanga je na yeye angekuwa ana mawazo kama yako ungekuwa umejichimbia wapi kama si Vikindu, mie nadhani kinachotakiwa kama unajenga usikomae sana mpaka senti yako ya mwisho kwenye ujenzi kiasi kwamba unashindwa kula yaani percent kidogo unapeleka kwenye ujenzi na nyingine unafanya other issues. Kuna maeneo kibao 13 years ago yalikuwa yanaonekana shamba lakini leo yamejaa hata kuwa na hiyo ardhi nayo ni strategy mojawapo ya kuhifadhi hela kuepuka bank charges kibao ambazo tunakatwa bank maana siku hizi hakuna hata siku moja ukakuta kuna interest zaidi ya kukuta avail balance na actual balance. Kiwanja kilichonunuliwa 1 million 2000 leo ni 10 million, maoni yangu ndio biashara ifanyike lakini nyumba bado si ya kujenga kwa kusema ipo siku utapata 60 million na kuanza kuporomosha kuanzia msingi mpaka kuezeka kwani kumbuka vifaa kila siku vinapanda.
 
fresh mkuu nimekidownload sema cjapata tym ya kukisoma maana cha hao rich dad poor dad..kidogo nidrop school..nackilizia mida mida nikisome nimalize..maaana daaahhhh
 

tehe tehe wape hao, kuendesha mavogue wanaona ushindi kumbe heheheheh! thanks my dear.
 
lara 1
kwakuwa bado haujaanza mchakato wa kuzibadili hizo 10m kuwa 300m naomba nisiwe na maswali mengi kwasasa lakini ukianza mchakato tafadhali uwe unatoa marejesho ili wewe uwe mfano halisi na wa kuigwa hapa jf
 

TELL me about it, hebu huyu muheshimiwa atufungue macho ni biashara gani bongo leo utazungusha ml30 au 40 ifike ml 400,
baba wachina wenyewe na ungangali wao wanauza mahindi ya kuchoma kariakoo, sasa hesabu za kupiga ukisha kula ile mabo yako{u know wht I mean} ukija kwenye real life unakuta haiwezekani,
mwenye kujenga au kununua nyumba au ardhi mara zote hajuti, hao wenye kufanya biashara za ajabu ajabu kwa tama ya kuzalisha haraka, ni vilio kila siku,
 
Huu ujumbe mzuri sana kwani unatuamsha watu kukumbuka pia upande wa pili.

Nafikiri Watanzania kwa ujumla, wengi wetu hatujajua kuwekeza pesa kwenye vitu vingine zaidi ya Nyumba.

Utasikia mtu anatamba kuwa ana nyumba 10 ila nduguze masikini wa kutupwa wakati angelifungua kakiwanda, basi angeliajiri nduguze wote haka kama ni udereva.

Ila pia hatuwezi wote kukimbilia kwanza biashara na si kujenga, kwani wengine hata kipaji na bahati hawana wakati ukishajenga, una uhakika wa pesa kuingia ingawa si kama kufanya biashara na ukawa na bahati yako.

Cha muhimu hapa ni kuwapa watu upande mwingine wa maisha. Mtu mwanzo unaweza kuwa hata wazo huna ila kama umepewa mawazo kama haya na kama tungelikuwa tunafundishwa tangi Mashuleni, Makanisani, Misikitini nk kama wanavyofanya wenzetu Wahindi kule Jamatini au Wayahudi kwenye Masinagogi yao, basi tungelikuwa tangu utotoni tuna Option nyingi katika maisha na si kufikiria tu shule, kazi, nyumba, gari, mke, watoto, wajukuu...... KIFO.
 
Mimi niliwekeza kwenye biashara ya maduka makubwa mawili hapo mwananyamala kwa kopa na mombasa ukonga, na mengine klm moro na Arusha, yakawa yanalipa sana nikatajirika sikuwa na fikra za kujenga wala kununua gari, nia yangu ilikuwa nidunduize hadi niwe bilionea, maduka yangu ya kaanza kukumbwa na mikosi mara wezi mara moto mara hasara mara matapeli, nikajikuta nimefilisika sina hata peni, nikahamua kuachana na biashara zamaduka nikaanzisha nyingine tofauti na ile, tatizo likawa ni mtaji mdogo, nikajaribu kwenda bank wakaniambia wanataka hati ya nyumba, nikawa sina hivyo wakaninyima mkopo japo nilikuwa na uwezo wa kuulipa wote hata kama nisingekuwa na biashara coz nilikuwa na miradi mingine yenye uwezo wa kuzalisha kila mwezi kuweza kulipa mikopo, lakini bank hawakukubali kunipa mkopo hadi waone hati ya nyumba, ndipo nilipo hamua kujipanga nikajenga nyumba yenye thamani ya 32ml nikajipanga tena kidogo dogo nikajenga nyingine ya 60ml na sasa na malizia ya 75ml, bank wameweza kunikopesha 150ml na nimesha lipa na karibia kumalizia maregesho nikope nyingine 200ml, ndo maana nasema kujenga ni muhimu inakupa kuaminika hata kwa wateja wako, pia inakuwezesha kuona mbali zaidi ya hapo unapo waza wewe, pesa haziwekeki na hata kama ukizikusanya zitakupa anasa zisizo na maana lakini ukijenga nyumba ukaimalizia vizuri labda umejenga kwa garama ya 40ml mwaka huu mwaka ujao utaiuza kwa faida ya 100ml bila tatizo. Mimi ni mangi bana na mangi bila kuwa na nyumba mjini na kijijini sio mangi.
 
Mifumo ya 20th century ndio inanganganiwa na wabongo. Kwa nini BENKI HAZIONGELEWI? HILI SUALA LINGEKUWA NA UNAFUU SANA ENDAPO BENKI ZINGEKUWA ZINASAIDIA WANANCHI KUNUNUA AU KUJENGA KAMA ILIVYO KATIKA NCHI ZILIZOENDELEA. LAKINI KWA HALI ILIVYO SASA HIVI, KILA KITU NI KUBAHATISHA. ANGALAU NYUMBA INAKUSITIRI NA UNAWEZA KUPATA JAPO PESA YA KULISHA WATOTO.
 

Nakuunga mkono asilimia 100! Tatizo watanzania wengi wetu ni waoga na tunaishi kwa mazoea na si kutafakari mambo! Nimeshuhudia wengi wanaojifanya kukimbilia kujenga wanateseka tu na maisha..Mimi nadhani katika maisha jambo la muhimu ni kujihakikishia kipato cha kila siku kipo hata kama hujajenga...sasa wengi wetu tujishajenga huwa tunadhani tumemaliza! Na matokeo yake tunaishia kufa maskini.
 

Kwanini ujilimit kuwa wewe mwisho wako ni kulisha watoto? Aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea. Why dont you dream big? As lazima wanao wasome US au hata IST ukishindwa kabisa kabisaaa!

Yaani wabongo people are even afraid of dreaming big! YOUR ATTITUDE DETERMINES YOUR ALTITUDE!
 

Wewe unachanganya mambo! Case yako ni BAD INVESTMENT MANAGEMENT! Ulishindwa kumanage rasili mali zako ndo maana ukawa bankrupt. Hata nyumba ukianza kujenga ukishindwa kujipanga utaishia kuwa gofu tu.

Mfano owner wa Pepsi Tz anaishi Masaki nyumba ya 6000$ (Dalali ndo kaniibia huu umbea) miaka kibao wala hana nia ya kujenga/ kununua residential house mitaa ile. Japo ana MAJUMBA mengi ya kibiashara na Godowns kibao. Issue ni kuwa kwake kaona residential house anayataka yeye ni mzigo, na hizo 6000 dolari kwake sio issue ukilinganisha na priority zake.
 

Mi nakaa kwenye free house,, mzee wangu alikuwa na mawazo kama hayo tunayoyapinga akajenga nyumba kibao mjini na kabla hajarudisha hela zake Mungu akamchukua.. Tunaofaidi ndio sisi kizazi chake...
 
Acha uchochezi ..... hupendi kucha zako tena!!!

Achana nae huyo! Wote tukiwa matajiri nani atakuwa shamba boi wetu? Maisha ndo yalivo lazima kuwe na wafalme na watumwa! Unchagua tu mwenyewe mimi bana utumwa utanifaa kama huyo mdau, au mimi bila ufalume dunia itakuwa haitoshi hii wala haikaliki.
 

Vitu viwili unasahau sana lara 1 ......... chukua kitabu chako cha investment soma topic inayozungumzia "purchasing power" hakikisha unaelewa vyema, rudia tena na tena; baada ya kumaliza kusoma hiyo tafuta kitabu kingine kinachofundisha kitu kinaitwa BOP yaani "Balance of Payment" hakikisha unaelewa vema, rudia tena na tena.

Ukishamaliza kusoma na kujiridhisha kuwa umeelewa intensively ...... rudi sasa uandike post yako upya!!!!!

Km utahitaji hints zaidi nicheki PM!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…