Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Kwa muda mrefu, hayati Hafidh Ali alikuwa anaonekana kama taswira ya waamuzi bora kuwahi kutokea Zanzibar, akiaminiwa na IFOZA wakati huo na baadaye ZFA na sasa shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF), na hadi Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la dunia, FIFA. Hafidh Ali hakuishia kuchezesha mechi uwanjani tu, bali alipewa majukumu ya kuratibu mechi baada ya kustaafu na alikuwemo kwenye kamati za CAF akichangia uzoefu wake katika uendeshaji mchezo huo maarufu duniani. Alikuwa taswira ya uamuzi bora kwa sababu Zanzibar ilizalisha waamuzi wengine wengi baada yake ambao pia waliaminiwa na CAF na FIFA na hivyo kupewa mechi nje ya nchi.
Nimepata ukakasi mkubwa kuona namna ambavyo TFF inatumia nguvu kubwa kuwaimarisha waamuzi na viongozi wa Zanzibar ilihali tayari kuna ZFF, Ligu Kuu ya NBC ni ligi ambayo inajumuisha timu zilizopo Tanganyika maarufu kama Tanzania Bara, na sio hakuna ujumuisho wa timu kutoka Zanzibar. Sina uhakika kama kuna Waamuzi au Makamisaa kutoka Tanganyika wanaochezesha Ligi Kuu ya Zanzibar? Ila sidhani kama ZFF wana dhamira ya kukuza mpira wa Tanzania bali mpira wa Zanzibar pekee.
Katika mchezo wa Azam FC dhidi ya Coastal Union, mchezo wa tarehe 8 mwezi huu wa nane nimeshangaa sana kuona tena waamuzi kutoka Zanzibar, Ally Ramadhan pamoja na Nasri Siyah katika kusimamia sheria kumi na saba katika mchezo huu. Ni kwamba Tanganyika hatuna waamuzi? Ama hatuna watu sahihi wa kusimamia sheria hizi. Ikumbukwe kocha wa APR alichokisema kuhusu waamuzi wa Zanzibar kipindi cha nyuma.
TFF inaipiga tafua ZFF na soka la Zanzibar, kitu ambacho ni kizuri sana kwa afya ya Zanzibar ila je Tanganyika ama Tanganyika inafaidika nini? Waamuzi wangapi wazawa wa Tanganyika wanachezesha michezo ya Zanzibar? Nafahamu kuna viongozi wa TFF ni raia kutoka Zanzibar, Je kuna viongozi wa ZFF ambao ni raia kutoka Tanganyika? Kwanini TFF isitafute waamuzi kutoka Bara kuchezesha michezo yetu.