Waafrika wanatia aibu sana

Waafrika wanatia aibu sana

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
11,880
Reaction score
10,372
Tukio lililotokezea hivi karibuni kwa Mmilikiwa Club ya Napoli nchini Italia kuzungumzia kuwa kwa sasa hatapendelea tena kusajili wachezaji kutoka Africa kwa sababu ya kuwa wamekua wakim cost sana inapokuja suala la wao kwenda kucheza AFCON kati kati ya msimu Limegeuzwa na kufanywa kuwa ni jambo la kibaguzi.

Kwenye mitandao ya kijamii Waafrica wamejikusanya kwa wengi mno wakiwa wanaporomosha matusi na kutilisha huruma kuwa huyo mzee amewafanyia Ubaguzi.

Mpaka lini tutaendelea kutia aibu kama hivi? waafrica hatuwezi criticizing wala rejection za aina yoyote ile sisi tunahamishia kwenye Ubaguzi. Siku zote tumekua ni watu wa kutilisha huruma ya kipuuzi tu na kuficha madhaifu yetu kwenye kichaka cha Ubaguzi.

Napoli president slammed for 'lack of respect' to Africa by Nigeria coach Abdallah
 
Mashindano ya Africa Kila baada ya miaka miwili hayana mvuto yamekaa ki mapato zaid.
 
Hata fergusson enzi zake alikuwa hataki wachezaji wenye asili ya Africa unamtegemea mtu halafu anaondoka kati kati ya mashindano anaenda afcon.
 
tuna takiwa kuishi ktk malengo yetu na wao yao, kama malengo yao na yetu hayafanani basi kila mtu ashike chake, sio busara wao kutupangia au kutuburuza kwa manufaa yao zaidi... zipo klabu nyingi tu zina hitaji wachezaji kutoka afrika, na Napoli haito kwepa kusajili mchezaji toka afrika kama atakuwa ni bora...

mfano wamuache kumsajili Mane au Salah kisa AFCON?
 
Hata fergusson enzi zake alikuwa hataki wachezaji wenye asili ya Africa unamtegemea mtu halafu anaondoka kati kati ya mashindano anaenda afcon.
lakini wenger, mourhno, pep etc waliwatumia...
 
tuna takiwa kuishi ktk malengo yetu na wao yao, kama malengo yao na yetu hayafanani basi kila mtu ashike chake, sio busara wao kutupangia au kutuburuza kwa manufaa yao zaidi... zipo klabu nyingi tu zina hitaji wachezaji kutoka afrika, na Napoli haito kwepa kusajili mchezaji toka afrika kama atakuwa ni bora...

mfano wamuache kumsajili Mane au Salah kisa AFCON?
Basi wachezaji wetu wasiende kwenye vilabu vyao sababu January ndio league zimechanganya hapo wa kushuka daraja ana pambana kubaki na wa ubingwa ana pambana arafu mchezaji mhimu anaondka huoni ina athari kwenye timu? alf mpira ni vizuri twende pamoja sababu kuna sehemu tuna link dunia nzima
 
Yaani wewe umeona hilo tu?
Kosa la waafrika silioni sababu wao wanatetea utamaduni wao ambao ni afcon imekuwa tangu miaka na miaka .
Mbona pia hujasema pia alisema na yale mashindano ya Amerika kusini pia huko hatosajili?
 
Huo ni mtazamo wake,ata hivyo timu sio Napoli tu.licha ya hivyo hiyo Napoli mbona ni timu ya kawaida tu.Dunia ina miezi 12 tu ya mwaka na kwa vyovyote vile majira na nyakati lazima vitakua tofauti.kwahiyo mambo yote lazima yafanyike hivyo hivyo kwasababu haiwezekani kupata vyote.Naunga mkono kua huyo bwana alichojaribu kukitengeneza ni ubaguzi kwasababu kabla yakulaumu Afcon alitakiwa ajue sababu ni nini hadi michuano hiyo inaingiliana na ratiba za ligi za kwao.
 
Hata fergusson enzi zake alikuwa hataki wachezaji wenye asili ya Africa unamtegemea mtu halafu anaondoka kati kati ya mashindano anaenda afcon.
Kwani wanasajiliwaga timu nzima hadi wakiondoka timu ipwae?.Hivyo ni visingizio tu wanajaribu kuvileta.
 
Back
Top Bottom