WAALIMU NAOMBENI USHAURI WENU HAPA KUHUSU HILI.Kwa waalimu tu.

WAALIMU NAOMBENI USHAURI WENU HAPA KUHUSU HILI.Kwa waalimu tu.

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Nilianza kazi mwaka2008 katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo katika shule ya sekondari Matipwili Km100kutoka Dar.Nikatumika ipatayo miaka4.Ukatokea utaratibu kwamba anaetaka kusoma ni kwa zamu.Jamaa mmoja akaenda kusoma na mie mwaka wangu2011 ikawa zamu yangu.Ilipofika mwezi wa tano nikaaply TCU Na pia ilipofika mwezi wa7 nikapata barua ya uhamisho kuhamia Chalinze.Nikaripoti kule na nikaanza kazi hadi mwezi wa9 na pia Tcu wakatoa majibu kua nimechaguliwa chuo kikuu.Taarifa na ruhusa kwenda kusoma vilitangulia kwa DEO Nikiwa Shule ya awali.Nikaandika Barus ya Ruhusa Mkuu wa shule Mpya akaipitisha ila DEO Akaniambia hatutokupa ruhusa airisha usome mwakani.Kwangu ilikua vigumu kwani nimekaa miaka4mbugani katika mazingira magumu na shida ya usafiri kwa kua nilikua na Diploma nikaona hainitoshi.Nilivumilia miaka4Porini kule lakini uvumilivu wangu ulikua bure.Mwezi wa 10nikawaaga shule kua nikaombe kuahirisha mwaka ila ilishindikana nikaamua nianze masomo.Mwezi huo wa kumi nikakatiwa Mshahara na kwa mwaka wa kwanza nilisoma kwa tabu sana na hadi mkate unakula uliooza.Nikamwomba Muumba anipe uvumilivu.Nikaenda wilayani nikamkuta jamaa mmoja anaitwa chilipwele akaniambia kama unataka mshahara suluhu acha shule rudi kazini.Nikaondoka nikaa kama miezi6 nikaenda ofisi ya Mkurugenzi nikitokea Iringa na nikaahidiwa nirudi baada ya siku3 maana Afisa Utumishi na DEO Hawapo.Nikarudi kama ahadi ilivyodai ila nikazungushwa tena mda ukaisha ofisi zikafingwa ila Afisa Utumishi alikuwepo.Familia yangu waliishi kwa tabu sana na bahati mbaya mke wangu alijifungua akafa akabaki mtoto mchanga ambae nilimwomba shangazi yangu akae nae mana me ni yatima.Akajaaliwa kwa sasa ana miezi sita na anaendelea vyema,Mimi naenda kuingia mwaka wa3 ila hadi sasa sijapewa barua yoyote ya kusimamishwa kazi na Kwanini sipewi Mshahara.Nimeongea na Mkuu wa shule akasema atafuatilia lakini ananifariji sioni matokeo yoyote.Waalimu wa Tanzania naombeni ushauri wenu mana sijui nianzie wapi mana nafanyiwa ubabe wa hali ya juu sana.Natoa namba ya simu mana hapa naingia mara chache komputa nimeuza ili nipate kuishi,Kama una ushauri nibip au tuma mesegi kwenda nambari 0759063942 ama 0712336687.Napata uchungu kuonewa katika nchi yangu alafu mnasema kuna demokrasia na amani.Bismillah
 
Panda Tamisemi watakusaidia mkuu, kwani vigezo na masharti umekidhi. Kesi kama hizi zilikuwepo nyingi sana na watu hawakatiwi mishahara isipokuwa kuna uhuni unafanyika, wanaacha kukuingizia kwenye ac yako wanajisevia wenyewe. Pole sana mwl.
 
pole mwl!ushauri wangu shughlka na mkuu wa shule kule ulikokuwa mpaka ukafungiwa mshahara kwan yeye ndo alotoa taarfa zako zote
 
Ok nadili na Mkuu wa shule ila ndo ananipa ahadi nimechoka
 
nenda tamisemi..au mpigie kawambwa...namba zake tafuta katika website ya bunge.. Pole mdau BUMIJA
 
Last edited by a moderator:
Kawambwa aweza nisaidia kweli
 
Naishi kwa tabu,ili niishi naendesha bodaboda angalau nisikate moto,siamini kua DEo yule angekua na uwezo wa kumfanyia binadamu hivi
 
:help:Ila naamini japo tunafanyiana utemi kila mtu atakufa tu,hata awe jeuri na mkuu vip maudongo atalamba
 
Mkuu pole kwa matatizo yote, ila naona umekosea kuandika kwenye heading kwamba ni "walimu tu" ndo inawahusu, kwa kufanya hivyo naamini utakosa michango ya wengi ambao wanafahamu kuhusu hilo kama wanasheria e.t.c nashauri waombe mods wakubadilishie title ili iwe inclusive zaidi.
 
Cha Kufanya, Kwanza andika barua ukiomba kurudishiwa mshahara wako ukijieleza kuwa upo masomoni, kisha tafuta wale maafisa utumishi watakusaidia zaidi athabu utakayo pata kama ulikuwa na promosheni hapo katikati ndio basi tena imekula kwako ila salary utapata
 
Back
Top Bottom