Waalimu wazoefu naomba ushauri wenu leo

Waalimu wazoefu naomba ushauri wenu leo

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Habarini wote, Nilianza kazi 2008 katika sekondari wilaya ya BAGAMOYO huko PWANI, na nikafanya kazi miaka4. Mwaka 2011May, nikaomba chuo kikuu na mwezi wa7 nikapata barua ya kuhama ndani ya wilaya Kuhamia huko chalinze.Nikaripoti kituo kipya na mwezi wa9 nikaitwa chuo. Mwezi wa5 2011 niliomba ruhusa ila sikujibiwa. Nikatoa taarifa nikanyimwa ruhusa,na nikaondoka. Tangu nianze first year sijapata salary hadi leo na sina barua yoyote, nimefika TSD wilaya wanadai hawana taarifa,na nikaenda kwa mkurugenzi nikaambiwa DEO ataitwa na afisa utumishi.Sikupewa muafaka nikaondoka mana mitihani chuoni ilikaribia mwaka jana. Na pia nilikua mbali sana na huko.Na mwaka juzi katika usajili wa watumishi nilienda na jina lilikuepo.Nimesoma kwa mkanda na bado miezi3 nihitimu.Jana nimepiga simu nimeambiwa nikimaliza nirudi maana makosa yalifanyika kiofisi kutokujibiwa barua mapema.3year hapa bado wiki2 tujaze mikoa ya kazi ,napata shida kua nikirudi watanifungulia hela au nijaze upya kazi?Naomba majibu ya hekima na yatoke kwa waalimu tu tafadhali.!!. 0759063942, facebook-Bumija Phd, kwa maulizo zaidi na pia mwandiko ndio huo mana natumia mobile na ni born before computer samahani kwa hilo.
 
Rudi kadai haki yako, kuruhusiwa kusoma ni haki yako kwa sababu ulishatimiza vigezo.wakulipe salary yako yote. Na wakishakupa fanya investment, ualim uwe kama security tu kwako lakini endeleza na komalia investments zako. Ukikaa kimya hiyo hela watu wataila, wakikuzingua nenda labor kawashtaki.kwa sababu uliomba ruhusa na waliiminyia makusudi, hakukuwa na sababu ya kukuzuia hata moja.komaa nao na prove them wrong kwamba walimu ni watu wa kuonewa tu.
Ila nakupa hongera sana kwa kufanya maamuzi magumu, wengine wangeendelea kujikalia tu eti kisa hawajaruhusiwa.
 
Mimi sio mwalimu, ushauri wangu ni kuhakikisha unafanya mambo yako kwa maandishi. Rudi ofisini, andika barua kudai malimbikizo ya mshahara. Yaani kitita chako kileee kama nakiona. Hongera kwa kujiendeleza na usiishie hapo.
 
Nadhani kama ulitoka kwenye ajira ya serikali sio rahisi kupata tena kazi.....tayari data zako wanazo.
Nafasi pekee uliyonayo ni kurudi kazini kama wanakupokea.
 
rudi kazini hautaajiriwa tena, kwani umekwisha ajiriwa la msingi kadai pesa yako ni haki yako, na huenda walikuwa wana kula ukiona wanaendlea kukusumbua nenda mahakamani.. mm nilisha wahi kukumbana na hali kama hiyo.
 
Kama wamekiri kuwa makosa yalikuwa yao wata kupokea na kukulipa stahiki zako zote, wala usijali mambo yatakaa sawa. Pia usiombe ajira mpya rudi kazini kwako.
 
Asanteni wote na naomba mawazo zaidi
 
Mkuu kama ulishaingizwa kwenye payroll rudi tu kituoni....

Ila usiache kupigania malimbikizo yako ukafaidisha watu bure
 
fanya yote kaka tz yetu haitabiriki omba ajira upya na wakati huohuo unarudi kazin kwenda kufait, mwakani ajira mpya zinatoka kama kazini mambo hayakukaa sawa kazin unaenda kuripoti,usitegemee sehemu moja tz yetu ni ngumu kaka
 
Hongera sana mwl.mi nakushauri urudi kituoni na ukaombe malimbikizo yako,utapewa tu.Usiombe tena ajira sbb jina lako bado lipo utumishi,hatari ya kuombe tena unaweza kukosa yote.
 
Hongera sana mwalimu kwa kujiendeleza kitaalamu,Haki ya mtu haipotei rudi kituoni ukiwa na details zako ukadai haki yako.
 
Lutsala asante kwa ushauri
 
Nadhani kama ulitoka kwenye ajira ya serikali sio rahisi kupata tena kazi.....tayari data zako wanazo.
Nafasi pekee uliyonayo ni kurudi kazini kama wanakupokea.

mkuu mfano aliyekuwa mwalimu serikalini akaenda jeshi..au hizi nafasi uhamiaji walizotoa akapata...ITAKUWA HANA MSHAHARA!!?? the point is hata ukibadili tasnia serikalini itakula kwako??.hebu weka nambo sawa plz
 
Back
Top Bottom