Pre GE2025 Waandishi 2 kutoka Mwananchi Communications na 1 wa EATV wakamatwa na Jeshi la Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Waandishi wa Habari Wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na mmoja wa EATV wamekamatwa na Jeshi la Polisi walipokuwa wakiripoti katika #Maandamano ya Amani yaliyoitishwa na CHADEMA.

Waandishi wa MCL waliokamatwa ni Michael Matemanga aliyekamatiwa Msimbazi na Lawrence Mnubi aliyekamatiwa Buguruni, Mariam Shabani (EATV) amekamatwa akiwa eneo la Ilala Boma

Imeelezwa Michael ameachiwa huru huku Lawrence na Mariam wakiendelea kushikiliwa

Soma pia: Waziri Nape astushwa Waandishi wa Mwananchi kushambuliwa na Watu Wasiojulikana, alaani na kuagiza Polisi Wawasake!
 
Kila mtu alaani kitendo cha kukamatwakamatwa kwa waandishi wa habari, sababu kukamatwa kwao tunanyimwa haki yetu ya kupata habari, maana waandishi kazi yao inajulikana ni kutupasha habari, si kuandamana, hata jeshi la Polisi linao waandishi wa habari.
 
Waandishi wa Habari Wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na mmoja wa EATV wamekamatwa na Jeshi la Polisi walipokuwa wakiripoti katika #Maandamano ya Amani yaliyoitishwa na CHADEMA.

Waandishi wa MCL waliokamatwa ni Michael Matemanga aliyekamatiwa Msimbazi na Lawrence Mnubi aliyekamatiwa Buguruni, Mariam Shabani (EATV) amekamatwa akiwa eneo la Ilala Boma

Imeelezwa Michael ameachiwa huru huku Lawrence na Mariam wakiendelea kushikiliwa

Soma pia: Waziri Nape astushwa Waandishi wa Mwananchi kushambuliwa na Watu Wasiojulikana, alaani na kuagiza Polisi Wawasake!
Kuna wakati ndugu zangu hawa walinda raia huwa wanatangaza na kukipa airtime kitu ambacho kimsingi walitakiwa kuzuia hata kusikika kwake. Sasa hapa wametengeneza mgogoro na matangazo yasiyo na ulaima wowote. Hivi kweli hawaoni hili au ni mimi tu na ukilaza wangu ndio natafsiri hivi?
 
Back
Top Bottom