realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Kutokana na ushabiki wa Mchezo wa Mpira kukua kwa kasi ni muhimu sana wakumbuke pia kufanya mikoani ili kuwapa raha mashabiki.
Ningeshauri hata matamasha hayo yakafanyika kikanda na kuwa na mpangilio mzuri na wa Kisomi.
Kama inashindikana basi kabla ya Tamasha kubwa yatangulie matamasha madogo madogo ya kikanda ndipo kuwe na hilo Tamasha kubwa.
Mikoani kuna mashabiki wengi sana ambao wajitolea pesa zao kuwa na ofisi zao kabisa.
Kwa kuwa wengi hawana kipato kikubwa lakini pia ili kuepusha ajali zisizokuwa na ulazima ni muhimu kutafuta namna ya kuwapa raha mashabiki wenu wa mikoani.
Na katika matamasha yenu zishirikisheni timu za chini, na hadi shule za msingi ziweze kushirikishwa ili kukuza vipaji.
Tunajua hizo ni siku kubwa sana na kila mtu angehitaji kujionesha lakini iwe ni kwa maslahi ya michezo na sio ubinafsi.
Kwa kuwa siku hizo hufuatiliwa na viongozi wakubwa na watoto pia tumieni Lugha nzuri na zenye busara ili vizazi vijavyo vijifunze.
Kingine pia watoto wa Shule za msingi na Sekondari ni mashabiki wenu wazuri sana.
Wakumbukeni hata kwa kuwagawia mipira na Jezi.
Ni hayo tu.