Waafrika wengi kwa asili tunachukia kusoma, tukisoma ni kwajili ya vyeti vitupe maslahi tu, home library ni sawa na kutafuta sindano kwenye nyasi!

Waafrika wengi kwa asili tunachukia kusoma, tukisoma ni kwajili ya vyeti vitupe maslahi tu, home library ni sawa na kutafuta sindano kwenye nyasi!

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Ndio maana inafikia kipindi wanafunzi wanapigwa, ni kwasababu ya kulazimisha mtu afanye asichokipenda by nature. Kuna shuhuda nyingi sana utazisikia, "Bila viboko nisingeweza shule". Hata wale wanaosoma kwa bidii shuleni ni kwa lengo la kupata vyeti wakiwa na mategemeo ya kimaslahi hasa ajira, sio kwajili ya kupenda kusoma !!

Kwa waafrika issue ya kusoma shule/chuo imekuwa ni kwa ajili ya kupata vyeti hata kwa kukariri bila kujua maana ya kinachosomwa, ushahidi wengi wakimaliz shule hawaji tena kugusa vitabu, hata ile siku ya kumaliza shule/vyuo hufurahi kwa kutupa madaftari, vitini, kuuza vitabu, n.k. ni ishara ya kuutua mzigo uliowachosha ila waliubeba kwajili ya mategemeo ya kimaslahi.

maktaba / library uanachama kwa mwaka ni shilingi elfu kumi tu lakini ni watu wachache sana wanaenda na katika hao asilimia kubwa wanasomea mambo ya shule / chuo wala sio kujisomea vitabu kujiongezea maarifa binafsi, huwezi kuja kusikia malalamiko hata ya vitabu kuwa vya zamani sana ama vichache, jibu rahisi ni kwamba hakuna watu wenye interest ya kujisomea.

Ukija kwa Wazungu hata hata kama kaishia la nne unakuta anapenda kujisomea vitabu kujiongeza maarifa, kila mwezi anaweza kusoma kitabu kimoja. ni kiu ya maarifa !! ipo ndani ya damu yao kama Waafrika tunavyopenda starehe!

Kwa wazungu ni kawaida kuingia nyumba ya mtu unakutana na home library, ama chumbani kuna vitabu kadhaa, ni kwamba tayari huyo mtu kakuzidi maarifa mengi sana, wewe uliepiga msuli kukariri definitions na forumula ili kupata cheti ni ngumu kumkuta kimaarifa.

wanajua kwamba kuna pdf za bure lakini wananunua vitabu kwasababu wanathamini maarifa na kuwapa support waandishi watoe vitabu zaidi.

1718656443796.png
 
Ndio maana inafikia kipindi wanafunzi wanapigwa, ni kwasababu ya kulazimisha mtu afanye asichokipenda. Kuna shuhuda nyingi sana utazisikia, "Bila viboko nisingeweza shule".

Hata wale wanaosoma kwa bidii shuleni ni kwa lengo la kupata vyeti wakiwa na ndoto za ajira ama kujiajiri wapate maslahi kwa kuambiwa, "Kazana kusoma utapata kazi nzuri", siyo kwajili ya kupenda kusoma.

Vitu pekee watavyosoma vitahusu namna ya kufaulu mitihani, nje ya hivyo ni mzigo hawana muda navyo. Ni kawaida kukuta wakimaliza shule/vyuo hufurahi kwa huchoma madaftari, kuuza vitabu ama wakibaki navyo vitajikusanyia vumbi.

Waafrika wengi hatuna utamaduni wa kujisomea kujiongezea maarifa binafsi.

Ukija kwa Wazungu mtu hata kama kamaliza darasa la saba anapenda kujisomea vitabu kuongeza maarifa, kila mwezi anaweza kusoma kitabu kimoja. Yaani ana kiu ya maarifa, hatishwi kwa viboko wala mategemeo ya kimaslahi, ipo ndani ya damu yao kama Waafrika tunavyopenda zaidi ngoma!

Unaingia nyumba ya mtu unakutana na home library, tayari huyo mtu kakuzidi maarifa mengi sana

View attachment 3019376
Una ambiwa ukitaka kumficha mtu mweusi jambo weka kwenye maandishi. Sisi ni wavivu kusoma sana.
 
Kwasababu wao wazungu toka mtoto yuko mdogo anasomewa vitabu je wewe hapo ulikuzwa ukiwa unasoma vitabu vya hadithi tu ?Hapa ndio waafrika tunachemka ujue tabia hujengwa
 
Issue ya kusoma ukiwa shule ni kwa ajili ya kufaulu upate cheti chenye daraja zuri tu, ili ukapate ajira!.

Hata ukisoma mavitabu kaka yote ukajua sana hapa Afrika siyo sehemu ya wenye ujuzi bali vyeti vyenye ufaulu.

Sasa usome mavitabu ili iweje, utaongeza knowledge, hekima n.k alafu unabaki hapa JF kutoa nondo tu!.
 
hayo yote ni kwasababu ya umaskin tulio nao tena umaskini wetu ni mbaya sana maana ni wa kurisishana alfu tunabebana kama ng'ombe. ngoja nianze kununua vitabu sasa
 
hayo yote ni kwasababu ya umaskin tulio nao tena umaskini wetu ni mbaya sana maana ni wa kurisishana alfu tunabebana kama ng'ombe. ngoja nianze kununua vitabu sasa
Afrika ni masikini kwenye maarifa lakini ni tajiri wa rasilimali, bila maarifa hata rasilimali zinakuwa ngumu ku manage

mataifa mengi yamewahi kuwa maskini lakini walipowekeza kwenye maarifa walifanikiwa, tunashushudia nchi hazina madini wala mafuta lakini zinauza ideas kama teknolojia kwa mabilioni ya dola
 
Back
Top Bottom