Waakuu hii ramani inamakosa gani?

Waakuu hii ramani inamakosa gani?

Screenshot_20230305_174426.jpg
Hapo wawekee mabinti zako choo chao, wawe huru.
 
Nimetafuta raman ya nyumba simple simple nimekutana na hii naomben ushaur kwenye hii ramani

View attachment 2534059

BAADA YA MAONI YA WATU NIMEKUJA NA UPDATES YA RAMANI YA PILI HII HAPA

NAYO MNAIONAJE MSICHOKE WAKUU KUNISHAURI


View attachment 2538259
Ndiyo nyumba ni yako una haki master yako iwe kama uwanja wa tenesi ila mbona unawapunja watoto vyumba vyao vinakuwa kama store kisa umewawekea choo!.
 
Huo mlango wa Bedroom 1 ungesogea na kubana upande wa public toilet halafu huo wa kutokea sitting room kwenda vyumbani usogeze kuelekea upande wa kitchen.

Lengo hapo kwanza ni kuweka privacy ya choo. Mtu anaweza banwa na tumbo hapo anakwenda chooni huku sebuleni mtasikia kila kitu au kuna wale watu wanachoo kina toa harufu babukubwa italeta matatizo especially hiyo harufu ikitoka huko toilet na kuja maeneo ya jikoni dining na sebuleni.

So its better mkajitahidi sana kuzingatia swala la privacy ya choo. Mimi napenda choo kiwe kimejificha huko mwisho wa korido tena kiwekewe korido ya pekee yake yaani ukiwa unaingia toilet unakuwa pekee yako na hata mtu akija unajua amekufuata na sio choo kipo katikati ya korido watu walipita halafu wewe ndio unashusha kombola unashangaa mtu anaguna kwanza kwa mbali maana wanasikia kila kitu.
 
Back
Top Bottom