Waakuu hii ramani inamakosa gani?

Ndiyo nyumba ni yako una haki master yako iwe kama uwanja wa tenesi ila mbona unawapunja watoto vyumba vyao vinakuwa kama store kisa umewawekea choo!.
 
Huo mlango wa Bedroom 1 ungesogea na kubana upande wa public toilet halafu huo wa kutokea sitting room kwenda vyumbani usogeze kuelekea upande wa kitchen.

Lengo hapo kwanza ni kuweka privacy ya choo. Mtu anaweza banwa na tumbo hapo anakwenda chooni huku sebuleni mtasikia kila kitu au kuna wale watu wanachoo kina toa harufu babukubwa italeta matatizo especially hiyo harufu ikitoka huko toilet na kuja maeneo ya jikoni dining na sebuleni.

So its better mkajitahidi sana kuzingatia swala la privacy ya choo. Mimi napenda choo kiwe kimejificha huko mwisho wa korido tena kiwekewe korido ya pekee yake yaani ukiwa unaingia toilet unakuwa pekee yako na hata mtu akija unajua amekufuata na sio choo kipo katikati ya korido watu walipita halafu wewe ndio unashusha kombola unashangaa mtu anaguna kwanza kwa mbali maana wanasikia kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…