Waafrika tujitambue kwenye hizi dini Uislam na Ukristo

Imole

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2021
Posts
1,438
Reaction score
4,053
Waafrika dini zetu kuu ni 2, Uislam na Ukristo. Japo dini mbili hizi zinatofautiana ila misingi yake mikuu ni kuleta amani na upendo baina ya watu na si vingine. So kimsingi mifumo yetu ya kiibada ni tofauti ila sababu ya ibada zetu ni kumjua Mungu na kuhubiri amani na upendo baina yetu sisi (usizini, usiibe, usidhulumu, usiue, n.k).

Tuje upande wa pili kutokana na dini hizi kuna watu wanayatumia maandiko kwa maslahi yao ila mitaji mikubwa walio nao ni hawa supporters wao wafuasi wa dini hasa sisi waafrika huku. dini ya Uislamu si dini ya waarabu na dini ya Ukristo si dini ya wazungu hao wayahudi ndo kabisaaa wenyewe wanawakataa wote.

Leo hii muarabu anaua/dhulumu mtu mwengine muislamu anasupport au mzungu/myahudi anaua watu huko mkristo anakuja anasuppott while yeye anafanya kwa maslahi yake, huu ni upumbavu wa viwango vya juu.

Mimi ni muislamu ila simsupport wala kumshobokea muarabu yeyote kama anajiona bora kwa upande wake na mimi najiona bora kwa upande wangu full stop. Muarabu au muislamu yeyote akifanya jambo linalokiuka haki za mtu mwengine sitaweza kumsupport mfano wa alshabab na boko haram wote wale wanayofanya kwa kisingizio cha mafundisho ya uislamu si kweli hakuna mafundisho ya vile.

Tuje kwa ndugu zetu wayahudi hawa ndo wamepata wafuasi wengi kutoka kwa wenzetu wakristo, wenzao wanayatumia maandiko kwa maslahi yao na tulivyo wajinga sisi na watumishi wetu tunawasupport, narudia hakuna dini inayofundisha machafuko na vita ukiona mtu anafanya hayo ameamua yeye kuyafanya na hastahili kusapotiwa, anayofanya israel kwa Palestine ni mambo ya kishetani na ndo ugaidi wenyewe wala si taifa la mungu linaloweza kufanya vile.
 
Ukiwaambia mtangulizeni Mungu kwanza kabla ya dini zenu wanakuona kama ibilisi vile.

Dini ni dini na Mungu ni Mungu. Wengi wamechagua kuziabudu dini. Ndio maana utawasikia dini inasema na sio Mungu anasema.
 
Kwahio unamtunguliza mungu yupi..? Huyo mungu umemjua kupitia dini/imani ipi..?
 
Dini zenu halisi nyie Waafrika mlishaziacha kitambo sana.
Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye matambiko kwa mizimu ya ukoo ili isaidie jamaa zao.

Siku hizi idadi ya wafuasi wa dini hizo inazidi kupungua na kuziachia nafasi dini za kimataifa, hasa Ukristo na Uislamu.

Hata hivyo mabaki ya imani ya asili yanawaandama waliojiunga na dini hizo, hasa kwa namna inayotazamwa nazo kuwa ushirikina.

Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani.
 
Usidinye, usilanduke
 
Ukiwaambia mtangulizeni Mungu kwanza kabla ya dini zenu wanakuona kama ibilisi vile.

Dini ni dini na Mungu ni Mungu. Wengi wamechagua kuziabudu dini. Ndio maana utawasikia dini inasema na sio Mungu anasema.
Mizimu? Idumu Mizimu?
 
Dini ya muafrika ni ushirikina ambayo ni kuabudu ktk milima miti misitu maziwa nyoka na viumbe hai vingine... Sadaka zake ni kafara ya mnyama pombe au binadamu...
Kimsingi ushirikina hii ndio dini ya kila binadamu (awe kutoka Africa Asia au America) kabla hajastarabika...
Baada ya binadamu kuanza kutumia akili na kupata maendeleo ya sayansi na teknolojia ndipo kila jamii ikaanza kustarabisha dini/imani yake ili ionekane nzuri kuliko za wengine...
Wazungu kwasababu ndio waliotangulia kustarabika duniani basi dini yao ya Kikristo ikapata kuwa na nguvu duniani kote wakaisambaza ikapata mashiko... Ndipo baadae waarabu nao baada ya kupata maendeleo wakastarabisha imani yao na kuanza kuisambaza Africa...
 
We kweli mweupe! Hizo dini unazosema sio dini za waafrika,hizo dini zilikuja na meli na mashua! Hata hao mnaowataja mnaposwali/sali hawakuwa waafrika! Jitambue wewe
Haijalishi imekuja na nini ila ndo dini zetu kwa sasa tulishaachana na hiyo mizimu
 
Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye matambiko kwa mizimu ya ukoo ili isaidie jamaa zao.

Siku hizi idadi ya wafuasi wa dini hizo inazidi kupungua na kuziachia nafasi dini za kimataifa, hasa Ukristo na Uislamu.

Hata hivyo mabaki ya imani ya asili yanawaandama waliojiunga na dini hizo, hasa kwa namna inayotazamwa nazo kuwa ushirikina.

Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani.
Sahihi mkuu watu wanazungumzia dini za mababu ila hawajui kuwa walichokuwa wakikifanya hao mababu ni uchawi
 
Back
Top Bottom