Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuna kundi kubwa la Waafrika waliofurahia na kushangilia sana ushindi wa Trump, kila nikisikia au nikisoma sababu wanazozitoa kumuhusudu Trump naona kama mfumo wao wa umeme kichwani una hitilafu, Tuangalie hoja moja ya kupunguzwa msaada na utegemezi wetu kwa mfano
Wale wanaosema misaada ya US itapungua kwa nchi za Africa na mashirika ya UN kama WHO hivyo tutajitegemea wanafikiria kivivu kwa kushindwa kuunganisha mambo. Chukulia mfano Tanzania ambayo inapokea msaada wa karibia $Million 500 kwa mwaka kutoka US, hivi kupungwa kwa hizi fedha kweli ndio kutaifanya serikali ya CCM kubadili sera zake za matumizi kwa viongozi na vitu visivyo vya kipaumbele??
Kupunguzwa kwa misaada ni hasara kwa watu masikini wa vijijini kwa sababu viongozi hawawezi kubadili mtindo wao wa maisha kwa kupunguzwa au kuondolewa msaada, mfano mzuri ni Zimbabwe.
Watakaoumia ni raia wanyonge wanaotegema Zahanati, ARVs, chanjo na condoms za ruzuku kutoka US.
Misaada ikipunguzwa au ikikatwa China ipo na fedha nyingi tu ila ni mkopo , viongozi watabadilisha mitaa kutoka Washington kuelekea Beijing huku raia wategemea misaada wakiumia zaidi kulipia mikopo ya Kichina kugharamia Afya kwa mfano, Sahauni hilo suala kwamba eti matumizi mabovu yatapunguzwa.