GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kama ulifanikiwa kusoma hadi Sekondari, na ulikuwa na Mwalimu mzuri wa Historia kama Mwalimu wetu, unaweza ukawa unaikumbuka hii kauli:" We produce what we do not consume and consume what we do not produce". Kwa tafsiri isiyo rasmi inaamisha hivi:"Tunazalisha tusichokitumia na kutumia tusichokizalisha".
Hiyo tulikutana nayo Form Two, kama sikosei. Ni mojawapo ya sababu iliyopelekea kuibuka kwa vuguvugu la kudai uhuru. Waafrika walichoka kuzalisha wasichokitumia, na kutumia wasichokizalisha.
Madhalani, kwa Tanzania, watu walilazimishwa kuotesha mazao ya biashara ambayo hatimaye yalisafirishwa kwenda viwandani Ulaya, na Waafrika wakaletewa bidhaa kama nguo n.k., toka viwanda vya Ulaya.
Kwa hiyo, Afrika ikawa mahali pa kuzalishia "raw materials" na pia kama soko la bidhaa za viwanda vya Ulaya.
Ikiwa ni miaka mingi tangu nchi za Kiafrika zijinasue kutoka katika makucha ya utawala wa Wakoloni, kuna utofauti wowote?
Je! Inazalisha inachozalisha kwa ajili yake au bado ni kwa ajili ya watu wa ng'ambo? Bado ni chanzo cha raw materials na soko la bidhaa za nchi za mabara mengine?
Ni nani anayeconsume "madhahabu" yetu?
Nani anayeyatumia "maalmasi" zetu?
Nani anayeyafaidi "Matanzanite" yetu?
Mbona bado zinaenda kwa watu weupe? Sisi hatujui kuyatumia? Hatuyapendi? Tunayaogopa? Hatuyajui matumizi yake?
Ukiacha mazao ya chakula, ni kipi tunachokizalisha kwa ajili yetu wenyewe? Magari, simu, silaha, madawa, makompyuta, zana za kilimo, n.k., kwa asilimia nyingi zinatoka hukoo!
Pamoja na kuwa nchi zetu ni huru, mbona kama bado tunaconsume what we do not produce na kuproduce what we do not consume?