Waafrika tumefikia kwenye hatua mbaya sana. Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu, wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa

Naona umeandika kinyume chake. Nikukuletea hiyo Quran iliyoandikwa kiarabu utaisoma?
Nimeishi na waislamu wengi hawaijui Quran. Wamekariri aya za kuswali tu lkn sasa mpe hiyo Quran mnavyotafutana.
 
Sijajua huelewi namna gani, labda niseme tena hivi, hakuna mtu aendeleae kufanya biashara imtiayo hasara! Kushamili kwa makanisa mengi na yanapata waumini, tambua lipo linalowafanya waumini kuhudhuria ibada zao, si bure tu!
Tatizo wengine mkikosa matamanio yenu mnadhani watu hawanufaiki ktk makanisa hayo!
Labda hujui, watu tunatofautiana namna ya kutambua thamani ya kitu, wewe waweza sema kitu hiki hakina thamani wakati wapo watu wengine wanaona thamani ndani yake!
Jambo jingine ni kuwa, raha na amani ya maisha ya mtu ipo katika nafsi yake, yaani kama mtu ana amani na raha ya dhati kuwa muumini wa dini flani, huwezi kumshawishi kuondoka huko kisa wewe huoni thamani ya akitendacho!
Jambo jingine unalopaswa kulijua, kila binadamu katika hali yoyote anayopitia anafanya hivyo kwa mpango wa Mungu, watu wote huwa tunajifunza kutoka wa wengine!
Ni nature, kila jambo lina wakati wake na katika wakati huo watu hujifunza mambo mbalimbali ya kuwaongoza kutenda uonavyo!
Binafsi sina tatizo na wewe, huenda kupinga kwako, kutoamini kwako kunakusaidia kuishi kwa amani, hayo ndo maisha!
 
Mkuu kupitia huu ujumbe nimepigia mstari wewe ni mmoja wa hao manabii fake mnaowaibia wajinga wasiopenda kunishughulisha kusoma maandika matakatifu yaani wale wanaopenda kulishwa na wachungaji uchwara kama wewe,eti hakuna mtu anapenda kuendelea na biashara imtiayo hasara unasahau mara hii kuwa ningi false prophets mnatumia magic power kuwafanya muendelee ku exist? Nalijua mno neno la Mungu aliyehai ktk hili namshukuru sana aliyehai mimi sibabaishwi kabisa na ninyi manabii uchwara although mke wangu anayumbishwa sana mpaka last week nikaingilia kati kumpiga marufuku na ninyi wajaa laana ma agent wa ant christ
 
Hisia zako zitakutesa, huenda ndo chaguo lako, umejifungamanisha na chuki, na kwa kujifunga kwako hivi kuna watu wanajifunza na wanapata nafuu ya maisha yao!
Naamini ktk kutenda wema na haki kwa kuwa kufanya hivyo ni kujitendea Mimi mwenyewe!
Kuwachukia watu na kuwatukana, ni jambo ambalo mtu anajitendea mwenyewe pia!
Fuatilia vizuri comments zangu, utagundua sipigii chapuo dini flani lakini naheshimu kile mtu anakithamini kwa namna yake!
 
Mimi situkani bali naongea fact kuweka mambo sawa niliokoka 1991 nikikumbuka wokovu na injili ya miaka hiyo ni tofauti kabisa na ninyi wajaa laana wa nyakati hizi,siku hizi huwezi kwenda kanisani kwa hao manabii fake ukapata GOMBO LA CHUO yaani INJILI ISIYOGHOSHIWA zaidi ya mahubiri ya mafanikio,watu hawafundishwi jinsi ya kuishi KITAUWA kumcha Mungu sababu manabii uchwara wanajua kumuambia mtu aache ulevi,uzinzi,uchawi,ibada ya sanamu nk kutamfanya huyo muumini asije tena kanisani kwake thats why ukienda kwa mwamposa utakuta Islamic worshippers wanahudhuria ibada as usual then baada ya kununua mafuta wanarudi makwao na dhambi zao na uislamu wao pasipo kutubu
 
Basi unachanganya mafaili Mzee, kwani unaelewa nini juu ya matabirio ya siku zinazoitwa za mwisho! Hutaki yatimie au hutaki kuamini unapoyashuhudia?
Ndio maana nimekwambia, mambo yanakwenda kwa nyakati zake, huu ni wakati wa kushuhudia unayoyaona na usipoelewa kuwa huu ni wakati wa haya unayoyaona basi utapata tabu sana!
Relax, be free! Mimi naelewa kinachoendelea na sipati tabu ninapoyaona yanayoendelewa! Kwa taarifa yako, mimi si muumini wa dhehebu lolote kwa muda takribani miaka 15, mara ya mwisho kuhudhuria kanisani ilikuwa kabla ya kumaliza chuo, na lilitokea jambo ambalo nililiona kama igizo mbele za Mungu kwenye maisha halisi!
Pamoja na hayo, ninayo elimu juu ya maisha katika ulimwengu wa mwili na nyama na yale yaliyo katika ulimwengu wa roho!
Elimu juu ya ulimwengu wa roho haimanishi kuwa mfuasi wa dini za kuzungu wala kiarabu, hata mababu zetu walitumia njia zao kadhaa kufanikisha masuala yao kwa kutumia elimu ya masuala ya ulimwengu wa roho!
Ukisikia mtu akitajwa mganga wa kienyeji, mchawi, malaika, jini, nk hawa wote hudhughulika ktk ulimwengu wa roho na uyaonayo wewe ni matokeo ya mipango ktk ulimwengu wa roho!
Natamani kukueleza ana kwa ana, huenda ktk uandishi huu nakosa namna ya kukufanya uelewe!
One thing to note, every action you do, comes from the spiritual plans!
 
Hayo mambo yako hivyo duniani kote hasa Marekani na Latin America.
 
Kuna kiwango dini ikifikia inakuwa kama uraibu.
Binafsi uwa nashangaa sana lakini nabaki kusikitika tu maana watu wenye imani na hao manabii na mitume fake kuwatoa huko ni ngumu sana.
 
Nimekuelewa mkuu ZNM
 
Reactions: ZNM

Wakristo wengi wanasali wenyewe bila kuongozwa na mchungaji, kwahiyo hamna tofauti na waislamu.
Lakini tujiulize ilikuaje tukakubali hizi dini za kigeni mpaka leo wakati tunaona wazi sio za kwetu, bali za waarabu na wayahudi?
Sisi tulikuwepo na imani zetu miaka mingi tu, kabla hata ya Musa.
 
Naona "case study" umejileta
 
“Dady I receive”😅😅
A good thing dini imebaki afrika, gulf countries na Latin America
Kwa sasa naona kinachosumbua ni social inclusion kwenye maisha binafsi ya mtu, kwamba kuweka mwanamke ndani lazima ndoa, hata kama ni mchawi wewe asubuhi nenda ibadani usiku ruka angani, zingatia zaka na sadaka hata kama unazini haitazingatiwa sana
 
UKWELI MCHUNGU, NGUMU KUMEZA
 
 
Hi,
Makala hii ni nzuri sana na inamengi sana ya kujifunza kutoka kwa mwandishi, lakini kinachonishangaza zaidi ni pale ninapoona mwandishi anaingia kwa kuwa-attack kabisa watumishi wa Mungu as if wote ni WAJANJA WA MJINI (Jambo ambalo ni uongo ulio wazi)

Tukumbuke kwenye maisha hakuna kazi isiyo na watu feki, ukienda kwenye siasa wapo waswahili-swahili, ukienda kwenye biashara wapo wapigaji, ukienda kwenye udactari wapo madactari feki nk, hii ina-maana hata katika taaluma hii ya kumtumikia Mungu hata fake Pastors au servnt wapo na wanaendelea kupotosha watu. Hivyo kuwepo kwa fake servant haimaanishi kuwa wenye wito halisi (Watumishi wa Kweli) hawapo, wapo na wanatenda kazi hata sasa.

Kwako MWANDISHI.....

Si kila kinachoandikwa au kushauliwa na wazungu kwetu (Africa) ni sahihi, BIG NO! na hili ndio tatizo kubwa linalotusumbua sisi, tunaamini kila ushauri unaoletwa na White People.

Labda cha kukusaidia Mwandishi...

Msaada pekee wa Waafrica unatoka kwa Mungu (Watumishi wake) na sio kwa wazungu, hata wewe kuwa hapo ulipo na kuanza kutembea na hizo "Side effect" za hao fake Pastors kuchafua watumishi halisi wa Mungu ni kutokana na msaada (Maombi) wa hao watumishi wa Mungu na kingine. Hivyo before hujawashambulia all Paators tambua kuwa kuna wengine unawaonea bila sababu.

Ubarikiwe. - Mwl Deus M.Ndololo
 
Hakuna Nabii wa MUNGU Akiyepewa Biblia ,Yesu Alipewa Injili Biblia ni theolojia za wazungu kuwahadaa watu ndio maana kuna makosa na mapungufu mengi unajua kabisa MUNGU ni Mkamilifu Sasa mbona achanganye Maneno unajua KBS. Huu ni uchakachuaji wa Binadam ,Open ur minds guys
 
Japo Mimi nimlokole kabisa lakini huu ujinga nimeachana nao siku.
Hii Mungu akubariki Fanya KAZI kwa bidii.
Akili kichwani, imani moyoni, pesa mfukoni.
 
Mr Deus labda hujaelewa andiko langu mimi sijasema wachungaji wote ni fake rahasha nimewataja baadhi ya hao wanaodanganya waumini kwa mahubiri yao ya uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…