Waajiriwa ndio wana muda gym na Jogging, Wafanyabiashara hawana huo muda

Hapa nipo kwenye shamrashamra za kili marathon tangu ijumaa na ofisi yangu haijafungwa weekend yote. Acheni kuwa na mawazo na kufanya mambo kizamani. I can operate from here.
Si ulisema unafunga biashara Kwasababu ya TRA
 
Kuna uzi unazungumzia mikasa ya ofisin/makazin naomba title kwa anayeujua
 
Mo dewji yule pale katika rat8ba yake bize ila ametenga saa moja la kufanya mazoezi.
 
Mfanyabiashara hana muda wa ujinga ujinga huo
Masharti ya afya ni ujinga!! Wafanyabiashara ndiyo wana hela na muda wa jogging na gym. Ukimbie jogging kazini umeajiriwa utawahi saa ngapi. Mfanyabiashara kajiajiri anajipangia muda wa kuingia na kutoka! Na kaajiri watumishi asipokuwepo
 
Huo ndio ukweli
 
Biashara ambayo inahitaji uwepo wako si salama.

Kuna watu biashara zao zawafanya hawakutani na familia ie Wauza bidhaa za sokoni, Maduka ya Mangi
So inahitaji uendeshe kwa simu? Sikiliza biasjara inahitaji mwenye Idea awepo, na sio kuweka shangazi, mke, mjomba, sijui shemeji wasimamie,
 
Mo dewji yule pale katika rat8ba yake bize ila ametenga saa moja la kufanya mazoezi.
Mo dewji ni levo nyingine yule sio Director kwanza, yaani yule ni Chairman ni kama Mengi, alivyo kuwa, au Dangote, Sasa hio levo ni ya mbali, tuzungumzia hawa wadogo
 
Nyongeza. Katika uchunguzi wangu, ni waajiriwa na wafanyabiashara wenye vipato vizuri ndio hupata muda wa kwenye Gym au joging.

Mwajiriwa na mfanyabiashara wa kipato cha chini mwenye majukumu hana hamu ya kwenda Gym, full stress za maisha. Si unajua ukitoka Gym inatakiwa uoge, ule vizuri. Sasa unaanzaje kuaga familia unaenda Gym wakati familia haijui itakula nini usiku!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
kulala saa 7 usiku kuamka saa 11 asubuhi na kuwai daladala ni gim tosha
 
Nafikiri huu ni mtazamo wako mwembamba waliojiajiri wengi. Hasa wenye mitaji mizuri na investment za maana hupangilia muda wake awe wapi kwa wakati gani. Manake kuingiza kwake pesa hakutegemei yeye kuwepo cite. Eneo la biashara.
Muajiriwa ratiba ikichenji tu humuoni gyme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…