Waafrika tukiambiwa tumelaanika tokea dunia iundwe huwa tunakataa, kununa na kukasirika

Waafrika tukiambiwa tumelaanika tokea dunia iundwe huwa tunakataa, kununa na kukasirika

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wakala wa Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu ametoa ' Kauli ' ambayo kiukweli imethibitisha kuwa ' Waafrika ' tumeshalaanika tokea dunia inaundwa na kamwe pale tukiwa tunapewa huu ukweli tusiwe tunakataa, tunanuna na kukasirika ( Na kumbukeni hata Mimi GENTAMYCINE ni Muafrika vile vile )

Wakala wake huyo amesema hii kauli ambayo nataka Sisi ' Waafrika ' wengi tuijadili na tuipime kwa kufikiri nje ya ' Boksi ' ili tuweze kujua kama hii ' laana ' kweli inatustahili au inastahili iwe kwa baadhi yetu.

" Kwa kipndi kirefu sana Thomas Ulimwengu alikuwa na tatizo la Goti lake ila tuliona tusimpeleke kwanza Hospitalini na badala yake tumpeleke katika maombi kanisa Makanisa mbalimbali ila tulipoona hali yake bado inazidi kuwa mbaya tukaona sasa haina jinsi tukimbilie tu Hospitalini kama ambayo tumefanya sasa ".

Namalizia kwa kuwaachieni tu Swali kwamba hivi Wachezaji akina Messi, Ronaldo, Suarez na wengineo wa huko Ulaya na hata Mbwana Samatta wetu akiumia huwa wanapelekwa Kwanza katika ' Makanisa ' au ' Misikiti ' Kuombewa au huwa wanapelekwa kwa ' Wataalam ' wa Tiba ili waweze kutibiwa ' Kisayansi ' zaidi?

Sijui kwanini nimeumbwa ' Muafrika ' kudadadeki! Huyu Wakala wa Mchezaji Thomas Ulimwengu ameshaniharibia siku yangu nzima ya leo baada ya kuusikia huu ' Upuuzi / Upupu ' wake

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom