Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Picha na AP.
Waandamanaji 10 wanaripotiwa kuuawa na polisi baada ya kuvamia jengo la Bunge la nchi hiyo na kuwashinda nguvu polisi.
Hali kwa sasa ni shwari kidogo baada ya polisi kuongeza nguvu ya idadi katika eneo hilo. Idadi ya watu wapatao 5o wamejeruhiwa na huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Sehemu moja ya jengo hilo la Bunge imeshika moto na moto huo bado waendelea.
Tukio hilo limetokea mara tu baada ya Bunge hilo kupitisha mswada wa sheria ya kodi inoongeza kodi katika bidhaa mbalimbali nchini huo.
Raisi Ruto amesema kuongeza kodi huko kutathibiti kukopa mikopo ambayo itaiathiri nchi hiyo kiuchumi.
Yadaiwa kuwa wabunge wengi walopitisha mswada huo wamepokea mlungula ili kurahisisha kupitishwa kwa muswaada huo ambao utaathiri wakenya wengi walo na kipato cha chini, wafanyabiashara na wachuuzi.
Picha na AP.
Kuna majeruhi wengi ambao wamejeruhiwa kwa risasi ambapo polisi waliamua kutumia nguvu na risasi halisi badala ya risasi za bandia au "rubber bullets".
Muswada huo uitwao Finance Bill 2024 umepitishwa leo asubuhi na wabunge kwa kura zipatazo 295 dhidi ya kura 106 huku kura tatu zikiharibika.
Chama cha Kwanza Alliance cha raisi Ruto kina wabunge wengi Bungeni na uwingi wao umerahisisha kupitishwa kwa mswada huo.
Mswada uo hivi sasa upo mezani kwa raisi Ruto ukingojea atie saini kuwa sheria rasmi.