Waandishi Habari Kuanza Kusajiliwa Mei

Waandishi Habari Kuanza Kusajiliwa Mei

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema inatarajia kuanza utaratibu wa kusajili waandishi wa habari kupitia mfumo wa kidijitali ifikapo mwanzoni mwa mwezi Mei, 2025.

487125388_18367111615193410_2278497960947774490_n.jpg

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na na bodi hiyo kwa kushirikiana na idara ya Habari Maelezo imeeleza kuwa ukamilishaji wa mfumo huo utakaotumika kwaajili ya usajili unaendelea kwa mafanikio.

Aidha taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo Patrick Kipangula imeeleza kuwa mfumo huo unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili.

Kadhalika imeeleza kuwa baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali yanayolenga kuimarisha zaidi uasalama, ubora, ufanisi na wenye kukidhi mahitaji imebidi kuongeza muda wa ukamilishaji wake.
 
Labda wasajili walioajiriwa tu. Waandishi wa kujitegemea mara uandike, mara uache kuandika kutokana na malipo duni huo usajili utasaidia nini kama certificate inaishia kutambuliwa tu ila haitasajiliwa mpaka uwe na diploma na kuendelea?
 
Mkuu kuna haja cerficates isifanyiwe usajili angalau hata diploma .........
 
Mkuu kuna haja cerficates isifanyiwe usajili angalau hata diploma .........
utakuta mwandishi ana certificate na amefanya kazi vema muda mrefu, kuweka vigezo vya diploma na degree ndio usajiliwe hii haitakaa vizuri. Bodi ya ithibati wangesajili na certificate tu, habari ya kujiendeleza kwa ngazi inayofuata iwe ni hiari tu kwa mwandishi kutaka apandishiwe mshahara na kupata maarifa zaidi
 
Eddo Kumwembe
JOSE mara
Swebe Nunda
Mauldi Baraka wa Kitenge
Wapuuzi wote wapiga kelele wajiandae kuliwa vichwa.
 
Eddo Kumwembe
JOSE mara
Swebe Nunda
Mauldi Baraka wa Kitenge
Wapuuzi wote wapiga kelele wajiandae kuliwa vichwa.
Kama Edo Kumwembe umemuweka kwenye kundi la Waandishi wa Habari basi tunaiomba Serikali Elimu izidi kutolewa.
 
Kama Edo Kumwembe umemuweka kwenye kundi la Waandishi wa Habari basi tunaiomba Serikali Elimu izidi kutolewa.
Nimemuweka hapo sababu sio Mwandishi wa habari hao kama sheria itafuatwa hatawasikika tena.
 
Back
Top Bottom