Septemba 20, 2025 Waandamanaji wanaopigania demokrasia kutoka Eswatini walikusanyika nje ya Ubalozi wa Marekani jijini Pretoria wakipinga vikali taarifa za makubaliano kati ya serikali ya Marekani na utawala wa kifalme wa Eswatini. Mkataba huo unadaiwa kuruhusu wahamiaji waliorudishwa kurejeshwa nhini humo, hali ambayo waandamanaji walisema inalenga maslahi ya kifedha ya Mfalme Mswati III na si ya wananchi wa kawaida
Waandamanaji walimtuhumu mfalme kwa kupokea hadi dola milioni 500 (Takribani Trilioni 2.5 kwa fedha za Tanzania) kutoka Marekani bila msaada wowote kurudi kwa wananchi
“Eswatini ina kiwango cha pili cha juu cha vifo vya kujiua barani Afrika kutokana na umasikini na matatizo ya kijamii. Hata hivyo mfalme anaweza kupokea dola milioni 500, ambazo hazitawasaidia watu,” alisema mratibu wa maandamano Philile Khumalo.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Vijana wa Eswatini (Swaziland Youth Congress), Sakhile Nxumalo, alisema fedha hizo zitaimarisha tu nguvu za kifamilia za kifalme, na kuendeleza anasa za mfalme na wake zake 15 badala ya kushughulikia ukosefu wa ajira wa vijana unaofikia asilimia 58. Waandamanaji walisisitiza kuwa Marekani na Eswatini zinapaswa kufikiria upya makubaliano hayo na kuweka mbele ustawi na haki za wananchi wa Eswatin
Source: African news