Waafrika tusingetawaliwa tungekuwa wapi hii leo?

Waafrika tusingetawaliwa tungekuwa wapi hii leo?

Swali hili ni swali la manung'uniko! Hasa lingilenga hali ya bara la afrika ilivyo kwa sasa kimaendeleo likilinganishwa na mabara mengine.
"Waafrika" Tusingetawaliwa tungekuwa wapi hii leo? Yaani kutawaliwa kwa bara la afrika imekuwa kama "favour" ya hata kuwa na vijimaendeleo kidogo tulivyo navyo!

Amerika iliwakutawaliwa na Waingereza! Na nchi Nyingi sana Duniani zimewahi kutawaliwa na mataifa tofauti tofauti!
Amerika ilianza kuendelea kwa Kasi baada ya Kujitawala yenyewe, mwingereza alikuwa anachuma na Kujenga London tu.
Je? Unafahamu Afrika ilishawahi kuivamia Ulaya na Kuipiga vibaya? Kabla ya kutawaliwa na Wazungu.

Je unafahamu teknolojia za awali kabisa za uvumbuzi zilipatikana Afrika! - Iron technology! irrigation Skills and etc.Kabla ya kutawaliwa na Wazungu.

Nyakati na Mwamko wa fikra unaweza kubadili hali halisi ghafla! Wakwanza akawa wa mwisho na wa mwisho akawa wa kwanza!
What went wrong?
Tuzidi kupambana na Matamaa ya Madaraka Kisiasa,Kuridhika Mapema na Kukata Tamaa tutawapita haooo.
High Hopes!
Hizi story za kufikirika huwa mnazitoa wapi ?

Afrika ipi iliwahi kuitawala Ulaya ?
 
Swali lako zuri lakini lina makosa katika kudhania (assumptions).

a. Marekani na China zote ni nchi zilizowahi kutawaliwa na wengine. Ethiopia na Liberia ni nchi za Kiafrika ambazo hazikutaliwa na nchi nyingine.

b. Kutaliwa peke yake hakuwezi kuwa kipimo cha nchi kuwepo au kutokuwepo katika hali fulani. Na bahati mbaya nchi nyingi ambazo zimekuja kutawala wengine nazo ziliwahi kutawaliwa...

c. Kutaliwa si sababu ya kushindwa kufanya jambo lolote, na kutawala wengine si sababu ya nchi kufanikiwa kuliko nchi nyingine.
Wamarekani wa leo ndio wale waingereza walioamua kuishi kwa kukataa remote control ya London. Wakaona wajiwekee utawala wao.
 
Tungekuwa tunaishi maisha ya upori pori yasiyo na ustaarabu wa kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Mzungu kaistaarabisha Africa. Kutoka kwenye usokwe sokwe mpaka kwenye utimamu wa akili. Kusoma, kuvaa, kukaa darasani, mifumo ya utawala, mifumo ya fedha na biashara, vyote tumejifunza kwa mzungu.
Samori toule muafrica alipambana miaka 12 na mfaranca,Leo jaribu bongo ikipige na mturuki tuu tuone Kama tutapambana hata 4 years .
chief mkwava buhehe alikuwa na kiwanda Cha magobole, kiwanda Cha mapanga. Tungekuwa mbali sana ndio maana wanaitwa wanyonyaji
 
Unamwaibisha GODZILLA huko alipo
Hebu kale msasa History Form 2
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mwambie mkuu hapo juu akasome kitabu HOW EUROPE UNDERDEVELOP AFRICA by Walter Rodney alafu aje kusoma upya alichokiandika mwandishi anasema mpaka kufikia karne ya 15 Afrika na Ulaya ilikuwa sawa karibia nyanja zote, sasa mkuu hapo juu sijui amefundishwa na nani huo mtazamo,haya ndio madhara ya kufundishwa na walimu wasiopenda kazi zao .Historia uweza kumfanya mtu aendelee au kumnyong'onyesha mtu.
 
Back
Top Bottom