MrfursaTZA
Member
- Jul 26, 2024
- 29
- 94
Waafrika wa leo wamekuwa dhaifu kiasi cha kushukuru na kuthamini viumbe wa mawinguni, ambao hawajawahi hata kuwaona, bali wamesikia tu kupitia watu wengine. Wengi wa watu hao ni wakoloni, wazungu na waarabu, ambao walileta imani hizi.
Kondoo wa dini wanapata shida kubwa wanapoulizwa maswali yanayohusu imani zao. Jaribu tu kumuuliza kondoo mmoja, "Ukiwa mbinguni, utaenda kukaa wapi?" Atajibu, "Kwa Mungu." Ukiuliza, "Je, mbingu anayokaa Mungu iliumbwa na nani?" Ataanza kuishiwa na majibu. Na ukimuuliza, "Wakati Mungu anaumba mbingu hiyo, alikuwa akiishi wapi?" Atashindwa kabisa na atakuita kafiri. Katika hali ya kuchanganyikiwa, anaweza kusema, "Umekufuru!"
Maswali kama haya huwafanya kondoo wa dini kushindwa kabisa kujibu. Ukimuuliza, "Je, una kiwanja huko mbinguni au utaishi kwa kupanga?" Hajui. "Je, unamfahamu ndugu yako yeyote anayeishi huko, kama vile mama yako au bibi yako?" Hajui. Yote anayojua ni kuwachukia mizimu na kuwadharau mababu zake, akidhani ni wabaya kwake.
Endelea kumuuliza, "Mnasema zipo mbingu saba au zaidi, je, wewe utakaa mbingu ipi?" Kondoo hawezi kujibu, na hapo ndipo anapokimbia kwa sababu ya aibu.
Achana na Kondoo wa Dini
1. Ukikosana na mtu au kiumbe, omba msamaha kwa yule uliyemkosea. Usidanganyike kuomba msamaha mawinguni, kwani kama yule uliyemkosea hajasamehe, basi hakuna msamaha wowote kutoka popote pale, na dhambi hiyo itakutesa sana.
2. Kama una shida, kama vile njaa au ugonjwa, usitegemee msaada wa watu wa mawinguni. Tumainia watu wa hapa duniani.
3. Ukipikiwa chakula, au unapewa maji ya kunywa, au unasaidiwa kwa namna yoyote ile, mshukuru yule aliyekusaidia. Si viumbe wa mawinguni bali ni watu wa hapa duniani.
Naamini mmeshajifunza kuwa kuna watu hapa duniani wanaothamini sana viumbe wa mawinguni. Wakipata shida, wanatukumbuka sisi tulio hai, lakini shida ikiisha, wanasema wamesaidiwa na viumbe wa mawinguni kama Yesu, Muhammad, au Allah. Ni vyema tukathamini zaidi wenzetu wa hapa duniani.