Ukristo unamtaja mungu kama roho,na kwa kuwa ni roho macho ya nyama hayawezi kumuona.Mungu huyu hujidhihirisha kwa wanadamu kwa namna mbili:ANTHROMORPHIC-Mungu anavaa mwili wa binadamu(incarnate) na kuishi nao mpaka muda wake utakapotimia anaondoka.THERIOMORPHIC-Mungu anajidhihirisha kwa vitu vingine.Kwa kuwa mungu huhitaji patulivu kujidhihirisha:chini ya mti,pembeni ya jiwe,pembeni ya mto,chini ya mlima au pango yote haya ni maeneo tulivu(sanctuary) kwa iba(tambiko).Kujenga makanisa,misikiti,masinagogi ni matokeo ya binadamu kubanana na kuathiri mazingira asili.Unayemtuhumu mwafrika kuabudu chini ya mti,mlima,jiwe nk.wajua unachokiongea kweli?