Waalimu acha kuhamishia hasira zenu kwa watoto wetu, Rais Samia yuko pale pambaneni naye.

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Hizi adhabu za viboko zipigwe marufuku kabisa! Haiingii akilini mwalimu kupiga watoto namna hii kama anapiga mbwa koko. Kama hamna uvumilivu achaneni na kazi hii badala ya kuumiza watoto wetu!

Huyu mwalimu mwehu asakwe popote alipo na apate stahili yake kisheria!
 
Mimi mwenyewe naona zifutwe fimbo mashuleni , mwanafunzi aje SHULE au asije, afeli au afaulu , asome asisome ni shauri yake na wazazi wake . Ibaki adhabu ya kufukuzwa na ma suspension TU . Kila mtu akapambane na wanae maana walimu wakifaulisha na kuwarudisha kwenye mstari watoto hata husikii vyombo vya habari vikimsifia ila akosee mara moja TU ni jela
 
Tunaposema mfumo wa elimu hauko sawa tunamaanisha kwa upana mkubwa sana aisee

Ni hatari wanafunzi kufundishwa na walimu wenye stress za maisha, Ni hatari wanafunzi kufundishwa na walimu wasio na mbinu za kuishi na wanafunzi matokeo yake hutreat wanafunzi kama mbuzi.

Mfumo wa elimu unahitaji reform kubwa kuendana na kasi ya maendeleo ya Dunia.
Zigo hili la kumuadhibu mwanafunzi bila shaka Serikali itamuachia mwalimu na hata kumfungulia mashitaka au hata kumfukuza kazi ilihali yenyewe ndio inapaswa kuwajibishwa kwa kusajiri walimu wasio na mbinu za kuishi na wanafunzi.
 
Mimi ndio maana nilivyokuwa Darasa la 7 kuna ticha mmoja niliwahi kupambana naye nikamzidi maujanja nikamuachia kipigo🐼
 
Shida wazazi ni wapumbavu

Wanafunzi wakiwa haina nidhamu mnawalaumu walimu

Wanafunzi wakifeli lawama kwa walimu

NB
ADHABU YA VIBOKO IPO ILA INA UTARATIBU AMBAO ASILIMIA 90 HAUTEKELEZWI NDIO MAANA CHANGAMOTO KAMA HIZO ZINATOKEA
 
📌📌📌
 
Huyu mbona cha mtoto kipind nasoma high-school sengerema pale
Kuna siku mwalimu bhana akanisema kwamba hatujaamka prepo ya satisa usiku

Oya babu tulipigwa fimbo hizo mpaka makalio yakawa yanalia mbwata nilikua nakalia tumbo wiki nzima 😅

Sema ndo hivo mwalimu nimekutana nae juzi tunapiga story
 
Hizi adhabu za viboko zipigwe marufuku kabisa! Haiingii akilini mwalimu kupiga watoto namna hii kama anapiga mbwa koko. Kama hamna uvumilivu achaneni na kazi hii badala ya kuumiza watoto wetu!

Huyu mwalimu mwehu asakwe popote alipo na apate stahili yake kisheria!View attachment 3260238
Watajuana bwana.

Mitano tena
 
mtuma post naona umeishatoa hukumu hata kabla ya kubalance story, huo ni upande mmoja wa mwanafunzi,je mwalimu huyo yuko peke yake tuu katka shule hiyo? hakuna mkuu wa shule,makamu,mtaaluma,mwalimu wa nidhamu,mwalimu wa darasa na wadau wengine hadi apigwe picha huko vichochoroni amefikaje hapo?
 
Zamani tulikuwa tunapewa adhabu za viboko lakini kwa utaratibu mzuri.
Adhabu ya viboko ilikuwa inatolewa kulingana na uzito wa kosa! Kulikuwa na adhabu nyingine mbadala wa kupiga viboko!
Lakini nyakati hizi walimu wanapiga kiholela wanavyotaka!
 
Tunaposema mfumo wa elimu hauko sawa tunamaanisha kwa upana mkubwa sana aisee

Ni hatari wanafunzi kufundishwa na walimu wenye stress za maisha, Ni hatari wanafunzi kufundishwa na walimu wasio na mbinu za kuishi na wanafunzi matokeo yake hutreat wanafunzi kama mbuzi.

Mfumo wa elimu unahitaji reform kubwa kuendana na kasi ya maendeleo ya Dunia.
Zigo hili la kumuadhibu mwanafunzi bila shaka Serikali itamuachia mwalimu na hata kumfungulia mashitaka au hata kumfukuza kazi ilihali yenyewe ndio inapaswa kuwajibishwa kwa kusajiri walimu wasio na mbinu za kuishi na wanafunzi.
reform kwenye katiba kwanza ndo tushuke huku chini sababu waliopo madarakani sio machaguo ya wananchi na hawawajibiki kwa wananchi ,hawana weledi na ujuzi katika nafasi zao ndomaana wanahamishana kila kukicha,wanaotutawala sifa yao ni kkk,kazi kusema tuu ndiooooooooooo
 
Hasira ya kuitwa kwenye semina isiyokuwa na malipo huku ukitumia pesa zako takribani 25k kwa ajili ya nauli na chakula.
Wanashiriki kuiba kura ili ccm ishinde ukiwauliza wanakwambia " wana vapo"
 
reform kwenye katiba kwanza ndo tushuke huku chini sababu waliopo madarakani sio machaguo ya wananchi na hawawajibiki kwa wananchi ,hawana weledi na ujuzi katika nafasi zao ndomaana wanahamishana kila kukicha,wanaotutawala sifa yao ni kkk,kazi kusema tuu ndiooooooooooo
No reform, poor election
 
Hizi adhabu za viboko zipigwe marufuku kabisa! Haiingii akilini mwalimu kupiga watoto namna hii kama anapiga mbwa koko. Kama hamna uvumilivu achaneni na kazi hii badala ya kuumiza watoto wetu!

Huyu mwalimu mwehu asakwe popote alipo na apate stahili yake kisheria!View attachment 3260238
Watoto wanafanyiwa ukatili mkubwa sana .
Wanafunzi sio wahalifu.
Hata wahalifu wana haki zao .
Wanafunzi ni rasilimali inayoandaliwa na taifa ili itumie vipaji vyao kulijenga taifa la kesho.
Walimu wamepewa jukumu la kufundisha na kuibua vipaji walivyo navyo wanafunzi .

Wakati mwangina mtoto anapigwa na kuumizwa vibaya kwa sababu ya kipaji chake.

Mwingine anaitwa msumbufu darsani lakini kiuhalisia unaweza ukakuta alikua anaongea mambo ya msingi kwa wenzake .
Mwingine napenda michezo sana . Mwingine napenda kuhojia na kuuliza sana.
Mwingine anaelewa haraka na mwingine taratibu . Walimu wanalipwa ili kufanikisha ndoto za watoto wetu sio ndoto zao peke yao hao walimu.
 
Back
Top Bottom