Waafrika tumefikia kwenye hatua mbaya sana. Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu, wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa

Mkuu hapo sipingani na wewe lkn tambua kuna baadhi ya makanisa hayo ya kinabii watu wanashinda makanisani tangu asubuhi mpaka jioni 24/7
Katika hali ya kawaida, mtu anayeshinda kanisani kila siku basi hakuna anachochangia kwa kanisa hilo, na kama anachangia basi ana vyanzo kadhaa vingine vimuwezeshayo kupata cha kuchangia kwa kanisa!
Ninachojua, kama kuna wanufaikao ktk kanisa, wao kuhudhuria kanisani kwa huduma, na huhudumia watu tofauti tofauti wasio waumini wa kila siku kwa kanisa hilo!
Kwa wahudumu kuwa kanisani kila siku ni sawa kwa kuwa hiyo kazi kwao ndiyo chanzo chao cha mapato!
I tell you the truth, its not easy for everyone to be busy every day being in the church for nothing, never!
 
Mkuu jongea kanisan.usiache kwenda kwasababu ya hayo.Wakileta habar za michango wewe unpiga kimya.Ukiona una nafas ya kutoa unatoa vinginevyo unafanya ibada kwa Mungu wako unarud nyumban.Simple like that
Je ni lazima kufanya ibada kwa Mungu wa wazungu na waarabu? Ina maana sisi waafrika hatuna Mungu wetu?
 
Sijui lini sisi waafrika tutaamka kutoka katika hili. Maana usingizi huu ni mzito na tumefunikwa blanketi zito na nje kuna baridi kali …..hizi imani hazina hata miaka 500 Afrika….je mababu zetu ilikwaje? Waliiishije? Na Leo hata majina yetu ya asili yamepotea…..na denn waliotutesaaa, kutuuua, kutuuzaaa kama mbwa…kutufunga minyororo Leo eti tunawaabudu…..na kwenda kuhiji kwao badala ya kwa mababu zetu….
 
Kumbuka, kila jambo lina wakati wake, kupingana na jambo ktk wakati wake hutofanikiwa, wakati wake ukipita mambo yanabadilika!
 
Aliyesema dini ni kasumba sawa na bangi hakukosea. Si Ukristo, Ubudha wala Uislam, wote ni utumwa wa kujitakia ambapo mabwana wanaofuga watumwa hutokea kuwa matajiri wakati watumwa wakiendelea kuwaramba matako.
Upuuzi huo sisi Waislam hatunaga.
Kwanza kwenye Uislam ukiongeza kitu ambacho hakipo kwenye Quraan ama Hadithi ya mtume ujue kichapo kinakuhusu.

Tatizo wakristo wengi hamuijui Bible kwa kuisoma, bali munaishia kuzibeba tu mikononi.

Tofauti na sisi Waislam, wengi tunakijua kitabu chetu kwa kukisoma.

Yani ukiingia msikitini ni wachache wasie ijua kilicho andikwa kwenye Quraan, yani mpaka mtoto wa miaka kumi na mbili anajua kuisoma na kuielewa Quraan.

Nyinyi kanisani anae ijua Bíblia ni mchungaji tu, wafuasi kalibu wote hawaji.

Kiufupi kanisani asipokua mchungaji basi ibada hakuna siku hiyo, wakati msikitini hata sheykh asipokuepo hata mimi naswalisha.
 
Kiongozi nakupa taarifa sahihi ninyi mnaojiita manabii,mitume sijui makuhani wa zama hizi sehemu yenu ni bottom less pit or hell you always deceive worshipers kupitia miujiza ya kipepo huwezi kuthibitisha humu kuwa attending to church without struggling to find your own bread utapata chochote kutoka kanjsani you are a living lier
 
Wengi ya walokole sisi..tumeweka kila kitu ktk imani..akili tumemwachia shetani..mtu hasomi anategemea kufaulu kwa maombi au mafuta ya upako...naona kabisa kana mwokozi hatotokea huku kwa walokole..basi siku zijazo watoto wetu watasusia imani kabisaaa...maana wanavyoona wazazi wanafanya ujinga kwa kigezo cha imani..wataaachaaa....
 
Ukweli ni kwamba hakuna dhehebu sahihi hapa duniani..na tukumbuke kuwa ktk biblia hakuna eneo Yesu alisema hawa wako sahihi..wale sio sahihi...alisema atakae mwamini hatohukumiwa..na asiyemwamini atahukumiwa. Binafsi baada ya kutambua hili..limenisaidia kuheshimu na kupenda kila mtu anajiita mkristo..kamwe sijioni wa thamani zaidi ya mwingine..na kwangu kanisa bora..ni lile litakaloniwezesha kumjua na kumtii Yesu ktk roho na kweli period...nikikuta mlutheli anafundisha vema au sawa na biblia..nasali..mkatoliki..twende kazi.
 
Hakika wewe ni mcha Mungu wakweli ubarikiwe mnoo kiongozi wangu hii post yako imenibariki sana sana
 
Yaani tumetekwa na dini mpaka misionaries waliotuletea ili watutawale wanatushangaa [emoji849][emoji849][emoji849] yaani mtu haambiliki chochote kuhusu anachosema mchungaji huku akimwambia mavuno yake yote amtolee bwana(pastor) huku akioteshwa ndoto za watu wanaofanya kazi kwa bidii sana mchungaji anajisifia alikuwa analala njaa na mkewe lakini sasa anamiliki V8 na nyumba ya ghorofa na muumini anashangilia huku anaenda kula kiporo kilichobaki jana.
 
Mm najiuliza tu.wale babu zetu ambao waliishi kabla ya kuja hiz dini nao hukumu yao siku ya ufufuo itakuwaje

Maana waliamin miungu yao na walifanikiwa vizuri tu

Walioleta din huko kwao mauaji ushoga na wengne hawaend kanisani kabisa nao tunawaweka kundi gani?

Wachina hawaamin katika dini na ndio taifa linalokuja kasi Sana kwa maendeleo

Mm binafsi namashaka Sana na hizi dini za kuletewa na waarabu na wazungu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hi
 
Ebwana wiki kama moja iliyopita nilikaa tu kitaa, mara nikaona vitu vya ajabu, waya aina za kopa zikawa zinajikusanya zikajifinyanga finyanga, ikatengenezeka coil, mara madini ya chuma yakajitengeza mapangaboi, ikatengezeka stendi na vitu vingine pia. Nikwambiavyo sahivi nina feni nzuri imo ndani iliyojitengeneza wenyewe.
Unaaamini?

Note: Mleta mada yupo sahihi sana sana sana, ila haiusiani na kukanusha uwepo wa Mungu
 
Ebwana wiki kama moja iliyopita nilikaa tu kitaa, mara nikaona vitu vya ajabu, waya aina za kopa zikawa zinajikusanya zikajifinyanga finyanga, ikatengenezeka coil, mara madini ya chuma yakajitengeza mapangaboi, ikatengezeka stendi na vitu vingine pia. Nikwambiavyo sahivi nina feni nzuri imo ndani iliyojitengeneza wenyewe.
Unaaamini?

Note: Mleta mada yupo sahihi sana sana sana, ila haiusiani na kukanusha uwepo wa Mungu
 
Nyani haoni kundule. Nyie tena ndo msiseme. Wakati wakristo wamegeuka watumwa wa kutegemea miujiza na wokovu, waislam mnategemea ugaidi. Mko tayari kuua kwa ajili ya Allah na Mtume lakini si kwa ajili ya wazazi wenu. Utasikia mtu mzima akisema "ukimtukana Mtume kichwa chako halali yangu." Ukitaka kujua ni mtumwa mtukane baba au mama yake, anakwenda polisi. Waafrika wote ni watumwa ukiondoa wale ambao hawaamini kwenye utumwa huu ambao nyinyi huwaita makafiri na wakristo huwaita wapagani. Angalia majina yenu na mafungamano yenu. Mnabaguliwa na wazungu na waarabu lakini hamjitambui. Miungu yenu ni ima ya kiarabu au kizungu. Manasujudu kila siku kuelekea kwa mabwana zenu. Mnajiita waislam au wakristo kwanza lakini si waswahili. Mnatuchelewesha kweli kweli. Hata kushiriki mabishano haya ni kwa vile sina jinsi. mnaboa kweli kweli wanangu. Mnafundishwa hata kutawaza na namna ya kuanza kula utadhani hamkuwa mkiyafanya haya kabla ya kuingizwa utumwani. Kila kitu chenu ni kitamu na halali isipokuwa kujitambua ndo haramu.
 
AKILI KICHWANI, PESA MFUKONI, YESU MOYONI.
 
Tunajificha kwenye kichaka cha maombi na maombezi dhidi ya nguvu za giza.kwamba kila tatizo linalotusibu basi shetani .ofcz shetan mtaabishaji yupo ila walokole wengi sis ni wavivu sanaaa na tunaishi kwa mazoea sana kupitiliza
 
Je ni lazima kufanya ibada kwa Mungu wa wazungu na waarabu? Ina maana sisi waafrika hatuna Mungu wetu?
Kwakua sie tumzaliwa n kukuzwa kwenye iman hii hatuna namna.Kama kuna wenye iman zingine (i hope wapo) na wanaona zinawanufaisha basi nao ruksa kuendelea na ibada zao as long as hazi wa cost.maana hata kama ukristo au uislam unakuongezea gharama badala ya kukupa manufaa (sio ya kifedha tuu) nasi hazina maana.
Maana kama mwanadamu/mshkaji wako wa karibu anaweza akakusaidia au akaguswa na kuumia kwa matatizo ulio nayo basi Mungu anapaswa kufanya zaid ya hapo..Kama huoni hilo bas imani haina faida.imani hiz za kukamuana pesaaa mwanzo mwisho za kazi gani sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…