Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Inasikitisha sana kusikia kesi za watu wanaojiua, ama kwa kunywa sumu, kwa kujinyonga, kwa kujipiga risasi au kwa kujitupa chini kutoka ghorofani. Wanaofanya hivyo huwa wanafikiri kwamba wakijiua ndio watapumzika tabu zao. Wanafikiri kujiua ndio mwisho wa kero walizo nazo. Wanadhani wakijiua wata-rest in peace. Mawazo hayo ni potofu; tuyapinge kwa njia zote. Yanatoka kwa yule mwovu shetani na mapepo yake.
Ukweli ni kwamba kujiua ni hasara. Anayejiua kwa kufikiri anaepuka matatizo, ni sawa na mtu anayeruka majivu na kukanyaga moto. Kujiua ni dhambi(Kutoka 20:13). “Usiue” ni moja kati ya amri kumi za Mungu. Katika 1 Wakorintho 3:16-17 tunasoma pia kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mtu akiliharibu hekalu hilo, Maandiko yamenena wazi Mungu atamharibu mtu huyo.
Watendao dhambi za aina zote, wakifa, wanaenda kuteseka motoni. Kitabu cha Luka 16:22-24(SRUV) kinatupa picha ya hali ilivyo baada ya mtu mwenye dhambi kufa:
"Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Abrahamu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu."
Hivyo tuwashauri mapema, tuwaonye, tuwaambie ukweli huo wanaotaka kujiua.
Duniani kuna dhiki nyingi lakini hilo lisiwe sababu ya kumfanya mtu ajiue. Maana akijiua sekunde ile ile anaingia katika mateso mazito kuliko yale aliyokuwa anayapata duniani. Wenye mawazo ya kujiua tuwape pia Maandiko haya yenye faraja na matumaini:
Yohana 16:33
“...Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu.”
Yohana 14:1-3
“Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Katika nyumba ya Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.”
Yesu atakaporudi, wote tunaomwamini na kuishi maisha matakatifu, atatunyakua na kutupeleka mbinguni kwenye raha isiyo na mwisho. Hatutakumbuka tena tabu na dhiki za dunia hii.