Waafrika wanalazimisha mafanikio ya Morocco yawe ya Waafrika wote

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Sijui ni tumerogwa au haya yote ni sababu ya elimu duni au Mungu ndo alivyo tuumba yaani sijui jamii yetu ya kiafrika ina matatizo gani.

Waafrika ndio jamii pekee ambayo utapambana kwa nguvu zako kusoma kwa shida lakini ukipata kazi wanataka mshahara unao upokea uwe wa ukoo mzima.

Waafrika ndo jamii pekee ambayo utapambana peke yako kutafuta mafanikio kwenye maisha yako saa nyingine kuhatarisha mpaka maisha yako ili ufikie hayo mafanikio , lakini baada ya kupata huo utajiri wana razimisha uwe wa ukoo mzima.

Mfano angalia waafrika wanavyo razimisha mafanikio ya Morocco yawe ya waafrika wote.
Tena unakuta jitu zima ambalo kwa kuliangalia utasema ni jitu lenye akili ,lakini unakuta eti lina lalamika kuhusu kauli iliyo tolewa na naodha wa Morocco aliye sema ushindi wa Morocco ni wa na waarabu eti waafrika wamebaguliwa.

Jamaa aliongea ukweli kwa sababu timu yao imeandaliwa na mpaka sasa inahudumiwa kwa pesa za walipa kodi wa Morocco na si za waafrika ,sema tu waafrika ni jamii iliyo zoea kulalamika hata kwenye mambo ya kijinga

Ww unaye razimisha ushindi wa Morocco uwe wa waafrika wote kwa mchango upi ulio wapa mpaka kufikia hayo mafanikio yao?

Morocco inatumia mamilion ya $ ya kodi za wamoroco kuwekeza kwenye kwenye soka kuanzia kujenga viwanja vya kisasa na akademi ,wakati ss huku Tz viwanja vyote CCM imevingangania wakati hata kuviendeleza imeshindwa.

Kama unaishabikia Morocco ishangilie kwa sababu unapenda inavyo cheza au kuna wachezaji unawahusudi lakini sio kwa sababu uchwara eti ni wawa kilishi wa Afrika, ishabikie kama mnavyo shabikia uhispania, Ujerumani,Ubeligiji ambazo hazina uhusiano wowote na waafrika.

Waafirika ni watu tunao penda kupata matokeo hata kama hatujafanya mtihani.

Unakuta mtu hataki uwepo wa single mother mitaani lakini kwenye uzi wa kula tunda kimasihara ana simulia jinsi ambavyo ameshala kula mabinti zaidi ya 7 kimasihara tena bila kondomu.

Waafrika tuache unonko tufanye mambo yetu sisi kama sisi tuache tabia ya kijishikiza nyuma ya jamii nyingine kwa vigezo uchwara.
 
Kiasili waafrika ni wajamaa. Zamani kidogo hapa kwetu uliweza kwenda kijiji chochote ukajitambulisha kuwa unasafiri na unahitaji malazi na ukapewa na chakula na maji ya kuoga. Uzungu ndo unatutoa kwenye ujamaa ila bado upo katika viwango kama hivi vya mpira wa miguu. Ghana inashinda Tanzania tunashangilia. Huenda itafika wakati itapotea na kila mtu atafata mambo yake.
 
We naye hamnazo, Sawa pengine Waafrica hatuna mchango wowote kwenye kwa timu yao kwasababu hatulipi kodi za nchi yao Ndio maana walitubagua wakati wa kuongea kwao, lakini je umewahi kujiuliza wale Waarabu na Waislam wasio wa Morocco ambao walikuwa dedicated kwenye ushindi huo wanamchango gani kwenye mali/kodi za Morocco zilizotumika kuiandaa timu yao?(Maana Siye hatuna mchango wowote kwenye kodi)
 
Mechi ya final AFCON kati ya Senegal vs Misri,wengi walishangilia Senegal na kuwabeza Misri kua ni waarabu sio waafrika!

Sasa inakuaje tena tunajipendekeza kwa Morocco? leo hii nina uhakika ikicheza Morocco vs Ghana,nyie wote mnaolalamika kubaguliwa mtaishangilia Ghana na mtaona Morocco sio waafrika! halafu acha kuchanganya Uarabu na uislamu,hakuna mchezaji wa Morocco aliyetaja uislamu,kama hujui wapo waarabu ila sio waislamu bali ni wakristo,

Tuache unafiki kwanza,ubaguzi tunao sana ila sisi kubagua hua tunaona ni sawa ila tukibaguliwa ndio tuna anza kulia lia.
 
Kama hufuatilii mambo bora ukae kimya,Eti hakuna mchezaji wa Morocco aliyetaja Uislam! Sema wewe hufuatilii mambo!! Khs wao kubaguliwa ndani ya Africa na Waafrica weusi ni kutokana na tabia zao za ubaguzi za enzi na enzi!!!
 
Maana yake wewe unampangia mtu kutumia mshahara wake. Amesema yeye dedication kwa waarab, sasa unamkataza kama nani
 
Kama hufuatilii mambo bora ukae kimya,Eti hakuna mchezaji wa Morocco aliyetaja Uislam! Sema wewe hufuatilii mambo!! Khs wao kubaguliwa ndani ya Africa na Waafrica weusi ni kutokana na tabia zao za ubaguzi za enzi na enzi!!!
Basi hapo mwenyewe unaona umeandika bonge la point.. πŸ˜€ πŸ˜€

Leta ushahidi kama kuna mchezaji alitaja dini,na unaposema wana tabia za ubaguzi toka enzi na enzi.hebu tuambie hizo tabia za toka enzi na enzi ni zipi? au unaongelea ubaguzi wa enzi na enzi wa mzungu kwa muafrika? au wewe ndio wale wanaomuabudu mkoloni?
 
Kwa mtazamo wangu binafsi, kuishabikia Morocco kisa inatoka Afrika naona ni utaahira. Ila kama ndo timu yako ya toka utotoni Sawa.

Na kuona ushindi(mafanikio) ya morocco kuwa ni ya Afrika mzima huo ni upumbavu. Ni Sawa na kusema Argentina akibeba uwe ni ushindi wa Amerika ya kusini NZIMA. Au France akibeba uwe ni ushindi wa Ulaya nzima.

Huo ni utaahira
 
Maana yake wewe unampangia mtu kutumia mshahara wake. Amesema yeye dedication kwa waarab, sasa unamkataza kama nani
Simkatazi lkn mie nam Jibu huyo hapo anayetuponda siye tunaowananga hao Waarabu!!!


Mie pia natumia kipato changu kusema Waarabu wajuane wenyewe
 
Siwezi kuhangaika na mtu asiyefuatilia mambo
 
Wao ndo wanajua faida yao na ndio maana waliwataja na wakawaacha nyinyi.
 
Mkuu umeongea kweli kila mtu apambanie taifa lake tuache tabia ya kurazimisha kutembelea kwenye migongo ya wengine.
 
Hii ni kweli haswa fainal ile Senegal akashinda waliwabeza sana waarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…