Waandamanaji 20 wakamatwa Cameroon kwa kuchochea ghasia uchaguzi mkuu

Waandamanaji 20 wakamatwa Cameroon kwa kuchochea ghasia uchaguzi mkuu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
1761199663266.png

Takribani watu 20 wamekamatwa nchini Cameroon kuhusiana na maandamano yanayohusiana na uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, huku mvutano ukiendelea kuongezeka kabla ya matokeo rasmi kutangazwa wiki hii

Waziri wa Utawala wa Ndani, Paul Atanga Nji, amethibitisha kukamatwa kwa baadhi ya waandamanaji katika mji wa Garoua, kaskazini mwa nchi, akisema kwamba “wengi wao wamehusishwa na vitendo vya uchochezi na ghasia". Taarifa yake ilieleza kuwa watu 20 kati ya waliokamatwa watapelekwa mahakamani kijeshi kujibu mashtaka ya uchochezi na kuhamasisha uasi, huku wengine wakipelekwa Yaounde kwa uchunguzi zaidi.

Mvutano umeongezeka baada ya mgombea wa upinzani, Issa Tchiroma Bakary, kudai ushindi wiki iliyopita na kumtaka rais wa sasa Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, akubali matokeo. Chama cha Biya kimekanusha madai hayo na kumtuhumu Tchiroma kwa kujaribu kuvuruga mchakato wa uchaguzi

Soma Kiongozi wa Upinzani ajitangaza Mshindi wa Urais Cameroon, amuomba Rais Paul Biya akubali Matokeo

Baraza la Katiba linatarajiwa kutangaza matokeo rasmi ya mwisho siku ya Alhamisi, Oktoba 26, huku wachambuzi wengi wakitabiri ushindi kwa Biya kutokana na mgawanyiko ndani ya upinzani na marufuku ya mgombea wake mwenye nguvu zaidi.

Baada ya uchaguzi, maandamano yameripotiwa katika miji kadhaa kufuatia madai ya udanganyifu wa kura. Mashirika ya kiraia yameripoti kuwepo kwa “dosari nyingi,” ikiwemo kupigwa kura mara mbili, vituo kuhamishwa, na majina ya marehemu kuendelea kuwepo kwenye daftari la wapiga kura

Oktoba 20, 2025 Baraza la Maaskofu wa Katoliki la Cameroon ilisisitiza haki na amani katika katika mchakato mzima wa uchaguzi. Vilevile, mashirika manane ya kiraia yaliyochunguza uchaguzi huo yalibaini kuwa kulikuwa na ukosefu wa usawa katika usambazaji wa karatasi za kura na jaribio la kujaza masanduku ya kura

Soma Cameroon: Kanisa Katoliki latoa wito wa Haki na Amani

Hali ilizidi kuwa mbaya siku ya Oktoba 21, 2025, baada ya polisi kufyatua risasi na kumuua mwalimu wa kike katika eneo la Poumpoumre, Garoua, wakati walipokuwa wakitawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi. Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Lebledparle, mwalimu huyo alikuwa akirejea nyumbani kutoka kazini alipopigwa risasi

Waziri Nji amewataka raia kutulia na kuwa na imani na taasisi za uchaguzi, akionya kuwa serikali haitavumilia “jaribio lolote la uasi au kuvunja amani.”

Kwa sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (ELECAM) imesema kuwa imemaliza kuhesabu kura na matokeo ya awali yamekabidhiwa kwa Baraza la Katiba na Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba Biya anaongoza kwa zaidi ya asilimia 53 ya kura, ingawa matokeo rasmi bado yanangojea kuthibitishwa rasmi

Soma pia Rais Paul Biya anaongoza kwa 53% Matokeo ya awali Uchaguzi Cameroon

=============

At least 20 people have been arrested in Cameroon in connection with protests over the Oct. 12 presidential election, authorities said on Tuesday, as tensions mounted ahead of the proclamation of results expected later this week

Cameroon’s Minister of Territorial Administration, Paul Atanga Nji, confirmed the arrest of some of the protesters in the northern city of Garoua in a statement on Tuesday, without stating when and how many were arrested. Twenty of the “several” arrested will be brought before military courts to answer for the charges of insurrection and incitement to rebellion, the statement said, while others involved in criminal acts have been taken to Yaounde for further investigations

“The government watches with concern acts of provocation and disorder carried out by some trouble makers,” he said, claiming that those arrested were being manipulated by some political actors


Opposition candidate Issa Tchiroma Bakary claimed victory last week and urged President Paul Biya, the world’s oldest president at 92, to concede. Biya’s party has rejected Tchiroma’s claim of victory and accused the opposition candidate of trying to disrupt the electoral process. The constitutional council is expected to announce the final official results by Oct. 26

Source: Associated Press
 
Back
Top Bottom